- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hakuna Maji ya Kunywa, ila yako ya Kutosha ya Kughariki
(Imetafsiriwa)
Habari:
ISLAMABAD, Agosti 23 (APP): Waziri wa Shirikisho wa Mabadiliko ya Tabianchi Seneta Sherry Rehman, wakati wa hotuba yake katika mukhtasari wa dharura ya sasa ya mafuriko nchini na NDMA, alisisitiza haja ya uhamasishaji wa haraka wa Kimataifa na wa kitaifa wa juhudi za misaada ya kibinadamu na uokoaji ili kurudisha hali ya watu walioadhirika na kukumbwa na mafuriko.
Maoni:
Mvua za masika zimesababisha maafa kote Pakistan. Kulingana na ripoti ya hivi punde ya Mamlaka ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa, takriban watu 903 wamekufa nchini kutokana na mvua kali na mafuriko msimu huu wa joto, huku 50,000 wakikosa makaazi na wanaishi kwenye mahema sasa. Mnamo Jumatano iliripoti kuwa watu 126 waliuawa katika matukio yanayohusiana na mafuriko katika muda wa saa 48 zilizopita, huku wengi wa waathiriwa wakiwa wanawake na watoto.
Pakistan imekadiriwa kuwa mojawapo ya nchi zilizoathiriwa zaidi na hali ya hewa kote duniani kwa Orodha ya Hatari ya Hali ya Hewa Duniani. Sio tu kipengee cha mvua nyingi lakini kukosekana vikwazo vya kimaumbile. Kwa kweli sio tu uzembe katika kuendana na mabadiliko ya mazingira lakini uporaji katili wa maliasili ya Pakistan. Ukataji miti mkubwa haupaswi kulaumiwa kutokana na ujinga wa watu wa kawaida. Kwa hakika, "mafia wa mbao" waliojipanga vyema wakiungwa mkono na wanasiasa/maafisa wa serikali na maafisa wa misitu ndio waliosababisha upotevu wa misitu muhimu. Kiasi cha hasara kinaweza kupimwa kwa kulinganisha tu eneo lililokuwa limefinikwa na msitu 1947 na sasa. Wakati wa Ugawaji, Pakistan ilikuwa na asilimia 33 ya ardhi yake iliyofinikwa na misitu ambayo kulingana na makadirio ya sasa ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa ni asilimia 2.2.
Kila mwaka mambo yanazidi kuzorota na kila serikali inayohudumu inailaumu serikali iliyopita, huku serikali iliyopita ikilaumu ukosefu wa dhahiri usimamizi wake. Maafisa kama Sherry Rehman, badala ya kuzingatia juhudi za uokoaji, hawaoni aibu kutumia pesa nyingi za walipa kodi kufanya mikutano ya wanahabari na kuomba kila mtu. Tumeona wenyeji na watu kutoka sehemu nyengine za Pakistan wakisaidia na kujitolea kwa ajili ya ndugu na dada zao. Hawa ndio watu ambao ni tumaini na nguvu kwa wengine, kwani huduma zao sio kwa ajili ya ulafi wa pesa, umaarufu au jina. huku viongozi wanaokalia fedha na rasilimali wakinoa meno kwa ajili ya kuwajeruhi zaidi wahanga wa uharibifu huo. Muungano wa Ulaya (EU) umetangaza kutoa Euro 350,000 kwa ajili ya msaada wa kibinadamu kwa familia zilizoathiriwa na mafuriko nchini Pakistan. Maafisa wasio na haya watawauza watu wa Pakistan kwa mara nyengine tena na kuweka pesa mifukoni mwao wenyewe. Tunapoiangalia bajeti, tutaona kuwa hakuna mgao uliopendekezwa kwa majanga ya kimaumbile katika mpango wa kifedha wa mwaka wa fedha wa 2022-2023. Rupia bilioni 9 zimetengwa kwa jina la changamoto ya mazingira, wakati huo huo bilioni 60 zimetengwa kwa Baraza la Mawaziri.
Watu wa Karachi wameumia sana kiasi kwamba sasa mawingu ni dhiki kwao. Kwa mwaka mzima wanatamani maji na wakati wa masika wanakuwa waathirika wa mafuriko na kupigwa shoti na umeme. Kwa miaka mingi mitaro ya maji ya Karachi imekuwa ikitumiwa vibaya. Kwenye mitaro mingi midogo ya maji ya mvua, ujenzi haramu umefanyika. Katika makala yenye kichwa "Kwa nini Karachi Inafurika," mchora ramani za ujenzi na mpangaji miji maarufu, Arif Hasan anaandika:
"Wakati huo huo, Serikali ya Sindh, kwa matumizi yake yenyewe, imejenga sehemu za maegesho ya magari, afisi na hosteli za MPA kwenye nullahs na hata baadhi ya afisi za usajili za Mahakama Upeo ya Pakistan zimejengwa juu ya nullah." Kwa hivyo kinaya ni kuwa afisi yenu ya haki imekaa juu ya usalama wenu kutokana na mafuriko.
Katika kipindi cha historia, usambazaji wa maji ulikuwa ndio sababu ya ustaarabu mwingi kuoibuka na kusambaratika, kufungika au hata kutoweka. Waislamu katika kipindi chote cha utawala wao walielewa umuhimu wa usimamizi wa maji na usafi wa mazingira.
Bani Umayya walijenga mabwawa kwenye mito na mabonde, na walijenga mitaro na mikondo ya kuchepusha maji. Pia, walisafisha mitaro kila msimu na kujenga mikondo juu ya mito ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na bidhaa, na kuimarisha mtiririko wa maji. Lengo msingi la kujenga mabwawa lilikuwa ni kuzuia mafuriko ya ghafla katika mabonde (wādī), lakini kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya kilimo au malisho kulikuwa faida ya ziada. Bani Abbas walianzisha afisi ya usimamizi wa maji, ambayo waliiita Diwan ya al-Aqrah (maana yake idara ya maji).
Maabbasiya walijenga mabwawa kwenye Mto Furaat ili kudhibiti maji yake, na kisha kuyasambaza kwa kutumia vijito na njia ili kupata manufaa ya hali ya juu na kufika eneo kubwa zaidi. Matokeo yake, waliweza kulima na kunyunyizia maji mashamba yote. Mfumo wa maji ulioanzishwa na Waislamu Waarabu huko Andalusia ili kusambaza maji mji mkuu wa Uhispania, bado unafanya kazi tangu kuanzishwa kwake karne nyingi zilizopita.
Watawala wa Kiuthmani walitunza vizuri usambazaji wa maji. Mabwawa, mabirika, visima, matangi, na madimbwi yalijengwa ili kukusanya maji; njia za maji, mifereji, mabomba ya maji, na mizani za maji zilijengwa ili kusafirisha maji; mabomba na hifadhi za maji kwenye njia za maji zilijengwa ili kusambaza maji.
Hii si mifano tu bali namna Dola ya Kiislamu inavyowajali watu na rasilimali zake. Kiongozi wa kweli wa Kiislamu ni mchungaji juu yao. Afisi ya Khalifa ni jukumu kubwa kabisa na ni wale tu wanaowajibika na watiifu kwa Mwenyezi Mungu pekee ndio wanaoweza kulitimiza. Umar Bin Abdul Aziz ni mfano kamili kwa Amiri anaye elewa uzito wa majukumu yake.
Yeye (ra) alisema: “Wallahi ningetamani kuwa kati yangu na afisi hii kungekuwa na umbali wa Mashariki na Magharibi!” na daima alisisitiza kwamba watu wake wambadilishe endapo hawakufurahishwa naye kama khalifa wao, pendekezo ambalo walilikataa. Umar aliwaambia watu wake, “Watawala kwa kawaida huteua watu wa kuwachunga raia wao. Nimekuweka nyinyi kuwa waangalizi juu yangu na tabia yangu.”
Ibn Umar amepokea kutoka kwa Mtume (saw),
«أَلَا كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ فَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ وَالْمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى أَهْلِ بَيْتِ زَوْجِهَا وَوَلَدِهِ وَهِيَ مَسْئُولَةٌ عَنْهُمْ وَعَبْدُ الرَّجُلِ رَاعٍ عَلَى مَالِ سَيِّدِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُ أَلَا فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»
“Ninyi nyote ni wachungaji na kila mmoja wenu ataulizwa alivyovichunga. Mume ni mchungaji wa watu wa nyumba yake na ataulizwa kuhusu aliowachunga. Mke ni mchungaji wa nyumba ya mumewe na watoto wake na ataulizwa kuwahusu. Na mtumwa ni mchungaji juu ya mali ya bwana wake, na ataulizwa kuihusu. Basi jueni, kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mmoja ataulizwa kuhusu alivyovichunga.”
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan