- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Uongozi wa Kijeshi Sio Ngawira
(Imetafsiriwa)
Habari:
“Waziri Mkuu Shehbaz Sharif alimteua Jenerali Asim Munir kama mkuu wa jeshi mpya wa Pakistan, chaguo ambalo linaweza kuimarisha upinzani wa Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan kwa serikali na kuzua mapigano yake makubwa na jeshi. Khan, ambaye kama waziri mkuu alimuondoa Munir kutoka wadhifa wa mkuu wa upelelezi, atauona uteuzi huo kama kikwazo kinachowezekana kwa jaribio lake la kulazimisha uchaguzi wa mapema... Munir kwa sasa anahudumu katika makao makuu ya jeshi kama mkuu makao hayo, akisimamia mahitaji ya vitengo vyote vya kijeshi. Mbali na ISI, pia ameongoza idara ya ujasusi ya kijeshi. Amehudumu chini ya amri ya moja kwa moja ya Bajwa katika maeneo ya kaskazini yenye matatizo mara nyingi yanayopakana na Afghanistan, China na India.” (Bloomberg)
Habari:
Kulikuwa na mapambano makali juu ya uongozi wa Jeshi la Pakistan. Yalifanyika kati ya kambi mbili za kijeshi zinazopingana. Kambi ya kwanza iliongozwa na mkuu wa jeshi anayeondoka, Jenerali Qamar Bajwa. Kundi jengine liliongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Inter-Services Intelligence (ISI), Luteni Jenerali Faiz Hameed, pamoja na Imran Khan, waziri mkuu aliyeng’olewa madarakani. Inaonekana kana kwamba kambi ya Jenerali Bajwa imesuluhisha mzozo huo kwa niaba yake. Imehakikisha kuwa Jenerali Munir anamrithi Jenerali Bajwa kama mkuu wa jeshi. Hii ni baada ya Faiz Hamid kutengwa, wakati Imran Khan alipojeruhiwa na kutishiwa kuuawa, endapo hataacha kugombana kwa ajili ya Hameed. Hilo basi, kivitendo, lilitokea.
Umuhimu wa uteuzi wa Munir kama mkuu wa jeshi unatangaza hali ya kisiasa ambayo dola ya Pakistan sasa itawekwa, pamoja na dori itakayochukua kikanda. Uteuzi wa Munir, aliye na usuli wa kijasusi, ukiwemo ujasusi wa ndani, uko sambamba na sera na mkakati wa Amerika katika eneo hilo. Sera ya Marekani inalenga katika kuiweka pembeni dori ya Pakistan kikanda na kuidhoofisha kijeshi, huku ikiipa India mkono huru katika eneo hilo, hasa nchini Afghanistan na katika kukabiliana na China.
Ama kuhusu dori ya serikali ya Pakistan, mwelekeo wake utakuwa katika nyanja za ndani, haswa kudhoofika kwa jeshi, pamoja na kujitahidi kusambaratisha silaha za kimkakati za nyuklia, ambazo hazina maana tena, kwa mtazamo wa Wamarekani. Hii ni katika muktadha wa vizuizi vinavyoendelea dhidi ya India, na Pakistan kuisalimisha Kashmir Iliyokaliwa kimabavu kwa India, huku ikitaka kusawazisha mahusiano na India, kwa njia ya kuhitimisha amani ya kina na ya kudumu.
Wadhifa wa mkuu wa jeshi umekuwa ngawira inayotamaniwa, kwa ajili ya kulimbikiza mali na kutosheleza tamaa ya ukuu miongoni mwa kundi la majenerali, wanaopigania nyadhifa, kwa ajili ya maslahi binafsi. Gharama ya kupata vyeo hivi ni kuuza maslahi ya umma na masuala nyeti ya Ummah. Sharti la kuteuliwa katika nyadhifa nyeti ni utekelezaji wa ajenda za Amerika katika nchi yenyewe, na katika kanda. Siku zote hizi ni ajenda za maangamivu kwa nchi na watu. Haya yote yanawalazimu wanyoofu ndani ya jeshi la Pakistan kuwakamata mafisadi kwa vyeo, akaunti za benki, majumba na ardhi kubwa. Wasipofanya hivyo, basi wataangamia na kuangamia pamoja nao.
Mtume (saw) amesema,
«مَثَلُ الْقَائِمِ عَلَى حُدُودِ اللَّهِ وَالْوَاقِعِ فِيهَا كَمَثَلِ قَوْمٍ اسْتَهَمُوا عَلَى سَفِينَةٍ فَأَصَابَ بَعْضُهُمْ أَعْلَاهَا وَبَعْضُهُمْ أَسْفَلَهَا فَكَانَ الَّذِينَ فِي أَسْفَلِهَا إِذَا اسْتَقَوْا مِنْ الْمَاءِ مَرُّوا عَلَى مَنْ فَوْقَهُمْ فَقَالُوا لَوْ أَنَّا خَرَقْنَا فِي نَصِيبِنَا خَرْقًا وَلَمْ نُؤْذِ مَنْ فَوْقَنَا فَإِنْ يَتْرُكُوهُمْ وَمَا أَرَادُوا هَلَكُوا جَمِيعًا وَإِنْ أَخَذُوا عَلَى أَيْدِيهِمْ نَجَوْا وَنَجَوْا جَمِيعًا»
“Mfano wa mtu anayejifunga na amri na mipaka ya Mwenyezi Mungu, ikilinganisha na wale wanaokiuka, ni kama mfano wa wale waliopiga kura kwa ajili ya viti vyao kwenye jahazi. Baadhi yao walipata viti katika sehemu ya juu, na wengine katika sehemu ya chini. Wale wa pili walipohitaji maji, ilibidi wapande kwenda kuleta maji (na hilo liliwasumbua wengine), kwa hiyo wakasema: ‘Tutoboe tundu katika sehemu yetu ya meli (na tupate maji) tuwaokoe walio juu yetu. kuwasumbua.’ Kwa hiyo, ikiwa watu wa sehemu ya juu watawaacha wafanye walivyopendekeza, watu wote wa meli wataangamia, lakini ikiwa watawazuia, pande zote mbili zitasalimika.” [Bukhari]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal al-Muhajir – Wilayah Pakistan