Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 India iko katika Vita na Uislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Takriban wasomi 20 walimwandikia barua Waziri Mkuu Modi wakitaka kupigwa marufuku kwa vitabu vinavyohusiana na Uislamu wa kisiasa katika vyuo vikuu vinavyofadhiliwa na serikali. Pia kumekuwepo na visa vyengine vya vijana wa Kiislamu kukamatwa kwa kushukiwa kujihusisha na ISIS.

Maoni:

Kumekuwa na kasi ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini India katika muongo mmoja uliopita. Hivi majuzi, hali hii imefikia kiwango cha juu zaidi huku wasomi na maprofesa kadhaa wakimwandikia barua Waziri Mkuu wakitaka kupigwa marufuku kwa vitabu vinavyotokana na Uislamu wa Kisiasa. [manushi.in] Barua hiyo inaangazia fikra za Mawdudi (rah) na jinsi fikra zake zimeathiri harakati mbalimbali za Kiislamu zikiwemo harakati mbalimbali za Jihad.

Ni lazima ieleweke wazi kwamba Uislamu wa Kisiasa sio ukiritimba wa wanafikra au makundi fulani; bali, Uislamu wa Kisiasa ni mojawapo ya vipengee msingi vya Uislamu. Waislamu kwa jumla wamekataa misimamo ya kupitiliza ya makundi kama ISIS, lakini hiyo haimaanishi kwamba Waislamu wameachana na baadhi ya mambo msingi ya Dini yao ambayo ni pamoja na siasa. Si ajabu kwamba harakati au makundi mengi yaliyopo katika Umma wa Kiislamu yana maumbile ya kisiasa. Siasa katika Uislamu ni njia ya Mtume wetu kipenzi (saw). Ni sunnah ya Anbiya (manabii) mbalimbali wa Bani Israil kama ilivyotajwa katika Hadith. Mtume (saw) amesema:

‏«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لاَ نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ‏.‏ قَالُوا فَمَا تَأْمُرُنَا قَالَ فُوا بِبَيْعَةِ الأَوَّلِ فَالأَوَّلِ، أَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ، فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُم»‏

“Walikuwa Banu Israil wanaoendesha siasa zao ni mitume wao: kila alipokufa mtume, alifuatiwa na mtume mwengine. Na hakika yake hakutakuwa na mtume mwengine baada yangu, lakini kutakuwepo na makhalifa na watakuwa wengi. Wakauliza: ‘Watuamrisha nini?’ Akasema: mpeni ahadi ya utiifu (Ba’yah) mmoja baada ya mwengine. Wapeni haki zao, kwani hakika Mwenyezi Mungu atawauliza yale aliyowatawalishia.” [al-Bukhari 3455]

Serikali ya sasa ina matatizo na Qur’an na Uislamu wenyewe, na sio na wanafikra au makundi maalum. Inalaani na kuharamisha majadiliano ya aina yoyote yanayohusiana na vipengee vya kisiasa vya Uislamu na jinsi Uislamu unavyotoa suluhu kwa matatizo mbalimbali ya kisasa yaliyoletwa na mfumo wa kirasilimali ulioundwa na mwanadamu.

Uislamu ni Haq (haki) iliyoteremshwa kutoka kwa Mola wa walimwengu wote. Uislamu una Aqidah (itikadi) kiakili iliyojengwa juu ya misingi ya kukatikiwa ya kifikra yenye kukinaisha akili na kushibisha umbile (Fitra) la mwanadamu. Uislamu haushajiishi utiifu wa kiupofu na kiburi kwa imani ya mababu.

[وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّبِعُوا۟ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُوا۟ بَلْ نَتَّبِعُ مَآ أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ ءَابَآءَنَآ ۗ أَوَلَوْ كَانَ ءَابَآؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْـًۭٔا وَلَا يَهْتَدُونَ]

“Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu; wao husema: Bali tutafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka?” [2:170]

Sheria na mafundisho ya Uislamu yameweka amani na uadilifu tangu siku Rasuulullah (saw) alipoanzisha Dola ya Kiislamu mjini Madina. Sheria zake adilifu za kijamii, kiuchumi na kimahakama zilikuwa zilieneza amani miongoni mwa watu wakiwemo raia wasiokuwa Waislamu wa Dola ya Kiislamu. M.K Gandhi alisema kwa usahihi kwamba India ingestawi kama ingetawaliwa na kiongozi kama Khalifa Umar (ra), lakini inapaswa kueleweka kwamba kielelezo kama hicho kilichoonyeshwa na Umar (ra) kilikuwa ni matokeo ya uwakilishi wa kweli wa siasa zilizotajwa katika Qur'ani Tukufu na Sunnah. Kwa hivyo kwa kweli ni sheria za Qur’an na Sunnah ndizo zingeidhamini India amani, maendeleo, haki na ustawi.

Serikali ya sasa ya Kibaniani yenye msimamo mkali iliopitiliza inaogopa fahamu ya umoja (upekee) wa ukweli. Chuki badala ya mdahalo na majadiliano ya fikra na fahamu zinazohusiana na Uislamu ndio ada. Matumizi ya lugha ya Kiurdu, Adhaan na kubadilisha likizo kuwa Ijumaa kunaonekana kuwa ni msimamo mkali na uwezekano imara wa kuibuka kwa Dola ya Kiislamu [timenownews.com]. Vitendo hivi si lolote bali ni kutia hofu na kuutumia Uislamu na Waislamu kama visingizio ili kufikia malengo ya kisiasa. Fikra ya uwingi iliyojengwa ndani ya Demokrasia na vita vya kiulimwengu dhidi ya ugaidi ni vichocheo vya serikali hii yenye msimamo mkali vya kumakinisha utawala.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Fattaah ibn Farooq

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu