Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Chaguzi za Kidemokrasia: Njia ya Kumakinisha Ukoloni Mamboleo

(Imetafsiriwa)

Habari:

Baada ya IEBC kumtangaza naibu rais Dkt William Ruto kuwa ndiye rais – mteule, ujumbe wa maseneta wa Amerika ukiongozwa na Seneta Chris Coons uliizuru Kenya. Ikumbukwe kwamba seneta Chris alikuwa mchangiaji mkubwa sana wa mazungumzo ya ‘handshake’ kati ya rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa waziri mkuu Raila Amolo Odinga.

Maoni:

Ujumbe huu uliokutana na viongozi muhimu serikalini kiuhakika unahitaji kumulikwa kwa kina na kuangaliwa kwa umakini mkubwa.

Kwa upande mwengine, balozi wa Uingereza nchini Kenya, Jane Marriot kwenye mtandao wake wa Twitter akaandika kwamba: ‘Uingereza haiungi mkono au kupendekeza mgombea au chama chochote katika uchaguzi huu’.

Marekani na Uingereza kuingilia mchakato wa kisiasa wa Kenya inaonesha wazi mapambano na kinyang’anyiro kwa mataifa ya ulimwengu wa tatu ili yaendelee kuwekwa chini ya ushawishi na mduara ule ule wa mabeberu wa kikoloni. Na hili ndilo linaloangaliwa zaidi na mataifa haya.

Ukoloni kama sera ya kigeni ya mataifa ya Kimagharibi hujaalia chaguzi za kidemokrasia zinabakia kuwa ni zana na uwanja wa mapambano na kinyang’anyiro kwa rasilimali za ulimwengu wa tatu.

Mataifa ya Kimagharibi ya Kibepari yameweza kutunga urongo wa madaraka na uhuru ambao hata huwahadaa wasomi miongoni mwa wananchi. Hakika Demokrasia inabaki na itaendelea kuwa njia ya kikoloni kudumisha ukoloni mamboleo.

Sisi katika Hizb ut-Tahrir twapenda kueleza kinagaubaga kwamba walimwengu hawatoweza kujikomboa kutokana na pingu za ukoloni isipokuwa kupitia kusimamisha Uislamu kimfumo na kiserikali.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Omar Al-Beity

Mwanachama wa Afisi ya Habari Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu