Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Bangladesh Yahitaji Dola ya Khilafah ili kuwa Huru kutokana na Utumwa wa Ukoloni Mamboleo

(Imetafsiriwa)

Habari:

Bodi kuu ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) imeidhinisha mpango wa usaidizi kwa Bangladesh wenye thamani ya $4.7bn kwa viwango vya sasa vya ubadilishanaji fedha, na kuifanya nchi hiyo ya Kusini mwa Asia kuwa ya kwanza kufikia Mfumo wake mpya wa Ustahimilivu na Uendelevu (RSF). Ufadhili huo uliotangazwa mnamo Jumatatu ni pamoja na $3.3bn chini ya Programu za IMF za Upanuzi wa Mikopo na Mfuko wa Upanuzi Fedha na $1.4bn chini ya RSF mpya, ambayo inalenga kusaidia nchi za kipato cha kati na nchi za visiwa zilizo hatarini. IMF ilisema kifurushi hicho cha ukopaji cha miezi 42 "kitasaidia kuhifadhi utulivu wa uchumi, kulinda walio hatarini na kukuza ukuaji jumuishi na wa kijani". Pia ilisema inajumuisha mageuzi yanayolenga kuunda nafasi ya fedha ili kuwezesha matumizi makubwa ya kijamii na kimaendeleo, kuimarisha sekta ya fedha ya Bangladesh, kuimarisha mageuzi ya fedha na utawala, na kujenga uwezo wa kustahamili tabianchi. (https://www.aljazeera.com, Januari 30, 2023)

Maoni:

Kifurushi cha mkopo wa IMF wa dolari bilioni 4.7 kinakuja na afueni kwa serikali ya sasa lakini inawatia wasiwasi watu jumla. Kwa sababu kifurushi hiki ile inayojulikana kama ajenda ya mageuzi ya kiuchumi kama vile mkakati wa kukusanya mapato ya ndani, uondoaji wa aina zote za ruzuku, na mfumo wa ubadilishanaji wa dolari unaotegemea soko, n.k. ambayo yana athari mbaya kwa maisha na riziki za watu. Madhara mabaya ya kile kinachoitwa mageuzi ya kiuchumi tayari yanaonekana kwani serikali ya Hasina tayari imepitisha baadhi ya sera kulingana na masharti ya IMF. Bei ya umeme iliongezwa tena mnamo Januari 31, 2023 ambayo ni chini ya wiki 3 kutoka kwa bei ya mwisho iliyopandishwa mnamo Januari 12, 2023. Ajenda mpya ya marekebisho ya IMF iliyoongezwa itafanya hali kuwa ngumu zaidi kwa watu wengi ambao tayari wanabeba mzigo mkubwa wa kifedha. Sera za serikali zilizoagizwa na IMF. Kifurushi hiki cha hivi punde kitasababisha duru nyingine ya masaibu kwani matumizi ya serikali kwa ustawi wa umma yatapunguzwa na ushuru zaidi utatozwa. Hata hivyo maslahi ya wakopeshaji wa kigeni yatapatikana kupitia kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kulipa madeni ya nje. Kupitia sera hizo, IMF, chombo muhimu cha Wakoloni wa makafiri, inalinda kwa utaratibu maslahi ya wakopeshaji wa kikoloni, ambapo watawala vibaraka wa ardhi za Kiislamu wanashirikiana nao kuiba utajiri wa kiuchumi wa Umma. Kwa hivyo, vifurushi vya mkopo vya IMF na kinachojulikana kama ajenda ya urekebishaji kamwe hazijaokoa nchi yoyote yenye dhiki. Uchumi wa Sri Lanka na Pakistan ni mifano ya hivi punde zaidi ya dhulma hii ya ukoloni mamboleo - ziko mbali sana kutokana na kupona licha ya kuwa zimejiwasilisha kwa sera za IMF.

Ukombozi wa kiuchumi wa Bangladesh unahusiana moja kwa moja na kukataliwa kwa taasisi za ukoloni mamboleo na sera zao ambazo zimetufanya tuwe watumwa katika mfumo wa kiulimwengu wa kikoloni. Mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu unahitaji kutabikishwa na Dola ya Khilafah Rashida utakaokuwa na miundo na mipango yake wenyewe ya maendeleo. Taasisi za kifedha chini ya Dola ya Khilafah hazitatawanya mikopo na misaada tu bali zitatekeleza sera madhubuti na za kipekee za Kiislamu kwa ajili ya uchumi unaojitegemea usioegemea dola za nje. Khilafah inayokaribia itakuwa ni alfajiri mpya sio tu kwa Umma wa Kiislamu pekee bali kwa wanadamu wengine wote walio chini ya ukandamizaji wa kibepari.

[إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا]

“Hakika batili lazima itoweke!” [Al-Isra 17:81].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Shiraz
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu