Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  26 Jumada I 1439 Na: 1439/010
M.  Jumatatu, 12 Februari 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Makongamano ya Kimataifa, Mipango ya Amani, Pasi na Kukomesha Wala Kupunguza Mashambulizi ya Mabomu ya Urusi!
(Imetafsiriwa)

Matukio ya umwagikaji damu yanayojiri Mashariki mwa Ghouta na Idlib; Mtandao wa Kutetea Haki za Kibinadamu wa Syria umesema kwamba raia wapatao 370 wameuwawa Mashariki mwa Ghouta tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ukitaja kuwa miongoni mwa wafu ni watoto 63 na wanawake 72. Katika eneo la Idlib, hususan mji wa Sarakib, ambao ndio uliolengwa kwa dhoruba hii tangu mnamo 25 Disemba, Warusi na serikali ya kihalifu ya Syria zimemwaga chuki zake dhidi yake, ikitangazwa na baraza lake la mji kuwa eneo lililo kabiliwa na janga, ambapo idadi ya vifo mwezi Januari ilikuwa ni watu wapatao 30 na zaidi ya raia 60 kujeruhiwa. Hii ni ikiongezewa na kulengwa kwa mashule na mahospitali, ambazo idadi yake kubwa haziendeshi tena shughuli zake.

Tangu kutokea kwa mapinduzi ya Syria mnamo 2011, mipango kadha wa kadha ya kiarabu na ya kimataifa imefanywa, lengo lake linalodaiwa ni kufikia suluhisho la amani la mzozo huu! Ni vipi itasemwa kuwa ni suluhisho la amani, huku likiwa linafanywa juu ya maiti za watoto na damu za wasiokuwa na hatia. Mashambulizi ya kuendelea kutosaza kitu, na uchinjaji ukiendelea kuchukua maisha zaidi ya raia kila uchao?!

Miaka mingi ya makongamano yaliyo feli yaliyo lenga kutia jivu machoni mwa rai jumla, kuanzia kwa makongamano ya Geneva yaliyo malizika kwa kujiuzulu kwa Lakhdar Brahimi baada ya kumrithi Kofi Annan na mahali pake kuchukuliwa na Steffan de Mistura, mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria mnamo Julai 2014; kisha mazungumzo jijini Vienna, yaliyo anza awamu zake mnamo Novemba 2015, baada ya uingiliaji wa kijeshi wa Urusi nchini Syria kuisaidia serikali hii mwishoni mwa mwezi Septemba na uliomalizika mnamo 26 Januari 2018 baada ya zaidi ya awamu tisa za kimataifa, zilizo sababisha mauwaji zaidi, mahangaiko na ukosefu wa makao.     

Hatujasahau majadiliano ya Astana, yaliyo pelekea makubaliano juu ya kubuniwa kwa maeneo manne ya kuhafifisha na kupunguza mapigano na wala si kusitisha mapigano yote kwa jumla, ikiwemo katika eneo la Idlib, ambalo leo linashambuliwa kwa chuki ya hali ya juu. Silsila ya mwisho (ya khiyana) ya aina hiyo ilikuwa ni kongamano lililo fanywa mnamo 30 Januari 2018 eneo la Sochi kupitia mualiko wa Urusi, lililo pendekeza kubuniwa kwa kamati ya kuiandika upya katiba ya Syria na kutoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi wa kidemokrasia.

Makongamano na mipango imeendelea kufanyika kwa miaka yote hii kwa madai ya lengo la kuleta amani, huku ndege za kivita za Urusi na mashambulizi ya angani yakikosa kusita au kupungua. Haya ni majadiliano ambayo hayakulenga wala hayatalenga kuipindua serikali hii katili bali yanalenga kupindua azma ya watu wa Syria wenye ikhlasi na kurefusha muda wa jambazi Bashar na washirika wake kuendelea kunajisi mikono yao kwa damu za raia, na kuwahangaisha na kuwakosesha makao. 

Miaka saba ya vita uchungu vilivyo anzishwa na serikali hii na washirika wake katika maeneo kadha wa kadha ya waasi nchini Syria, na miaka mitano ya uvamizi wa kinyama katika eneo la Mashariki mwa Ghouta, ambalo kwa sasa ndilo lililo bakia na ndio ngome kubwa zaidi ya upinzani, na tunachosikia ni mipango na miito ya kimataifa pekee juu ya haja ya kusitisha mapigano ili kuruhusu kutolewa kwa misaada ya kibinadamu, kana kwamba yanayo tendeka hayako chini ya usimamizi wa nguvu hii katili ya kimataifa! Na kana kwamba yanayo tendeka yanahitaji tu kutumwa kwa vyakula na mablanketi, na lakini kutoka kwa nani?! Kutoka kwa muuwaji au wale walioshiriki na kumsaidia katika kumwaga damu ya watu wa Syria wasiokuwa na hatia!

Je, sauti za kuomboleza na vilio zilizo enea kote nchini Syria hazijayafikia masikio ya wale wanaopeleka majeshi yao kwa utiifu kwa mabwana zao katika michezo iliyo andaliwa kabla?! Je, watawala hawa makhaini hawaja tambua bado kwamba Umma wa Kiislamu umewakufuru wao na mipango yao tasa?!

Hivyo basi, Enyi Waislamu, wang'oeni watawala wenu makhaini, na muiunge mkono Dini ya Allah kwa kuifanya itawale dunia kwa uadilifu na ile amani ya kweli inayotarajiwa iweze kupatikana, kupitia kubanduliwa kwa ukafiri na wapambe wake na kuondosha batili na kuishinda kote ulimwenguni. Mwenye Nguvu (swt) Asema :

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ)

“Enyi Mulio amini mukimnusuru Allah Naye atawanusuru na ataithibitisha miguu yenu. Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atazipoteza amali zao.”  [Muhammad: 7-8]

Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu