Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Saudi Arabia Yakejeli Mfumo wa Kijamii wa Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Timu ya soka ya Saudi Arabia imemsajili Cristiano Ronaldo kwa mkataba wa michezo wa dolari milioni 175, hivyo yeye na familia yake watahamia Saudi Arabia. Watoto wake wanne wataandamana na mama yao, ambaye si mke wake kisheria. Hivi sasa, Saudi Arabia ina sheria "kali" za kuishi pamoja watu ambao si wanandoa. Ili kukabiliana na hili, Saudi Arabia imezipinda sheria kwa ajili ya Ronaldo, na ataruhusiwa kuwa mkaazi anayeishi na mwanamke ambaye hajamuoa.

Maoni:

Juhudi za hivi sasa za uongozi wa Saudia kuidhinisha Haramu ni sehemu ya kampeni ya kimataifa katika ardhi za Kiislamu ya kuhujumu Sharia na kuhalalisha maadili ya Kimagharibi. Ukweli kwamba Ronaldo ni mtu maarufu sana pia hutumiwa kunadi uasherati kama kitu cha kutamanika na kisichopingana na mafanikio.

Vijana watavutwa kwenye maadili na mafanikio ya watu mashuhuri, na kupotosha kizazi kijacho mbali na Uislamu ni ajenda inayofanya kazi katika jamii za Kiislamu kote duniani. Zaidi ya hayo, wanawake watahisi kwamba inakubalika kubeba majukumu ya uhusiano, na kutojitolea kwa mwanamume/baba wa watoto wao pia ni thamani kubwa inayokuzwa katika ufahamu mdogo wa kijamii wa shakhsia ya Kiislamu. Kitendo hiki cha kufanya kukejeli Sharia ni tusi kwa Quran na Sunnah na pambano la moja kwa moja kwa sheria za Mwenyezi Mungu (swt) pindi anaposema ndani ya Quran;

[اَلزَّانِيَةُ وَالزَّانِىۡ فَاجۡلِدُوۡا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنۡهُمَا مِائَةَ جَلۡدَةٍ وَّلَا تَاۡخُذۡكُمۡ بِهِمَا رَاۡفَةٌ فِىۡ دِيۡنِ اللّٰهِ اِنۡ كُنۡتُمۡ تُؤۡمِنُوۡنَ بِاللّٰهِ وَالۡيَوۡمِ الۡاٰخِرِ وَلۡيَشۡهَدۡ عَذَابَهُمَا طَآئِفَةٌ مِّنَ الۡمُؤۡمِنِيۡنَ]

“Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini.” [An-Nur: 2]

Wakati ambapo wasiokuwa Waislamu wanaruhusiwa kusimamia baadhi ya maeneo ya maisha yao ya kibinafsi kwa mujibu wa imani zao binafsi, suala hapa ni kwamba msingi wa utawala wa Saudi Arabia unahusiana na kusalimu amri kwa fikra ya Kimagharibi ya kuwa huru na kuishi maisha ya kimaendeleo. Hili linaendana na usasa na upaji Saudi Arabia sura mpya ambayo ndio sera ya watawala wa huko. Hakuna uhalali katika hukmu kuwa sawia na Uislamu yenye asili ya mfumo isiokuwa wa Kiislamu. Utoaji wa leseni kwa vilabu vya usiku, usambazaji wa pombe na tasnia duni ili kukuza utalii yote yanaungwa mkono na serikali ya Saudi chini ya mwongozo wa "maendeleo".

Ukiukwaji wa wazi wa maadili ya Kiislamu unatokana na utumwa wa viongozi wetu ili kuwaridhisha wasiokuwa Waislamu wanaotawala nchi zetu. Hakuwezi kuwa na uvumilivu wa "kuvumilia" hili; mitazamo yote ya fikra ambazo ni fimbo ya kimaadili inayotumiwa kuwapiga Waislamu ili kuwa na utiifu kupitia hatia ya uwongo ya kibinadamu.

Tunatoa wito kwa Waislamu wote kukataa wazo la kwamba takhsisi inaweza kutolewa katika hukmu za Sharia au kwamba utabikishaji wa kivipande wa Quran na Sunnah unakubalika.

Imeandikwa kwa AjIli ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu