Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kufeli kwa Ubambanyaji wa Kisiasa na Fursa Halisi ya Mabadiliko

(Imetafsiriwa)

Habari:

“Leo, demokrasia yetu inaning’inia,” alisema Khan katika hotuba yake ya kwanza ya hadhara tangu kuachiliwa huru kwake, akiwataja wale waliomwandama kama “mafia”. Hotuba yake haikupeperushwa kwenye runinga. (The Guardian)

Maoni:

Tangu mwishoni mwa miaka ya 50, uongozu wa jeshi ulianza kuingilia mfumo wa kisiasa wa Pakistan ili kuunda matokeo yanayofaa mapenzi yao.

Ubambanyaji wa kisiasa wa jukwaa la kisiasa la Pakistan uliongezeka wakati wa utawala wa Zia, lakini ulichukua nafasi kubwa wakati wa enzi ya demokrasia katika miaka ya tisiini.

Jeshi hilo lilibuni zana fulani kama vile mashtaka ya ufisadi, hujma, mateso, rushwa, utekaji nyara, mauaji ya kisiasa nk. ili kusimamia vishawishi vya kisiasa na baadaye zana hizi zikawa njia, hatua na mbinu za kuviingiza vishawishi vya kiraia madarakani, kuwasimamia wakiwa madarakani, na kisha kuwavunjia heshima na kuwaondoa madarakani, mara tu wahusika wa kisiasa watakapotimiza malengo yao.

Uongozi wa jeshi uliimarisha njia, hatua, na mbinu hizi wakati wa utawala wa familia ya Bhutto na utawala wa nasaba ya Sharif, wakicheza moja dhidi ya jengine.

Taasisi ya jeshi ilipata uzoefu wa njia, hatua na mbinu hizi, na maafisa wake walikubali zana kama hizo ili kudhibiti ufisadi wa familia ya Bhutto na Sharif kwa badali ya ulinzi wa maslahi ya kitaasisi.

Kwa hivyo baada ya kufanikiwa kutumia zana kama hizo kuunda matokeo ya kisiasa kwa miongo mitatu, Bajwa hakufikiria mara mbili juu ya kutumia zana kama hizo kumkuza, kumsimamia, na kisha kumfukuza Imran Khan.

Hata hivyo, Khan alikemea jaribio la mkuu wa jeshi la kumdhibiti na kupambana naye, hasa baada ya kutimuliwa akifichua majaribio ya COAS ya kumnyamazisha na kumkashifu.

Majaribio haya pia yalisababisha mshtuko katika taasisi ya jeshi na umma. Hii ni kwa sababu wengi walimwona Khan akiwa msafi na mkweli ukilinganisha na ufisadi wa kina wa siasa za utawala wa nasaba na uingiliaji wa mara kwa mara wa uongozi wa jeshi katika kuchezea taasisi ya kisiasa.

Zaidi ya hayo, Khan aliweza kugusa hisia za siri za chuki dhidi ya Marekani za jamii ya Pakistan kwa jumla, lakini hasa vijana ambao walikulia katika ulimwengu wa 11/9 na kulichukia sana tabaka la kisiasa kwa ufisadi uliokithiri na vile vile uongozi wa jeshi kwa kufanya makubaliano mengi kwa vita vya Marekani dhidi ya GWOT.

Bajwa, akifuatwa na Munir, walidhani kwamba zana ambazo jeshi lilikuwa limeimarisha katika ubambanyaji wa kisiasa zingewasaidia vyema katika kumsimamia Khan. Hivyo basi, walimdharau Khan, ngome yake wa ufuasi wa kidemografia katika jamii na wafuasi wake katika taasisi ya jeshi na miongoni mwa maafisa waliostaafu.

Kwa hivyo, nchi sasa iko katika maji ya shingo. Zana zinazotumika kwa ubambanyanji wa kisiasa hazijafeli tu bali pia zimezua hali ya wasiwasi katika taasisi ya jeshi. Hili pia limemnyima Munir mnyumbuko katika kumdhibiti Khan. Fauka ya hayo, hakuna upinzani unaofaa kwa PDM isipokuwa Khan na PTI. Ili uchaguzi mkuu uwe wa kuaminika, jeshi lazima liweke upinzani kama walivyokuwa wakifanya hapo awali. Vyenginevyo, umma hautakubali matokeo.

Wakati matokeo ya ubambanyaji wa kisiasa yamefeli huko nyuma, jeshi limeingilia kati kwa sheria ya kijeshi. Lakini kutokana na upinzani mkali dhidi ya jeshi, kushindwa kwake kumsimamia Khan na sakata ya kisiasa iliyofuata, uchumi uliodhoofika sana, tamko la sheria ya kijeshi sio tu makosa makubwa, lakini itachukuliwa na wengi kama jaribio la kutapatapa kwa Munir kukwamia madarakani kwa gharama yoyote ile bila kushughulikia maelfu ya masuala yenye utata. Pia ni maji ya shingo kwa Khan. Ameibuka na nguvu zaidi kuliko hapo awali, lakini hakuwa na matumaini akiwa madarakani, alifanya mabadiliko ya aibu, alikosa mpango mpana wa mabadiliko na amezungukwa na wanasiasa na washauri waliochafuka ambao wana doa la ufisadi ule ule kama wa wenzao wa PDM.

Kwa hivyo, katika masiku na wiki zijazo, hali ya kisiasa nchini Pakistan itasalia kuyumba, ikitoa fursa za dhahabu kwa watu waliojitolea kuleta mabadiliko msingi. Mabadiliko ambayo yamejikita katika Uislamu na kutaka kung’oa mfumo wa sasa wa kisiasa milele na kurudisha heshima na hadhi katika ardhi iliyo safi.

[مَتَى نَصْرُ اللَّهِ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّهِ قَرِيب]

“Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu!” [Surah Al-Baqarah 2: 214].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu