Jumamosi, 30 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mithili ya Watawala wa Kiarabu, Watawala wa Kiajemi Wanaitelekeza Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 18 Januari 2024, mrengo vyombo vya habari wa Jeshi la Pakistan, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Nambari PR-18/2024-ISPR, lilisema, “Katika masaa ya mapema ya tarehe 18 Januari 2024, Pakistan ilifanya mashambulizi thabiti dhidi ya maficho ndani ya Iran yaliyotumiwa na magaidi waliohusika na mashambulizi ya hivi karibuni nchini Pakistan. Mashambulizi hayo ya usahihi yalifanywa kwa kutumia droni za muuaji, roketi, risasi za mzunguko na silaha zilizosimama. Utunzaji wa kiwango cha juu ulichukuliwa ili kuzuia maangamivu kwa wasiowapiganaji.”

Maoni:

Mashambulizi hayo ya Pakistan ndani ya Iran, yalijiri siku moja baada ya mashambulizi ya Iran nchini Pakistan. Majeshi yote sasa yanajivunia juu ya utayari wao wa kupambana na ugaidi. Kwa hivyo, ni vipi kuhusu ugaidi ambao uvamizi wa Wazayuni umeufanya kwa zaidi ya siku 100? Je! Ni vipi kuhusu ulinzi wa Waislamu zaidi ya milioni katika Kivuko cha Mpakani cha Rafah, kwenye mpaka wa Ukanda wa Gaza na Misri? Wanakabiliwa na kifo kupitia mabomu, kudenguliwa, baridi, njaa na kiu, huku Firauni wa Misri, As-Sisi, analipisha maelfu ya dolai, kwa kila mtu, kwa kivuka kwao! Je! Droni na makombora zinarushiwa tu Waislamu, na sio kwa umbile katili, la vurugu la Mayahudi? Ni vipi hivyo, wakati Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ]

“Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao.” [Surah Al-Fath 48:29]? Vipi! Umma wa Kiisilamu unanyimwa siku ambayo droni zake na makombora zitapiga majeshi ya Mayahudi?

Kwa yakini, Umma wa Kiislamu na majeshi yake watafadhaishwa tu na uongozi wa sasa. Haishangazi kwamba maafisa wa Kiislamu wanasukumwa kuondoka jeshini, kuweka vichwa vyao chini huku wakingojea kustaafu au kufifia kwa hasira na mfadhaiko. Kwa kweli, majeshi ya Waislamu yanahitaji uongozi ambao huitendea kazi Quran Tukufu, badala ya kuisoma na kuihifadhi tu. Mwenyezi Mungu (swt) ameamuru,

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah 2:191] Hii ndio sababu kamanda wa jeshi Salahudin Al-Ayubi aliikomboa Palestina, baada ya kuwaunganisha Waislamu kwa kuwaondoa wasaliti kati yao… na hii ndio sababu Khalifa Abdul Hameed II, akitawala juu ya Waajemi na Waarabu, aliilinda kwa nguvu kamili ya Umma wa Kiislamu.

Ewe Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Ni kipi kinacho kuzuieni kuuondoa uongozi wenu tayari, na kutaharaki kuikomboa Palestina? Jueni kuwa utiifu kwa uongozi wenu wa sasa hautakuokoeni kutokana na adhabu Siku ya Kiyama. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوفِ»  “Hakika, utiifu ni katika jambo jema pekee.” [Ahmad]. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «لَا طَاعَةَ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ» “Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi There is no (معصية) Mwenyezi Mungu.” [Muslim]. Imeripotiwa pia katika Ibn Majah na Ahmad kwa riwaya sahih kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «مَنْ أَمَرَكُمْ مِنْهُمْ بِمَعْصِيَةِ اللَّهِ فَلَا تُطِيعُوهُ» “Yeyote miongoni mwao anayekuamrisheni kumuasi Mwenyezi Mungu basi msimtii.” Msiruhusu watawala kuharibu Akhera yenu. Msiruhusu wasimame katika njia yenu ya kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu (swt), kupata ushindi na shahada. Muondoeni mtawala yeyote anayesimama katika njia yenu ya kuikomboa Gaza, iwe ni kutoka kwa watawala wa waajemi au watawala wa Waarabu, pamoja na wale walio katika dola jirani na Palestina.

Je! Mnaaminije kuwa mtakuwa peke yenu katika harakati hii ya kihistoria na ya kishujaa? Hakika hamuko peke yenu, ikiwa mtasonga kuwaondoa wasaliti wanaokuzuieni. Zaidi ya yote, Mwenyezi Mungu (swt) yuko pamoja nanyi, ikiwa munatii amri yake. Hata watu wasio Waislamu hawataomboleza baada ya kuwaondoeni watawala na kuhamasisha kwa ajili ya Gaza, kwani mamilioni tayari wanapinga dhidi ya uhalifu wa vikosi vya Mayahudi. Ama Waislamu, wanashtuka kuwa bado mungali hamujasonga, kwa hivyo watakuungeni mkono kikamilifu mtakapofanya hivyo. Ama ule uongozi wa kisiasa unaohitajika kwa ajili ya kupanga na uratibu, munajua vyema kuwa Hizb ut Tahrir inafanya kazi kupata Nusra ya nyenzo ili kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, katika zaidi ya nchi moja ya Kiislamu. Mara tu mtawala mmoja wa Waislamu atakapopinduliwa, kutakuwepo na upinduaji wa kimaumbile wa wasaliti, mmoja baada ya mmoja, kwa mfululizo wa haraka. Kwa hivyo, vipi basi msiwe jeshi la kwanza kuwapindua wasaliti hawa, badala ya kuwa wa pili, wa tatu au wa mwisho kufanya hivyo?

Vita vimeanza na bado hamjakabiliana na adui. Basi jibu, enyi maafisa wa jeshi la jeshi la Pakistan, au mnangojea adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt). Ogopeni kukaa bila ya kutaharaki, kwamba ghadhabu kutoka kwa Mola wenu (swt) iwashukie juu yenu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache (38). Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu (39).”  [Surah At-Tawbah 9:38-39].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu