Ijumaa, 06 Rajab 1444 | 2023/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Muungano wa Ulaya Wajaribu Kuokoa “Mkataba wa Nyuklia” na Iran

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 4 Agosti 2022, mkutano wa wawakilishi wa nchi zinazoshiriki katika Mpango Kamili wa Pamoja wa Utendakazi (JCPOA) umepangwa kufanyika jijini Vienna. JCPOA - makubaliano ya kisiasa kati ya Iran na lile linachoitwa kundi la 5+1, ambalo linajumuisha wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (Marekani, Urusi, China, Uingereza, Ufaransa) na Ujerumani.

Kama mpatanishi, Muungano wa Ulaya pia unapanga kushiriki katika jaribio jengine la kuokoa makubaliano ya 2015, yanayojulikana kama "mkataba wa nyuklia".

Muungano wa Ulaya unafanya msukumo wa mwisho kuokoa mkataba wa nyuklia ya Iran kwa kuwaita wapatanishi wote pamoja kurudi ghafla na kwa haraka kwenye mazungumzo.

Afisa mmoja wa Marekani anayefahamu suala hilo alithibitisha kuwa mjumbe maalum wa Marekani kwa Iran Rob Malley atahudhuria mazungumzo hayo. (Chanzo: https://www.politico.eu/article/iran-nuclear-talk-resume-thursday/)

Maoni:

Wasiwasi kuhusu maendeleo ya mpango wa nyuklia wa Iran ni kisingizio cha uwongo katika mapambano ya Marekani na mahasimu wake wa kisiasa na kijiografia kwa ajili ya kumiliki hifadhi kubwa ya mafuta na gesi ya Iran. Utawala wa Iran daima umedumisha na unaendelea kushikilia kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani na kwamba hautazalisha bomu la atomiki. Licha ya hayo, dola kubwa za kibepari za Kimagharibi zikiongozwa na Marekani zinauchukulia uwezekano tu wa Iran kupata uwezo wa kuunda silaha za nyuklia kuwa ni moja ya vitisho vikuu katika ajenda ya matatizo ya ulimwengu.

"Tishio la nyuklia" pamoja na "maneno ya kijeshi dhidi ya Magharibi na Israel" imekuwa ni sababu ya kutabanniwa kwa idadi kadhaa ya maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kuwekewa vikwazo dhidi ya Iran. Havikufungika tu na kugandisha mali za kigeni na kunyimwa kufikia teknolojia na vifaa vya uchimbaji, uboreshaji na usindikaji wa urania. Pia iliharamishwa kumuuzia silaha nzito na kitu chochote ambacho kingeweza kuchangia kuundwa kwa makombora ya balestiki yenye uwezo wa kubeba chaji za nyuklia.

Uharibifu mkubwa zaidi kwa uchumi wa Iran ulitokana na kuzuiwa kwa uagizaji wa mafuta kutoka Iran. Baada ya yote, uuzaji wa mafuta na gesi hutoa robo tatu ya mapato ya fedha za kigeni kwa bajeti yake. Licha ya "takhsisi kwa madhumuni ya kibinadamu na shughuli halali za kiuchumi" iliyotangazwa katika maazimio hayo, mgogoro wa kiuchumi uliofuata vikwazo ulisababisha umasikini kwa idadi kubwa ya Wairani, na mamilioni ya Wairani walikuwa kwenye ukingo wa njaa.

Vikwazo hivyo, ambavyo vilipunguza upatikanaji wa mafuta ya bei nafuu ya Iran, vimesababisha matatizo ya kiuchumi katika maeneo mengine duniani, ikiwa ni pamoja na katika nchi za Ulaya zilizoendelea kiviwanda zinazotegemea usambazaji wa nishati. Kwa hiyo, walifanya majaribio ya kutafuta njia za kukwepa au kuondoa vikwazo kutoka Iran. Mojawapo ya masuluhisho hayo ya kulegeza msimamo ni makubaliano ya kisiasa ya 14 Julai 2015 kati ya Iran na kundi la dola zinayojulikana kama 5+1, yaitwayo Mpango Kamili wa Pamoja wa Utendakazi (JCPOA), ambapo baada ya uhitimishwaji na utekelezwaji wa mwisho vikwazo vya Marekani vingeweza kuondolewa kutoka Iran, Muungano wa Ulaya na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Makubaliano hayo yaliitaka Iran kuweko kidhibiti hifadhi yake ya urania na uwezo wake wa urutubishaji, pamoja na IAEA kufikia vituo vyote vya nyuklia na udhibiti kamili wa mtandaoni wa matumizi ya nyenzo za mionzi kwa madhumuni ya amani pekee. Yalitaka pia kwamba Muungano wa Ulaya na Marekani zijiepushe na vikwazo dhidi ya Iran, ambavyo kurudiwa kwake au kuletwa upya kutazingatiwa na wao "kama msingi wa kusitisha utimizaji wa majukumu yao kwa jumla au kwa sehemu fulani."

Mnamo Oktoba 2017, Rais wa zamani wa Marekani Trump alitangaza kuwa hatalihakikishia tena Bunge la Congress kwamba JCPOA liko kwa maslahi ya Marekani, na mnamo tarehe 8 Mei 2018 alitangaza kujiondoa kwa nchi yake katika makubaliano hayo. Akisema kuwa Marekani ina ushahidi kuwa Iran inaendelea kutengeneza silaha za nyuklia, Trump alitangaza mipango ya kuregesha vikwazo dhidi ya Tehran. Kwa kujibu, Iran ilitangaza kujiondoa kwa hatua kutoka kwa mkataba huo na ujenzi wa kizazi kipya cha centrifuges ili kuongeza hifadhi ya urania na kuirutubisha juu ya kiwango kilichowekwa na mkataba wa nyuklia. Viongozi wa nchi za Ulaya wanaoshiriki katika makubaliano hayo walieleza masikitiko yao kwa kung'atuka kwa Trump na kubainisha kwamba JCPOA sio makubaliano ya pande mbili kati ya Marekani na Iran, walitoa wito kwa Tehran kuendelee kujitolea kwa ajili ya makubaliano hayo.

Kwa ujio wa utawala wa Biden katika Ikulu ya White House, Marekani iliregea kushiriki katika JCPOA. Hata hivyo, kwa kuzingatia maneno ya mwakilishi wa Marekani kwamba "matarajio yao ni ya kawaida", na pia kupitia taarifa za mwakilishi wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran kuhusu uanzishaji wa mamia ya mashini mpya na zilizoboreshwa za centrifuge, makubaliano ya JCPOA yanaelekea kufeli.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abu Ibrahim Bilal
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu