Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uingereza, kwa Chuki zake dhidi ya Uislamu na Waislamu, Yauita Ulinganizi Wetu wa Kuinusuru Gaza kuwa ni Ugaidi, huku Mikono yao Ikichuruzika Damu yetu, na Wanashindwa Kuuona Ukatili wao Wenyewe kama Ugaidi!
(Imetafsiriwa)

Habari:

Bunge la Uingereza limeidhinisha mipango ya kuliainisha Kundi la Kisiasa la Kiislamu Hizb ut Tahrir kama kundi la kigaidi. Hatua hii inajiri kufuatia ushiriki wa kundi hili katika kuandaa maandamano jijini London, hasa sambamba na maandamano ya waungaji mkono wa Palestina wakati wa mzozo kati ya ‘Israel’ na Hamas. Mabunge ya ‘House of Commons’ na ‘House of Lords’ yaliunga mkono mipango hii, na kutoa njia ya utekelezaji wa haraka wa marufuku hiyo. Kuanzia kesho, kuwa mwanachama wa Hizb ut Tahrir, kupigia debe uungwaji mkono wake, au kuonyesha nembo zake katika sehemu za umma kutazingatiwa kuwa ni kosa la jinai. (Sada Albalad)

Maoni:

Nchi za Magharibi, katika vivuli, wigo, na asili zake zote, zinaendelea kuonyesha meno yake ambayo siku zote zimekuwa makini kuyaficha ulimwengu, haswa Waislamu. Kauli mbiu zote za uhuru, haki za binadamu, ulimwengu huru, wingi wa vyama, na demokrasia zimeyeyuka kwa haraka, kana kwamba ni matone ya maji yanayoanguka kwenye sahani ya moto inayounguza, yakitoweka kwa kasi ili kuthibitisha kwamba hayakuwa chochote zaidi ya udanganyifu, mangati, na uwongo ambao nchi za Magharibi zilijigamba na kujinadi kwazo kwa ulimwengu kwa madhumuni ya ukoloni na kumwaga damu ya watu wake chini ya mwamvuli wake. Hazikukusudiwa kamwe kwa ajili ya maombi au kutabanniwa.

Vita vya kikatili dhidi ya Gaza inayosikitisha vimeziacha nchi za Magharibi zikiwa hazina jani la mtini la kujifinika, huku wakikubaliana kwa kauli moja kulipatia umbile la Kiyahudi usaidizi wa kijeshi, kisiasa, kifedha na kimaadili, na kuliwezesha kuwa bora katika kuua, kuangamiza na kusagasaga. Waislamu, wasio na hatia, watoto, wanawake, na uhai mjini Gaza, yote hayo ni kwa ajili ya kudumisha kambi yao ya hali ya juu ya kijeshi (umbile la Kiyahudi) katikati ya Umma wa Kiislamu, ndani kabisa ya ulimwengu wa Kiislamu. Walijihalalisha ukatili na usaidizi huo, licha ya kutokuwa na dini moja, utamaduni, rangi, au lugha moja. Hakuna kisingizio cha msaada huo, kana kwamba wanashiriki dini moja, rangi moja, utamaduni mmoja, au lugha moja, au angalau; wanaihalalisha kwa lugha ya uadilifu, ubinadamu na haki.

Hata hivyo, wanaendelea kuwapa Mayahudi vilipuzi, makombora na mabomu ambayo yameharibu kila kitu, na Waziri Mkuu wa Uingereza mwenyewe aliibuka bila kudhurika kutokana na kukumbatia makombora na vilipuzi hivyo, ambavyo yeye binafsi alivileta ndani ya ndege ya usafiri wa kijeshi. Yote haya yanachukuliwa kuwa ya kawaida na bila wasiwasi wowote kwao. Hawayaiti kuwa ni ugaidi au ukatili, ingawa yanadhihirisha kilele cha ugaidi na ukatili kwa kuua watu wasio na hatia, watoto na wanawake, na kuharibu shule, mahospitali na misikiti.

Kwa upande mwingine, makruseda hao wanachukulia kwamba Muislamu kumnusuru ndugu yake na kuonyesha mshikamano wake na wale wanaoshiriki dini, lugha, kabila, utamaduni mmoja, na kupigia debe ushindi wao, hata kama ni wito tu kupitia lugha, fikra, na hoja, inahesabika kuwa ni kitendo cha kigaidi ambacho kilihalalisha kupigwa marufuku kwa Hizb na kuitaja kuwa ni shirika la kigaidi!! Ajabu ilioje hii! Wale wanaowatetea wanaodhulumiwa na wanaokandamizwa wanahesabiwa kuwa ni magaidi, huku wanaomrushia mhalifu mabomu na silaha wanachukuliwa kuwa ni njiwa wa amani!!

Hii ni miaka ya misukosuko ambayo imerefuka juu ya Umma wa Kiislamu; Magharibi mhalifu asiye na maadili, kanuni, na ubinadamu, akiigeuza haki kuwa batili na batili kuwa haki. Huku akifichua meno yake bila kujali sura yake, watu wake, au ulimwengu, ni kama umbile la kinyama la Kiyahudi lenye shauku ya kukabiliana na Umma wa Kiislamu na kukabiliana na kuhisabiwa kunakokaribia, InshaAllah. Hapo Mwenyezi Mungu atazima batili, dhulma na ukoloni, na ataithibitisha haki, na ataupa ushindi Uislamu na Waislamu. Watarudi kama mabwana wa ulimwengu, wakiiongoza kuelekea kwenye uadilifu, furaha, na utulivu. Uingereza, wala Marekani, wala Magharibi yote hazitanufaika na kila wanachokifanya ili kuzuia mwamko wa Ummah na kuregea kwake mahali pake panapostahiki. Ushindi wa Mwenyezi Mungu hauepukiki na agizo lake halitazuiliwa na nguvu yoyote juu ya uso wa ardhi. Sisi na wao hakika tutakutana,

[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ]

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Ash-Shu'ara:227].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Mhandisi Baher Saleh
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu