Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  23 Jumada II 1439 Na: 1439/015
M.  Jumapili, 11 Machi 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Kwa Kukosekana Khilafah Wanawake Waheshimiwa wa Ash-Sham Wanakabiliwa na Kudhulumiwa Hata na Wale Wanaodai Kuwa Walinzi Wao!!!

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa linalo shughulikia ufadhili wa watu (UNFPA) limesema kuwa wanawake katika kambi za wakimbizi nchini Syria wamekuwa wakidhulumiwa kimapenzi na wanaume wanaotoa misaada kwa niaba ya UM na mashirika ya kimisaada ya kimataifa. Ripoti hiyo, “Sauti kutoka Syria 2018”, ili eleza kwa kina namna wanawake wakimbizi wa Syria wanavyo lazimishwa kutoa ngono kama badali kwa chakula kutoka UM, na kwamba dhulma hii imeenea maeneo yote kusini mwa Syria. Wafanyikazi wa misaada wameelezea namna ambavyo msaada wa kibinadamu aghalabu huweza kuzuiwa kwa wanawake hawa wenye papatiko isipokuwa wakubali kutimiza matilaba haya ya ngono, na kwamba tatizo hili limeenea mno kiasi ya kuwa baadhi ya wanawake wa Syria hukataa kwenda katika vituo vya ugawanyaji misaada kwa kuhofia kudhaniwa na watu kuwa wametoa miili yao kwa ajili ya misaada waliyo pokea. Dhulma hii ya kimapenzi imeendelea licha ya onyo kutoka kwa UM na mashirika ya kimisaada miaka mitatu iliyopita. Mnamo Juni 2015, Kamati ya Kimataifa ya Uokozi (IRC) iliwahoji wanawake na wasichana 190 mjini Dara’a na Quneitra na kupata kuwa asilimia 40% wamepitia dhulma za kimapenzi walipokuwa wakijaribu kufikia misaada. Matokea haya ya ripoti yake yaliwasilishwa katika mkutano wa mashirika ya UM nchini Jordan mwaka huo, huku dhulma kwa wanawake wakimbizi wa Syria ikiendelea. Danielle Spencer, mfanyikazi wa misaada na mshauri wa maswala ya kibinadamu, aliliambia shirika la habari la BBC kuwa anaamini kuwa baadhi ya mashirika ya kibiashara yanaifungia macho dhulma hii. Alisema, “Dhulma za kimapenzi na unyanyasaji wa wanawake na wasichana zimepuuzwa, zinajulikana lakini zimepuuzwa kwa miaka saba… UM na nidhamu iliyopo kwa sasa zimechagua miili ya wanawake kutolewa sadaka… huenda kuna uamuzi uliofanywa kuwa ni sawa kwa miili ya wanawake kuendelea kutumiwa, kudhulumiwa, na kunyanyaswa ili misaada ipeanwe kwa kundi kubwa zaidi la watu.”

Dada zetu wapendwa, waheshimiwa wa Ash-Sham waliponea kutokana na risasi, mabomu, njaa na dhulma za majeshi ya wahalifu ya Assad, huku wakiangukia unyanyasaji wa wale wanaodai kuwasaidia na kuwanusuru. Dada zetu walio hatarini na wenye papatiko hawaishi tu katika hali mbaya za kinyama ndani ya kambi hizi za ‘mauti’ za wakimbizi, bali kutokana na ripoti hizi ni dhahiri kuwa hawawezi kufikia hata misaada msingi, ikiwemo chakula pasi na tishio la heshima yao kukiukwa. Vile vile ni dalili zaidi kuwa UM, mashirika mengine ya kimisaada na serikali za ulimwengu wa Kiislamu haziwezi kuaminiwa kusimamia maslahi ya dada zetu wapendwa. Badala yake wameonesha kuwa kulinda heshima yao sio kipaumbele machoni mwao.  

Kwa kweli, kwa kukosekana uongozi wa Kiislamu wa Khilafah katika njia ya Utume, hakuna usalama kila mahali kwa wanawake waheshimiwa wa Ash-Sham, na hawana pa kukimbilia hifadhi, ulinzi na maisha ya utu. Hakika, hakuna dola nyengine yoyote isipokuwa Khilafah, inayotawaliwa kwa sharia za Allah (swt) inayoitazama heshima ya wanawake wake kwa upeo mkubwa, ikiweka ulinzi wake katika kiwango sawia na ulinzi wa maisha yenyewe, na kumuadhibu vikali yeyote anaye jaribu hata kutoa neno tu la kuikiuka! Mtume (saw) yeye mwenyewe, kama mtawala wa dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina, alilifurusha kabila zima la Kiyahudi la Banu Qaynuqa kwa kumvunjia heshima mwanamke wa Kiislamu. Khalifah mtukufu wa Kiabasiyya, Al-Mu’tassim Billah, alipeleka jeshi kubwa lenye nguvu mpaka mji wa Amurriyah nchini Uturuki, eneo lenye ngome imara ya Kirumi, kumuokoa mwanamke mmoja wa Kiislamu aliye nyanyaswa na mwanajeshi wa Kirumi, japokuwa makao makuu ya Khilafah yalikuwepo jijini Baghdad wakati huo. Huu ndio urithi usiokuwa na mfanowe wa hadhi kubwa ya heshima ambayo uongozi huu halisi wa Kiislamu wa Khilafah unaweza kuwapa wanawake wake pamoja na hisia kuu ya utekelezaji majukumu kutoka kwa viongozi wake kuwahifadhi kutokana na madhara yoyote. Tunawalingania Waislamu, na hususan wale walioko katika majeshi ya Waislamu ambao Allah (swt) amewakabidhi nguvu za kijeshi, kusimamisha kwa haraka dola hii tukufu ya Khilafah ambayo pekee ndio inayo weza kuaminiwa kulinda hadhi, ufanisi na utulivu wa wanawake.  

وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Allah amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu, na kufanya mema, atawafanya makhalifa katika ardhi, kama alivyo wafanya makhalifa waliokuwa kabla yao, na atawamakinishia dini yao aliyo waridhia (Uislamu). Na atawabadilishia baada ya hofu yao usalama, wataniabudu Mimi wala hawatanishirikisha na kitu chochote, na yeyote atakaye kufuru baada ya hapo, basi hao ndio mafasiki (waovu)” An-Nur: 55]

Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu