Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hakuna Kikomo kwa Unyama na Chuki za Kikatili za Wazayuni

(Imetafsiriwa)

Habari:

Tangu tarehe 5 Agosti 2022, Ijumaa hii iliyopita, umbile la Kizayuni kwa mara nyingine tena limefanya mashambulizi ya angani dhidi ya Gaza na kuua makumi, wakiwemo kwa uchache watoto 15 na kujeruhi mamia. Wakati huo huo walowezi wa Kizayuni kwa mamia waliolindwa na Vikosi vya Uvamizi, walivamia Msikiti wa Al-Aqsa mnamo tarehe 7 Agosti, wakiimba nyimbo za chuki dhidi ya Uislamu na kumtusi Mtume Muhammad (saw).

Maoni:

Wazayuni hao kwa mara nyingine tena wanaweka wazi kwa walimwengu mzima kuona kwamba hakuna kikomo kwa ukatili na chuki zao za kinyama dhidi ya Waislamu wa Palestina. Wauaji hawa wa watoto wanahisi kuwa salama katika maovu yao dhidi ya kila kitu kilicho kitakatifu, kwa sababu wanajua kwamba vituo vya amri huko Cairo, Amman, Ankara, Riyadh na Tehran viko mikononi mwa wasaliti waoga wasiojali hata kidogo damu ya wasio na hatia. Watumwa hawa wa Magharibi hawajali chochote kwa Msikiti wa Al-Aqsa, ili mradi mabwana zao wa kikoloni wameridhika nao. Kwa kuzingatia matukio ya hivi punde, yafuatayo lazima yabaki kuwa lengo la wale wote wanaotaka kuwanusuru kaka na dada zetu huko Gaza na Palestina kwa jumla:

Wahisabuni watawala hawa wasaliti kwa kutotenda na kuwa washirika. Watawala hawa ndio "Jeshi halisi la Ulinzi la Israel" , bila ya ulinzi wao, umbile la Kizayuni halingebakia kwa muda mrefu. Wakati watawala hawa wamekaa bila kuchukua hatua bila kutikisika huku damu za watoto wa Kiislamu zikichuruzika, wanatuma vikosi vyao kwenda kuwaua Waislamu nchini Yemen, Syria na nchi nyenginezo, pale inapotumikia maslahi ya mabwana zao wakoloni wa  Kimagharibi. Watawala hawa hawana hawastahiki utiifu halali wa Waislamu bali wanapaswa kulaaniwa na kuhisabiwa kwa mujibu wa viwango vya Kiislamu.

Kataeni njama zote za kuhalalisha uvamizi wa Wazayuni na kuisalimisha Palestina. Mazungumzo yoyote yanayolenga kuhalalisha uvamizi huo si chochote ila ni majaribio ya kuwafanya Waislamu waihalalishe "Israel" na kujisalimisha kwa mpango wa kikoloni wa kuitoa Palestina kutoka kitovu cha ardhi za Waislamu. Katika miaka ya hivi majuzi tumeshuhudia juhudi mpya za uhalalishaji mahusiano wa dola kadhaa za kitaifa za kisaliti za Kiarabu. Huku Umma wa Kiislamu kwa ujumla umekataa juhudi hizi, baadhi ya "mashekhe" na wengine wanaodai kuwa "wabebaji da’wah" wameshiriki katika juhudi hizi za uhalalishaji. Tabia kama hiyo lazima iitwe usaliti. Hatuwezi kukubaliana na shinikizo au uongo uliopakwa asali bali ni lazima tusimame kidete juu ya ukinaifu wetu wa Kiislamu unaoharamisha kupeana hata shubiri moja ya ardhi ya Waislamu, katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina au kwengineko. Dola ya kitaifa ya Palestina kwa msingi wa mipaka ya kabla au baada ya 1967 itakuwa ni utambuzi na uhalalishaji wa uvamizi wa kimabavu wa ardhi ya Waislamu.

Kataeni uingiliaji kati wa Magharibi, iwe ni dola kubwa za kikoloni, hasa Marekani, ambayo kwa mara nyengine tena imetangaza uungaji mkono wake usio na masharti kwa uvamizi wa Kizayuni wa Palestina na uhalifu usioelezeka dhidi ya watu wake, au kile kinachoitwa "jamii ya kimataifa" na mashirika yake, kama vile Umoja wa Mataifa, ambayo ilikuwa ni taasisi hii hii ambayo kwayo “Israeli” iliasisiwa hapo kwanza. Masuluhisho ya Kimagharibi kwa matatizo ya Umma wa Kiislamu, likiwemo suala la Palestina, yanalenga tu kuhifadhi hali tete iliyopo na kuuweka Umma wa Kiislamu katika hali ya udhaifu na utumwa kwa Magharibi. Kimsingi uvamizi wa Wazayuni wa Palestina si chochote zaidi ya kuwa ni mstari wa mbele katika vita vya wakoloni wa Kimagharibi dhidi ya Umma wa Kiislamu. Uingiliaji wowote wa Magharibi kwa hivyo unakataliwa, kwa mtazamo wa Kiislamu, na uzoefu wote unasisitiza ukweli kwamba uingiliaji wa Kimagharibi katika Ardhi za Kiislamu unapelekea tu kwenye umwagaji damu zaidi na udhalilifu, maadamu Umma unakataa kuisujudia Magharibi badala ya Mwenyezi Mungu.

Wito kwa majeshi ya Waislamu wajipange. Hakuna kiasi cha ushawishi, maandamano, au kususia chenyewe pekee kitakomesha uvamizi wa umwagaji damu. Licha ya kuwa vitendo hivi vinafanywa kwa nia safi na Waislamu wengi, ukweli wa mambo ni kwamba suluhisho la kijeshi ni muhimu ili kutatua suala la uvamizi wa kijeshi. Ili kuyaweka mbali majeshi ya Kiislamu na Ummah wao na wajibu wao, mara nyingi tunawasikia wakosoaji wakiuliza kwa nini Waislamu wasio na mafunzo, silaha, nguvu za kimwili au uwezo, hawaendi kupigana na uvamizi nchini Palestina na kwengineko. Wakati huo huo majeshi yametulia tuli ndani ya kambi zao, wakati kihakika wao ndio vikosi hasa vya Ummah huu vilivyo na uwezo wa kivitendo wa kuondoa uvamizi huo. Kupitia Sunnah ya kipenzi chetu Mtume (saw), tunajifunza kwamba Muislamu anapojikuta hawezi kubadili uovu kwa mikono yake mwenyewe, ni lazima awaite kwa ulimi wake wale wenye uwezo. Katika siku hizi za mwezi wa Muharram, ambapo tunafunga siku ya Ashura na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukumbuka ushindi wa Musa (as) dhidi ya Firauni, hatupaswi kupoteza matumaini katika ushindi wa Mwenyezi Mungu au Umma wetu wenyewe bali tuwe na imani kamili kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu na ushindi wa karibu, ambao maadui wa Uislamu hawatapata pa kukimbia!

Simamisheni Khilafah, ikomboeni Palestina na ardhi nyengine zote za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu. Hakuna chombo chengine cha kisiasa isipokuwa Khilafah Rashida kitakachozikomboa ardhi za Kiislamu kutoka kwa maadui, kutuunganisha baada ya mgawanyiko wetu, kututia nguvu baada ya udhaifu wetu, kutawala kwa huruma na uadilifu wa Uislamu na kueneza nuru yake duniani baada ya kugubikwa na giza la urasilimali na unyonyaji wa wakoloni. Nusuruni ulinganizi wa kiulimwengu wa kuisimamisha tena huku mukitafuta radhi za Mwenyezi Mungu, na kazi yenu itazaa matunda yenye baraka katika maisha haya na Akhera.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Elias Lamrabet

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu