- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Je, Tuangalie Neno Lako au Matendo Yako?
(Imetafsiriwa)
Habari:
Shambulizi la bomu lilitokea katika mtaa wa Taksim Istiklal jijini Istanbul mnamo tarehe 13 Novemba na kuua watu 6 na kujeruhi vibaya watu 81, 2 kati yao wakijeruhiwa vibaya. "Hatukubali, tunakataa rambirambi za Ubalozi wa Marekani" alisema Waziri wa Mambo ya Ndani, Suleyman Soylu, ambaye alitoa kauli baada ya shambulizi hilo.
Soylu: "Bila shaka, muungano wetu na dola inayolisha maeneo ya kigaidi ya Kobani na kutuma pesa kutoka kwa seneti yao wenyewe kwa ufahamu huu, ambao unajaribu kuvuruga amani ya Uturuki kutoka huko, unapaswa kujadiliwa. Sisi sio adui wa yeyote, hatutupii macho ardhi ya mtu yeyote. Sisi si msaliti wa mtu yeyote. Ningependa kueleza kwamba bila shaka hatuna nguvu ya kuvumilia khiyana hizi ..." (Mashirika 14.11.2022)
Maoni:
Wakati Uislamu unahubiri maamrisho mengi yanayolenga kuwasifu Waislamu ambao dhati na maneno yao ni ya kweli, umetangaza uhadaifu, uwongo na maneno matupu kuwa ni haramu na mabaya. Hasa ukweli na kutegemewa kwa watu katika mamlaka ya uongozi ni muhimu zaidi, ambao ni hitaji la majukumu kwa Mwenyezi Mungu na Waislamu. Waislamu wameshuhudia mateso, uharibifu, kifo, usaliti, udanganyifu na uongo katika jografia hii na katika ardhi hizi kwa karne moja ambayo sasa wanashangaa ni ipi ndio chungu zaidi.
Dini, damu, uhai, mali na kujistiri kwa Waislamu ni matukufu, na jukumu la msingi la kuwalinda limekabidhiwa kwa dola. Kwa bahati mbaya, leo, wakati maadili haya yanakanyagwa na makafiri kila siku katika jografia hii, kutokuwa na aibu na maneno makali matupu ya watawala wanaoruhusu haya kwa kweli hayaleti maana yoyote. Tunapaswa tumuulize Waziri aliyesema tunajua hata saizi za viatu vya magaidi nchini hadi kufikia jana, inakuwaje hawezi kuzuia shambulizi la bomu katika mojawapo ya sehemu muhimu sana nchini!
Maadamu unakubali Marekani, Uingereza, Urusi, China, dola za Magharibi na uwepo wa Mayahudi kuwa marafiki na washirika, ambao ni wahusika wa ugaidi, maisha ya Ummah huu kamwe hayatakuwa salama. Ujanja huo sio kueleza kuwa Ubalozi wa Marekani, ambao ulitoa ujumbe wa rambirambi juu ya shambulizi la bomu lililotokea, hukukubali rambirambi zake. Ili uweze kuchukua hatua katika kukabiliana na mashambulizi. Ni kuzuia vitendo hivi bila kugharimu maisha ya watu. Ni kuharibu mchezo huo. Vyenginevyo, rambirambi ambazo Waziri wa Mambo ya Ndani hakuzikubali, Rais Erdogan amezikubali salamu za rambirambi zilizotolewa na Marekani kutoka ngazi ya juu kabisa wakati wa mkutano wake na Biden kwenye Mkutano wa G-20. Sio hilo tu, lakini angali anazungumza kuhusu ushirika, uhusiano, ununuzi na ndege za kisasa za F-16. Tumechoshwa na maneno yako ya kupumbaza, maneno yako ya kisiasa, kauli zako zinazohadaa umma, mahusiano yako na dola za kigaidi, kazi zako zisizolingana. Nyote wawili mtamaanisha kuwa dola hizi za kigaidi ndizo wahusika wa nafsi zilizopotea, na bado mtaendelea kuzungumzia kuhusu muungano huo. Mutasema kuwa nyinyi sio adui wa mtu yeyote. Mpendwa Mheshimiwa; tutabakia kuwa maadui na makafiri hawa, hasa kwa dola hizi za kigaidi zinazoosha mikono yao kwa damu ya Waislamu, mpaka Siku ya Kiyama. Hatutasimama mpaka tuuangamize utawala wao wa kidhalimu. Huu ndio ulazima wa imani yetu. Sasa mnapaswa kufanya uamuzi. Ima mtaachana na maneno matupu ya kupumbaza yanayowalaghai wananchi na kuachana na michezo ya muungano na dola hizi za kikoloni, upuuzi halisi wa kisiasa... Mtazifunga balozi za dola hizi za kigaidi, ambazo ndio kitovu cha ujasusi, na kuziondoa ardhi zetu kutokana na kuwa msingi wa operesheni za makafiri. Au mutaendelea kuzitazama dola hizi za kigaidi, ambazo mumezipa kila aina ya usaidizi kwa vitendo vyenu, na kuwafanya Waislamu walipie gharama.
Tunajua kwamba Waislamu wataihami dini yao, damu zao, maisha yao, kwa gharama ya uhai wao, na hatuna budi ila kuunda Khilafah itakayotishia dola za kigaidi. Kwa badali ya Khilafah, hofu itabadilika kuwa usalama, wasiwasi utabadilika kuwa amani, unyonge utabadilika kuwa nguvu na heshima.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA