Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Matetemeko ya Ardhi katika Ardhi za Waislamu - Ukumbusho wa Nguzu za Mwenyezi Mungu na Kufeli kwa Watawala wa Sasa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Tangu Jumatatu asubuhi, zaidi ya watu 11,000 wamekufa baada ya matetemeko makubwa ya ardhi kupiga miji mingi kote Uturuki na Syria. Idadi ya vifo inaongezeka huku watu wakisakwa na kupatikana wakiwa wamefukiwa chini ya majengo na vifusi. Matetemeko hayo ya ardhi yenye ukubwa wa 7.8, 7.5 na zaidi ya mitikiso 200, yametokea kusini mashariki mwa Uturuki na sehemu za Syria, na yameathiri maeneo mengine ya eneo hilo kama vile kaskazini mwa Iraq na Lebanon.

Maoni:

Sisi kama Waislamu tunaomboleza hasara za ndugu na dada zetu wa Ummah huu katika ardhi za Waislamu waliofikwa na janga hili, na tunawaombea waendelee kuwa na subira na taabu zao zifuatiwe na wepesi katika maisha haya na yajayo.

Matukio ya maafa na majanga ya kimaumbile kama haya, ni dalili za Uweza na Nguvu za Mwenyezi Mungu (swt) na udhaifu wa mwanadamu. Kwamba sisi kama wanadamu, tunahitaji na kwa hiyo tunapaswa kumsujudia Mwenyezi Mungu katika nyanja zote za maisha, kwani tunamuhitaji Yeye na kunyenyekea Kwake, hali Yeye hana haja ya ibada na kunyenyekea kwetu. Hizi ni dalili za kutafakariwa na ukumbusho wa utukufu wa Muumba wetu (swt). Ukumbusho huu haupaswi kutuathiri tu kama watu binafsi, tunapoona matukio ya maafa haya yakitokea.

Wataalamu wa matetemeko ya ardhi na wanajiolojia wanaelezea ukweli kwamba kuna ufahamu wa hatari zinazowezekana za matetemeko ya ardhi nchini Uturuki, na wengine hata hawashangazwi. Kinachotajwa kuwa chanzo cha vifo vya watu wengi ni matokeo ya matetemeko hayo ya ardhi, yanayosababishwa na majengo na miundo ya zamani yenye ubora duni, kifusi ambacho watu wamefukiwa chini yake kutokana na matetemeko hayo. Katika miji ya Syria, kama vile Aleppo na Idlib, majengo yameharibiwa katika vita na kujengwa upya kwa nyenzo mbaya zaidi. Ni nani wa kulaumiwa kwa miundombinu duni hii, zaidi ya serikali, kama vile Kituruki?

Maeneo ambayo yako katika hatari ya tetemeko la ardhi, yanapaswa kuwa na majengo yaliyoundwa kustahamili angalau baadhi ya uharibifu unaoweza kutokea, na kulinda maisha ya watu. Hili ni swali la vipaumbele, maadili, na vima. Je, mfumo wa utawala upo, kufanya kazi kama mchungaji mwadilifu wa mambo ya watu, kama itakavyokuwa chini ya dola inayoongozwa na Khalifa mwadilifu? Au ni chini ya serikali za sasa, zilizofeli katika ardhi zetu, ambazo zinapora rasilimali za Ummah na hazijali maslahi mengine zaidi ya yao wenyewe?

Kufeli kwa serikali za sasa na watawala wasaliti, walafi kuna dori kubwa la kutowahesabu kwa miundombinu sahihi ili kuhakikisha hali salama yanapotokea maafa ya kimaumbile.

Kwa sababu hizi, matetemeko haya si tu ukumbusho wa Uweza wa Mwenyezi Mungu, bali ni kufeli kwa tawala fisadi, dhaifu zinazotawala ardhi za Waislamu. Kwa hiyo, ni ukumbusho wa haja kubwa ya wakati wetu, Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo itachunga mambo ya Umma wa Kiislamu kwa kutumia rasilimali zetu nyingi katika kuwahudumia raia wote kwa miundombinu imara na ya kudumu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Younes Piskorczyk

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu