Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ikiwa Ulimwengu wa Kimagharibi una Mistari Mekundu, Uislamu Pia Unayo!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) wakiashiria shambulizi la hivi karibuni dhidi ya Msikiti wa Gazargah wa mkoa wa Herat wameeleza kuwa, ‘Ugaidi’ bado ungali ni moja ya vitisho vikubwa kwa amani na ustawi wa kimataifa, na kuhimiza ulazima wa kupambana nao. Msimamo kama huo unachukuliwa dhidi ya mlipuko uliotokea Ijumaa, Septemba 2, 2022 ndani ya Msikiti wa Gazargah wa mji wa Herat ambapo Mawlavi Mujib-ur-Rahman Ansari, khatibu wa Msikiti wa Gazargah wakiwemo watu wengine kadhaa waliuawa kishahidi na kujeruhiwa. Licha ya kuwa mzungumzaji fasaha wa Msikiti huo, Bw. Ansari alijulikana kama mtu mwenye ushawishi kwa umma vilevile.

Maoni:

Umoja wa Mataifa na dola kubwa daima zimekuwa zikiingilia ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya ndani ya Afghanistan. Siku zote zimekuwa zikijaribu kuzisimamia nchi za Kiislamu ili kulinda ubwana wao duniani kwa kuhakikisha wanaweka udhibiti wa mfumo wa kisekula. Marekani na dola nyenginezo mara kwa mara zimekuwa zikichukua misimamo ya kuingilia ili kuilazimisha Imarati ya Kiislamu kuzama katika maadili ya Kimagharibi na mtindo wa maisha ya kisekula. Kwa kuwa ni wazi kuwa Marekani imemteua Rina Amiri kuwa mjumbe maalum wa Marekani kwa wanawake, wasichana na haki za binadamu nchini Afghanistan, Thomas West kuwa Mwakilishi Maalum wa Marekani katika masuala ya Afghanistan, Richard Bennett kuwa Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Afghanistan pamoja na Mwakilishi maalum wa Muungano wa Ulaya na wajumbe maalum wa dola nyenginezo, ambayo yote yanaonyesha kwamba [Magharibi] haitaacha kuingilia kati ili kuhakikisha maslahi yao ya kisiasa na maadili ya Kimagharibi nchini Afghanistan.

Wanachama wa UNSC wametokea kupatiliza kulitumia tukio la hivi majuzi, kufanya kampeni ya 'tishio la ugaidi' nchini Afghanistan ili kulinda maslahi yao; Pindi dola za Kimagharibi zinapoeleza wasiwasi wao kuhusu uhuru, haki za wanawake, haki za binadamu na kadhalika, kuitishia Imirati ya Kiislamu kwa kutumia sera ya 'Fimbo na Karoti', hii ina humaanisha kwamba ulimwengu wa Magharibi una baadhi ya Mistari Mekundu ambayo Kwayo huwekeza kwa kiasi kikubwa itangazwe na kuzitekelezwa kwa wingi katika jamii zao; lakini inapokuja kwetu, wanaitumia kama zana na kauli mbiu tu ili kutuchanganya juu ya Mistari Mekundu yetu wenyewe. Kwa hakika maadili ya kisekula na maslahi ya dola za Kimagharibi yanawahitaji kuingilia kati masuala ya nchi nyingine na hata kubainisha jinsi uhusiano na majukumu ya wanandoa wa Kiislamu yanavyopaswa kuwa. Kinyume chake, wanaendelea kuitaka Imarati ya Kiislamu kuhakikisha kwamba haiingilii mambo ya mataifa mengine wao [IEA] hawavuki nje ya mipaka ya Afghanistan.

Imarati ya Kiislamu lazima itambue kwamba: 1) wazo la kutoingilia mambo ya wengine ni dhana isiyo ya kweli na ya kindoto; 2) ikiwa ulimwengu wa Magharibi una mistari mekundu na unaamiliana nasi kwa msingi huo, vilevile Uislamu pia una mistari mekundu ambayo lazima ilindwe na serikali ya Kiislamu na iwe ndio msingi wakati wa kuamiliana na mataifa mengine - na ikiwa atatokea mtu yeyote kukiuka, serikali ya Kiislamu lazima iwape jibu lisiloweza kuepukika.

Pindi serikali ya Kiislamu ilipoasisiwa kwa mara ya kwanza kabisa, ilijitangaza kuwa chombo pekee ambacho kingeweka viwango na vigezo si vya ndani tu bali kwa wanadamu wote. Kwa hiyo Uislamu wenyewe ni kiwango na kanuni ambayo inaweza tu kutekelezwa na serikali moja na yenye nguvu ya kimataifa. Uislamu ni kigezo cha usawa na makosa, kheri na shari, halali na haramu, na kukithiri na wastani. Uislamu umeteremshwa kuwa ndio kigezo pekee cha kubainisha ni upi usawa, makosa na wajibu wa mwanadamu. Kwa hivyo ni wakati sasa wa kuhami mistari mekundu na vigezo vyetu [vya Kiislamu] kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ili kanuni zetu zitekelezwe kama kigezo cha kiulimwengu kote duniani.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Saifullah Mustanir
Mkurugenzi wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu