Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uturuki na ‘Israel’ Waamua kwa Pamoja Kuteua Balozi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Akikumbuka kwamba mchakato wa mazungumzo na 'Israel' ulianza kwa kuundwa kwa serikali mpya nchini Israel na kuchaguliwa kwa Isaac Herzog kama Rais, Waziri wa Mambo ya Nje Mevlut Cavusoglu alisema, "Mchakato huo uliendelea kwa ziara ya Herzog nchini Uturuki na kisha ziara yangu nchini Israel, ziara ya Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje Yair Lapid jijini Ankara." alisema. (Shirika la Anadolu)

Maoni:

Katika kipindi cha miaka yake 10 ya kwanza madarakani, Rais Erdogan alipigana dhidi ya muongozi wa kijeshi, akisema dunia ni kubwa kuliko watu watano, ilikuwa na mafanikio dhidi ya Uwepo wa Kiyahudi wa Rais wa zamani wa Israel Shimon Peres kwa 'dakika moja' unajua kuua, aliondoka, akasitisha mahusiano ya kidiplomasia na Uwepo wa Kiyahudi baada ya tukio la Mavi Marmara. Wakati wa Mapinduzi ya Kiarabu, aliunga mkono harakati ya Ikhwan al-Muslimin nchini Misri na upinzani nchini Syria. Aliangazia matakwa ya mabadiliko nchini Uturuki, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Mazungumzo haya ya Rais Erdogan yamekubaliwa na kuungwa mkono na watu wa Uturuki na nchi nyingine za Kiislamu, ambao walikuwa wametengwa na hali halisi ya hapo awali na tawala za ukandamizaji. Hata ilipelekea kwenye ukweli kwamba aliitwa Kiongozi wa Ummah.

Hata hivyo, msingi wa matamshi ya mabadiliko ya Erdogan nchini Uturuki na eneo lake ulikuwa ni mizozo ya ushawishi wa dola za Kikoloni za Kikafiri ya Kimagharibi. Hata hivyo, Erdogan alifaulu kuficha mzozo huu nyuma ya matamshi ambayo Waislamu wa eneo hilo waliyapenda na kuyaunga mkono, na aliweza kudumisha utawala wake imara.

Kufeli kwa Mapinduzi ya Kiarabu katika utawala wa pili wa miaka 10 wa Erdogan na kuregea kwa hali halisi ya awali ni jaribio la mapinduzi la Julai 15 mwaka 2016. Mchakato wa janga la maambukizi la 2020 na 2021 na mfumko wa bei uliofuata, pamoja na kuzorota kwa uchumi, ilipelekea kupungua kwa uungaji mkono mkubwa kwa Erdogan.

Akiwa amekwama katika siasa za ndani na nje kabla ya uchaguzi ujao wa 2023, Erdogan aliamua kuteua kwa pamoja balozi kati ya Uturuki na Uwepo katili wa Mayahudi wa 'Israel', kama hitaji la Amerika la kuhalalisha mahusiano na Uwepo wa Mayahudi katika eneo hilo na uchumi kuimarika.

Ukweli kwamba Waislamu 49 wa Kipalestina waliuawa shahidi na Waislamu 360 walijeruhiwa kutokana na mashambulizi ya Uwepo wa Mayahudi huko Gaza, hata wiki mbili zilizopita na wakati suala hilo bado linaendelea, uamuzi huu unaonyesha hatua ambayo Erdogan amefikia.

Aidha, akisisitiza kuwa ni muhimu kwa Waziri wa Mambo ya Nje Çavuşoğlu kumteua balozi wa kuendeleza uhusiano baina ya nchi hizo mbili, alisema, "Tutaendelea kutetea haki za Palestina, Jerusalem na Gaza, na ni muhimu pia ujumbe wetu kuhusu suala hil utumwe moja kwa moja hadi Tel Aviv katika ngazi ya balozi."

Kauli yake pia  ni ya maagizo katika kuonyesha msimamo wao kuhusu sera ya kigeni.

Katika miezi 3 iliyopita;

Rais wa umbile la Kiyahudi Isaac Herzog, akitona damu ya Waislamu mikononi mwake, alikaribishwa na Rais Erdogan kwenye zulia jekundu jijini Ankara.

Bendera ya Uwepo wa Mayahudi ilibebwa na Askari Muislamu wa Kituruki.

Kaburi la Mzayuni maarufu Theodor Herzl, ambaye Sultan Abdulhamid Khan alimfukuza mbele yake kwa sababu alitaka ardhi kutoka Palestina, lilitembelewa na Waziri wa Mambo ya Nje Mevlut Cavusoglu na kuwekewa shada la maua.

Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi na Waziri wa Mambo ya Nje Yair Lapid walikutana na Cavusoglu jijini Ankara.

Shambulizi la hivi karibuni la Gaza la uwepo wa Mayahudi, ambapo Waislamu 49 wa Palestina waliuawa shahidi na 360 kujeruhiwa, lilipuuzwa.

Uamuzi wa pande zote umechukuliwa kati ya Uturuki na jamii ya Kiyahudi kumteua Balozi.

Rais Erdogan alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi Yair Lapid kuhusu uwepo nyakuzi wa Mayahudi.

Haya yote yanatokana na ukweli kwamba Rais Erdogan ameegemezwa juu ya msingi wa mfumo mbovu ya Kibepari unaoyapa tu kipaumbele maslahi, maslahi, madaraka na madaraka pekee katika siasa za ndani na nje ya nchi.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Uislamu, ambao ni hukmu ya Mwenyezi Mungu, hauchukui marejeo.

Kwa maneno nyengine, si Matakwa ya Mwenyezi Mungu wala matakwa ya watu yalikuchukuliwa kuwa ndio msingi, bali matakwa ya makafiri wakoloni wanaotawala dunia leo ndiyo yalichukuliwa kuwa msingi.

Hakuna shaka kwamba Mwenyezi Mungu hakubaliani na mtazamo huu wa Rais Erdogan, wala Waislamu hawakubaliani nao.

Wanaouidhinisha ni Makafiri wakoloni wa Magharibi, wanaotaka Uwepo wa Mayahudi na usalama Wake.

Kuutambua Uwepo wa Mayahudi kama dola, kumteua balozi kwa kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia, au hatua zozote zinazoweza kumaanisha kuuhalalisha kwake ni imeharamishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw).

Wale walioupa uhai uwepo wa Mayahudi kwa kujitoa kafara fadhila za Ummah kwa ajili ya maslahi yao wenyewe, kwa njia hiyo hiyo watateseka na kujutia yale waliyoyafanya pindi uwepo wa Mayahudi utakapotoweka.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Remzi Özer

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu