Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Covid-19 Janga la Kupangiliwa: Fursa ya Kuwakandamiza, Kuwapora na Kuwahofisha Wanadamu

Habari:

Serikali duniani kote zinashughulika hivi sasa kuweka mikakati ya kikatili ili kudhibiti kuenea kwa aina mpya ya Virusi vya Ugonjwa wa Korona vya 2019 kwa jina Omicron.

Maoni:

Tangu kutokea kwa mkurupuko wa janga la kupangiliwa mnamo mwanzoni mwa 2019 hadi sasa mwenendo wa maisha ya wanadamu yamebakia kupinduliwa juu chini. Maamuzi yasioingia akilini yenye ushawishi wa makampuni machache yanaendelea kusababisha matatizo ulimwenguni kote. Makampuni hayo yameasisiwa juu ya msingi mmoja muhimu nao ni kupatiliza matatizo ya watu ili kujilimbikizia faida kupitia kutunga na kutekeleza sheria na sera zenye mashaka kwa jina kupambana na janga la kupangiliwa la Covid-19.

Makampuni hayo yamekazanisha vitanzi vyao juu ya miundo mbinu ya afya ulimwenuni kote kiasi kwamba hakuna kiongozi wa serikali anayeweza kuwauliza swali pasina na kutarajia kushambuliwa kwa madhara. Hivyo basi, asasi za serikali ulimwenguni zinayasifu makampuni hayo katika juhudi zao za kutengeneza na kusafirisha chanjo. Haishangazi kwamba wale wanaodhaniwa kuwa ni vikwazo hung’olewa kwa haraka kutoka madarakani kwa kutumia njia yoyote ile, kwani lengo huhalalisha njia!

Serikali ambazo zilidai kuwa zinafurahia ubwana na uhuru usiokuwa na mipaka zimejipata kuwa zinatumika kama vikaragosi na makampuni hayo. Kwa kuwakandamiza raia zao kupitia kuwafungia, kuwapora kupitia kutumia rasilimali za umma katika kununua chanjo ambazo uwezo wake unatiliwa shaka na athari zake mbaya zikowazi kabisa. Kwa kuongezea wale ambao wamekataa kuchukua chanjo hizo wanadunishwa na kuhofishwa kwa kunyimwa huduma na wengine kutishiwa kuwa watafutwa kazi miongoni mwa dhulma nyinginezo.

Janga la kupangiliwa la Covid-19 ni ajenda ambayo lengo lake msingi ni kuleta mabadiliko hadaifu kupitia kupangilia upya nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii ambayo matokeo yake yanajulikana pekee na makampuni yaliyochochea. Wenye nguvu na wasiokuwa na nguvu wote wamemezwa na njama ovu na za kilafi za kipote cha watu wachache wanaodai kuwa wanawajali wanadamu. Alas! Wanachojali zaidi ni kuwaangamiza wanadamu kwa kutia faida kupitia shida zao.

Wakati ni sasa kwa kila mtu mwenye akili timamu kuungana na kusema LA kwa hizi sheria na sera nyingi zisizoingia akilini za kikatili ambazo zinayakaba maisha yetu. Kwa kusimama pamoja ni hatua katika mwelekeo sahihi kwa kuziambia serikali zetu kwamba imetosha kufanya biashara na makampuni yaliyo na njaa ya faida. Kwa kuongezea, tutakuwa tunayaambia makampuni yanayo furahia ulinzi wa kisheria kutokamana na bidhaa wanazozitengeza kwamba SISI SIO WANYAMA WA KUTUMIKA KATIKA MAJARIBIO!

Kimsingi, lazima tujifunge na ulinganizi wa kurudisha tena Khilafah kwa njia ya Utume. Kutokuwepo kwa Khilafah kumetoa mwanya kwa makampuni haya kuwepo na kuhangaisha wanadamu. Kwa kuongezea, kuwepo kwao kunaungwa mkono na viongozi wa kirasilimali wa kisekula ambao wameziuza roho zao kwa shetani kwa malipo ya vijipesa wanavyopewa na makampuni hayo.

Khilafah ni ngao na mlinzi ambaye kuwepo kwake ni kwa ajili ya kutekeleza Shari’ah ya Kiislamu ambayo vyanzo vyake ni Qur’an, Sunnah, Makubaliano ya Maswahaba na Qiyas. Hivyo basi, msingi wa ujenzi wake na kipimo cha vitendo vya wanadamu utakuwa ni Halal na Haram, na sio faida au hasara. Kwa msingi huo Khilafah haitokubali kuwepo kwa majanga ya kupangiliwa katika himaya yake. Hata hivyo, kunapotokea janga itakwenda mbio kukabiliana nalo na sio kunufaika kupitia kwake kwa kushirikiana na baadhi ya washikadau katika sekta ya afya kama inavyohushudiwa hivi sasa. Kwani utafiti huru unaendelea kuthibitisha kwamba Covid-19 ni janga la kupangiliwa na SIO janga kama inavyodaiwa na wanaotia faida ambao wanatumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kueneza uongo wao ili kupata mauzo zaidi!

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu