Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kuegemea Upande wa Dhalimu Kwapelekea Usaliti kwa Wanaodhulumiwa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wakati Waziri wa Mambo ya Nje, Cavusoglu akijibu maswali ya waandishi wa habari katika siku ya mwisho ya Mkutano wa 13 wa Mabalozi uliofanyika jijini Ankara, ambayo ilikuwa ni jana, alisema: "Tunahitaji kuleta upinzani na utawala pamoja kwa maridhiano kwa namna yoyote, vyenginevyo hakutakuwa na amani ya kudumu. Hivyo ndivyo tunavyosema siku zote".

Cavusoglu, aliyesema kwamba alikuwa na mazungumzo ya haraka na mwenzake wa Syria Faisal Mekdad wakati wa mkutano wa Harakati Isiyofungamana na upande wowote mnamo Oktoba 2021 katika mji mkuu wa Serbia Belgrade, alisema kwamba pia aliwasilisha mawazo yake wakati wa mkutano huu. (Mashirika 12.07.2022)

Maoni:

Japokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) anataja katika hadith zake nyingi ulazima wa kuondosha ukatili, ubaya na uovu wake, watu wachafu walio na shauku ya kufanya kinyume chake, hasa wale wanaoshikilia utawala, kwa bahati mbaya wanazidi kuwa wabaya.

«اتَّقُوا الظُّلْمَ فَإِنَّ الظُّلْمَ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ»

“Iogopeni dhulma, kwani hakika dhulma ni giza Siku ya Kiyama ...”

Ni makubaliano ya aina gani, ni amani ya aina gani inayoweza kufanywa mazimwi wakali ambao wamekuwa wakichinja mamilioni ya Waislamu kwa miaka 11 kwa mbinu za kikatili zaidi ambazo hazijawahi kushuhudiwa katika historia na kuwafanya wawe wakimbizi, ambao wamekanyaga hadhi ya binadamu kwa mateso yasiyofikirika, ambao wamekuwa duni zaidi kupitia ubakaji na ukatili na ambao wameonyesha kilele cha unyama kwa kuharibu miji?!

Wakati mateso na mauaji haya yakifanywa dhidi ya Waislamu, wale wanaowaunga mkono moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja wauaji hawa ni washirika wa dhambi hilo hilo. Tena, ni kielelezo tosha cha unafiki kwamba wale wanaotumia majeshi yao ardhini kutumikia maslahi ya kisiasa ya Marekani wanazungumzia amani leo. Akisisitiza haja ya kuondoa mashirika ya kigaidi nchini Syria, je Cavusoglu anachukulia ugaidi kama mambo yanayoshambulia maeneo yake mwenyewe?

Je, Marekani, Urusi, dola kubwa zaidi za kigaidi duniani, na mshirika wao nchini Syria Assad - muuaji wa mamilioni ya Waislamu aliowachinja, kuwaacha bila makao na kusababisha wawe wakimbizi - hawana sifa ya kuwa gaidi mkubwa zaidi? Na je, pambano la kwanza na kuu zaidi halikupaswa kuwa kwao?

Tunahitaji kumuuliza Bw. Cavusoglu! Je, wewe uliyeharibu na kuhujumu mapinduzi ambayo Waislamu walitaka kuyapata, ambaye unatoa kila aina ya msaada kwa makundi ili kukubaliana na mpango wa Marekani, ambaye unatia shinikizo kwa wale wasiokubaliana na ambaye umedunga kisu kwenye moyo wa mapinduzi kwa bahashishi ya operesheni za kijeshi, kumpatanisha dhalimu na waliodhulumiwa kupitia makubaliano ya kisiasa ambayo ni wajibu wako wa mwisho! Kwako wewe, aina zote za maadili zinaweza kupinduliwa ndani ya mfumo wa realpolitik, kwenye mhimili wa maslahi. Unaweza kulegeza msimamo na kukaa pamoja na wale uliowaita wauaji, magaidi kwa ajili ya maslahi. Hata hivyo, Waislamu hawajawahi kuwa na kamwe hawatakuwa na aina hii ya vipimo na maadili. Aliyedhulumiwa hawezi kujisikia huru bila kuivunja mikono ya dhalimu. Haki haiwezi kupatikana bila ya kulipa jicho kwa jicho kutoka kwa muuaji. Wanadamu hawawezi kupumzika kirahisi bila kuondolewa kwa mifumo na dola ambazo ndizo chanzo cha ukatili. Hivi ndivyo haswa unavyohitaji kufanya kwa ajili ya amani ya kudumu. Vyenginevyo, hutaweza ila kumtetea dhalimu.

Hujakata tamaa na utekelezaji mipango ya Marekani katika jiografia ya Kiislamu. Kutokana na ukweli kwamba unayatazama maisha kwa fikra chafu za siasa za kidemokrasia, hujawahi kuelewa mwelekeo, haki, ukweli na yale ambayo ni ya busara na yanayokubalika. Mtu mwenye hekima anajua kwamba hakutakuwa na amani kwa muuaji wa familia yake, na dhalimu anayeendeleza ukatili wake.

Iwapo utakuwa na akili kweli, basi weka kando mipango ya Marekani ya Geneva na Astana na kusanya jeshi lako kwa ajili tu ya Waislamu wanaodhulumiwa, uondoe utawala katili wa Assad na uonyeshe kwamba uko dhidi ya dhalimu. Kila mtu anajua kwamba unazo nguvu na fursa ya kufanya hili. Lakini kwa bahati mbaya, unaonyesha pia kwamba huna ujasiri na azma.

Kwa yakini, Makhalifa ambao wataonyesha ujasiri na dhamira hii watatoka kwenye kifua cha Ummah huu. Na siku hiyo, hakuna dhalimu atakayeweza kuendeleza ukatili wake. Hakuna muuaji atakayekosa kuadhibiwa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu