Jumatatu, 06 Rajab 1446 | 2025/01/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ndani ya Ubepari Usalama wa Chakula ni Mazigazi

(Imetafsiriwa)

Habari

Kuna mkanganyiko miongoni Wakenya wengi ya kuwa je ilikuwa ni busara kwa uamuzi wa serikali wa kuondosha marufuku ya vyakula vinavyotokana na mazao ya kisaki (GMO). Katika taifa ambalo kila mwaka hukumbwa na uhaba wa chakula unaosababishwa na mambo kadhaa ikiwemo ukame uliosababisha mamilioni ya Wakenya kukabiliwa na baa la njaa kila mwaka, dhana iliyoko ni kwamba vyakula vya GMO ni hatari kwa afya ya mwanadamu na katika kuendesha vyema kilimo. Mwezi mmoja tu baada ya rais William Samoe Ruto kula kiapo na kuingia afisini, serikali ilitangaza kuondoshwa kwa marufuku ya GMO humu nchini.

Maoni:

Njaa na Utapiamlo uliosuhubiana na umaskini katika maeneo kame na nusu kame ya nchi imekuwa ni ada na laana ya kila siku inayowafanya wanadamu na hata mifugo kustahamili makali ya njaa na vifo wakiachwa pasina na matumaini yoyote yale siku za usoni kwani wanaishi ndani ya mfumo wa Kibepari. Kenya ni nchi ya Kibepari ambayo sera zake za kiuchumi zinatokana na uzalishaji unaotazama thamani ya mwanadamu ya jinsi wanavyochangia katika ukuaji wa Pato la Taifa, kwa kuzingatia hili katika eneo kame na nusu kame ambalo huchangia kidogo katika Pato la Taifa la Kenya kwa mwaka, humaanisha huduma duni za serikali ikilinganishwa na maeneo mengine yanayochangia Pato la Taifa.

Hali hii imefanya maeneo mengi nchini kukosa miundombinu ya kisasa itakayotoa huduma kwa wananchi kama vile miundombinu ya afya na barabara ili kurahisisha usafiri wa umeme. Ni kutokana na uchakavu wa miundombinu na ukame wa muda mrefu na watu huishi chini ya uongozi wa kibepari uso na ubinadamu hata chembe unaomtazama mwanadamu maisha yake ni uzalishaji tu wa bidhaa na huduma. Kumnukuu waziri wa biashara Moses Kuria kwa kuwepo kwako tu katika nchi hii wewe tayari ni mgombea wa kifo na kwamba kuna mambo mengi yanashindana kukuua hivyo basi hakuna makosa kwa GMO kuwepo kwenye orodha ya mambo hayo.

Uislamu kama mfumo unaotoka kwa Muumba wa Mwanadamu, Uhai na Ulimwengu ulioteremshwa kwa lengo la kumuongoza mwanadamu kufikia katika maisha mema hapa  duniani na kesho Akhera. Huu ni mfumo uliotabikishwa kwa zaidi ya karne kumi na tatu hadi mwaka 1924 ulimwengu uliposhuhudia kuangushwa kwa Uislamu na nuru yake iliomfanya mwanadamu kupata usalama wa maisha yake ikiwemo usalama wa chakula tena chakula chenye afya bora.

Chini ya uongozi wa Uislamu, Ulimwengu ulishuhudia uzalishaji wa kilimo usio na kifani kutoka Uhispania hadi mto Furaat nchini Iraq na mfumo wa unyunyiziaji maji wa mekanikia kwa kutumia Mifereji na vinu vya upepo ambavyo vilisababisha kutokomezwa kwa mbu wanaosambaza Malaria nchini Iraq. Hakuna wakati katika historia chini ya Khilafah ya Kiislamu ambapo njaa ilikuwa jambo la kawaida bali fauka ya hilo nchini Ireland ya miaka ya 1840 Sultan Abdul Majid 1 alitoa pesa taslimu na chakula kuokoa familia za Ireland kutokana vifo vya kutokana na baa la njaa… Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

﴿يَهْدِي بِهِ اللَّهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلَامِ وَيُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴾

“Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama, na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake, na huwaongoa kwenye njia iliyo nyooka.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Omar

Mwanachama wa Afisi ya Habari Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu