Ijumaa, 11 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mwanamfalme wa Uingereza Harry Anawakilisha Vikamilifu Kipote cha Wauaji, cha Kikoloni cha Magharibi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Januari 05, 2023, vyombo kadhaa vya habari viliripoti kwamba Mwanamfalme Harry wa Uingereza, mtoto wa Mfalme Charles III, ameandika katika wasifu wake ujao kwamba yeye binafsi aliua watu 25 wakati akihudumu kama rubani mwenza wa helikopta na mwanajeshi wa Jeshi la Uingereza nchini Afghanistan.

Maoni:

Wakati  maoni ya Prince Harry kwamba "haoni aibu" kuwaua Waislamu 25 nchini Afghanistan kipindi cha uvamizi wa mauaji wa kikoloni, yameleta kwa haki majibu ya hasira kutoka kwa mjadala wa umma, kuna mambo kadhaa katika kesi hii, ambayo yanastahiki kutolewa maoni:

- Wakati Harry na wanajeshi wengine wa Magharibi, ambao walishiriki katika uvamizi wa wakoloni wa Afghanistan na Iraq, kwa kawaida watasisitiza kwamba waliwaua "magaidi", ukweli unabakia kwamba vikosi vya uvamizi vya Magharibi ndivyo vilivyowahangaisha raia kuliko mwengine yeyote, na kusababisha uharibifu usio na kipimo na mateso ya wanadamu katika ardhi za Kiislamu na kwengineko.

- Hakuna maadili matukufu au nia njema zilizowahi kuwa nyuma ya uvamizi na kukaliwa kimabavu kwa Afghanistan. Badala yake, vita dhidi ya Afghanistan vilichochewa tu na maslahi ya wakoloni wa Magharibi na uadui dhidi ya Uislamu na Umma wa Kiislamu, ukiongozwa na Marekani huku Uingereza na mataifa mengine ya Magharibi yakifuata nyuma.

- Wanamfalme Harry ameshutumu familia yake hadharani kwa upendeleo wao wa ubaguzi wa rangi dhidi ya mkewe. Ni Harry huyu huyu ambaye katika ujana wake alihudhuria karamu akiwa amevalia sare ya Wanazi, akiwa amevalia swastika mkononi, na ambaye amenaswa kwenye video akitoa maoni ya ubaguzi wa rangi kwa makadeti wenzake wa jeshi ambao huenda wana asili za Kiislamu. Huo ndio unafiki na undumakuwili wa kipote cha mabepari wa Magharibi. Harry huyu aliye dekezwa na kupendelewa anaua makumi ya Waislamu (ambao amewaonyesha taasubi za ubaguzi wa rangi, za kudhalilisha) bila ya majuto au aibu, katika vita haribifu vya uchokozi kwenye mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani; yote kwa ajili ya maslahi ya kimada na kistratejia ya dola za Magharibi. Kisha anaendelea kulalama, tena bila aibu, ukosefu wa uvumilivu wa rangi za watu katika familia yake ya kifalme ya Uingereza.

- Vivyo hivyo, kuna mtindo unaorudiwa wa tabia ya kiburi, mauaji, ya kikoloni ya dola kubwa za Magharibi dhidi ya ulimwengu mzima, sio tu ulimwengu wa Kiislamu. Wanavamia, kuharibu, kutawala, kuua, kutesa na kupora - na kisha kudai kusherehekewa kama mabingwa wa haki za binadamu. Wanajitokeza na kuunga mkono tawala ovu zaidi za kidhalimu katika ardhi za Kiislamu - na kisha wanaituhumu Sharia ya Kiislamu kuwa ya kiimla na ya kidhalimu. Wanalilia uvumilivu wakati inapolingana na maslahi yao, lakini wao ndio watendaji waliobobea wa ubaguzi wa rangi wa kimfumo na upendeleo.

Kwa hivyo, Mwanamfalme Harry wa Uingereza, katika kiburi chake kisicho na aibu na unafiki, na katika vitendo vyake vya uvamizi visivyo na majuto dhidi ya Waislamu wa Afghanistan, anawakilisha kikamilifu kipote cha kikoloni cha Magharibi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Elias Lamrabet

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu