Jumamosi, 04 Rajab 1446 | 2025/01/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tamthilia ya Kuamua Kima cha chini cha Mshahara Imeanza!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ratiba ya mikutano ya kazi ya kuamua Kima cha chini cha Mshahara imekuwa wazi. Tume ya Uamuzi wa Kima cha Chini cha Mshahara, inayojumuisha mwajiriwa, mwajiri na wawakilishi wa serikali, itafanya mkutano wake wa kwanza mnamo Disemba 7 na mkutano wa pili mnamo Disemba 14 ili kuamua kima cha chini cha mshahara cha mwaka 2023. Baada ya mikutano mitatu kufanywa, nyongeza ya kima cha chini cha 2023 itatangazwa. Nyongeza ya kima cha chini cha mishahara inatarajiwa kutangazwa kuanzia wiki ya mwisho ya Disemba. (Mashirika)

Maoni:

utafiti uamuzi wa kima cha chini cha mshahara, ambacho kimekuwa karibu mshahara wa jumla nchini Uturuki na ambao unasubiriwa kwa hamu na takriban wafanyikazi milioni 10, unaingizwa mwaka huu katika mazingira ya uchaguzi wa 2023. Kwa hakika, itakuwa sahihi zaidi kuziita kazi hizi "Tamthilia ya Kiwango cha Chini cha Mshahara". Kwa sababu tume ya uamuzi ya watu 15, ambao hawajui maana ya kufanya kazi na mshahara wa chini katika maisha yao, inajaribu kuamua mshahara wa kila mwezi wa wafanyikazi milioni 10 juu ya jinsi ya kuishi bila kufa.

Katika tamthilia hii, kwanza, mazingira yanaundwa dhidi ya wafanyikazi kwa kuhakikisha walio wengi katika mashirika makuu ya serikali, kisha wawakilishi wa wafanyikazi wanacheza dori zao duni kwa eti kukasirika, kutishia kuondoka kwenye meza, kufafanua mistari mekundu, na hatimaye, unyonyaji wa nguvu kazi na kiakili kuendelea kwa kuweka tarakimu katika kiwango sawa na kikomo cha njaa.

Kwa kweli, Kima cha chini cha Mshahara kiliundwa kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo Waziri alisahau kipaza sauti chake kuzima miaka mitatu iliyopita. Kiasi hicho kilipangwa kama Lira za Uturuki 7785 kwa mwaka wa 2023.

Hebu fikiria kwamba mwakilishi wa wafanyikazi anapokea mshahara kwa kiwango cha kikomo cha njaa kwa wale anaowawakilisha. Tena, fikiria hali ambayo, ikiambatana na kibwagizo cha vyombo vya habari iliyopokea nyuma yake, inatangaza ada hii ya mateso kama "injili" kwa watu wake. Zaidi ya hayo, kwa kurudisha kile alichotoa kwa kijiko kwa upande mmoja na mwiko kwa upande mwingine! Kwa upande mwingine, makampuni makubwa ya kibepari, ambayo yana kila aina ya marupurupu ya kimada kwa ushirikiano na serikali, hayachukulii hata ongezeko la kiwango cha mfumko wa bei kinachostahili wafanyikazi wao. Kwa kweli, hii ni tamthilia ya kuchukiza.

Kwa upande mwingine, Rais Erdogan anasema kwamba hawawadhulumu wafanyikazi kwa mfumko wa bei baada ya kila mshahara wa chini unaotangazwa. Bila shaka, maneno ya Erdogan pia ni uongo mkubwa. Kwa sababu, kabla ya kiwango cha chini cha mshahara kuamuliwa, ongezeko lilifanywa kwa bidhaa za msingi kama vile chakula, mavazi, nyumba, usafiri. Zaidi ya hayo, pamoja na ongezeko kubwa la hadi 200% ya umeme na gesi asilia wakati wa 2022, serikali inaongoza hasira ya kampuni za kilafi za kibepari kupunguza mapato ya chini na nyongeza ya 122% ya viwango vya ushuru na ada mnamo 2023.

Wakati mfumko wa bei wa kila mwaka uliotangazwa na serikali mwaka huu ni 85%, mfumko wa bei halisi umezidi 150%. Kima cha chini cha mshahara kinatarajiwa kuongezwa kwa kiwango cha juu cha 50%. Kwa maana nyengine, ongezeko la kima cha chini cha mshahara tayari limepeperuka kabla halijaingia mfukoni mwa mwajiriwa. Aidha, suluhisho la suala hili si kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa kiwango cha mfumko wa bei.

Tatizo kuu ni mshahara wa chini wenyewe, ambao hauwezekani kabisa kwa mtu kujimudu nao. Aidha, tatizo kuu ni mfumo wa kibepari wenyewe, ambao huchukua kutoka kwa maskini na kuwapa matajiri. Katika mfumo wa kibepari, ambapo kodi inatozwa hata kwa kima cha chini cha mshahara, watu hawathaminiwi kwa namna yoyote ile. Mfumo wa kibepari ni katili, usio na maadili na ni mfumo ambao lazima uangamizwe.  

Suluhisho ni mfumo wa kiuchumi wa Uislamu. Hakuna kitu kinachoitwa kima cha chini cha mshahara katika mfumo wa uchumi wa Kiislamu. Mshahara huamuliwa kati ya mwajiriwa na mwajiri kulingana na aina ya kazi, ugumu na manufaa yanayotolewa kwa mkato. Kama ambavyo dola haitaweka kiwango cha chini cha mshahara, mshahara wa mwajiriwa hauwezi kunyakuliwa chini ya jina la kodi. Kodi hutozwa kwa matajiri pekee na kulingana na mahitaji ya dola.

Mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu haukatazi utajiri kama Ukomunisti, wala hauruhusu kila njia ya kupata utajiri kama ubepari. Unaweka mizani ya kipekee katika uchumi kutokana na vifungu vyake maalum vinavyozuia utajiri kuwa bidhaa inayozunguka tu kati ya matajiri pekee. Kwa hivyo, ustawi ndio chanzo pekee cha amani na maisha ya utu. Mfumo wa uchumi wa Kiislamu unaweza kutabikishwa tu kupitia mkono wa dola ya Kiislamu, na ni wajibu wa kila Muislamu kufanya kazi ili kuisimamisha dola hiyo.

(كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْاَغْنِيَٓاءِ مِنْكُمْۜ)

“ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu.” [Hashr: 7]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Emin Yildirim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu