Jumanne, 07 Shawwal 1445 | 2024/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Uhakiki wa Habari 20/08/2022

Waziri Mkuu wa Zamani wa Australia Ashikilia Nyadhifa Nyingi za Baraza la Mawaziri

Ilifichuliwa wiki hii kwamba Waziri Mkuu wa zamani wa Australia Scott Morrison alichukua mamlaka kwa siri ya nyadhifa nyengine tano za baraza la mawaziri alipokuwa akiongoza serikali. Kwa mujibu wa ‘The Guardina’:

Waziri mkuu, Anthony Albanese, anasema Scott Morrison aliteuliwa kwa wizara tano za ziada, ikiwa ni pamoja na Hazina na mambo ya ndani, akitaja hatua za mtangulizi wake kuwa ni "utupwaji usio na kifani wa demokrasia yetu".

Waziri wa awali wa maswala ya ndani, Karen Andrews, amemtaka Morrison kujiuzulu kutoka bungeni kufuatia ufichuzi huo, lakini kiongozi wa upinzani, Peter Dutton, anasimama na kiongozi wake wa zamani.

Ken Wyatt, waziri mwenzake wa zamani, amemkashifu Morrison kwa kutoheshimu baraza la mawaziri kama "chombo muhimu katika serikali ya Westminster", lakini akamtaka abaki bungeni ili ahesabiwe.

"Inavunja moyo demokrasia yetu," Wyatt alisema. "Nilichanganyikiwa tu, sikuwa na ufahamu wowote juu hilo."

Katika mfumo wa kidemokrasia, serikali huchukuliwa kuwa inaendeshwa na chombo cha pamoja, baraza la mawaziri, na sio kiongozi mmoja. Msemo ‘Wa kwanza kati ya walio sawa’ hutumika kuelezea wajibu wa Waziri Mkuu haswa.

Kila waziri kinadharia anachukuliwa kuwa mtawala huru wa wizara yake mwenyewe. Katika nchi za demokrasia, mamlaka ya tawi la baraza la mawaziri pia yanabanwa, huku idara huru ya mahakama na bunge huru zikiundwa ili kuyasawazisha. Wazo la utenganishaji wa mamlaka lililetwa kwa mara ya kwanza na mwanafalsafa Mfaransa Montesquieu katika karne ya 18, ambaye alimshambulia mfalme wa Ufaransa kwa kumlinganisha na Khilafah Uthmani. Kulingana na Montesquieu, kumpa mamlaka mtawala mmoja ni udikteta; badala yake mamlaka yanapaswa kugawanywa miongoni mwa wengi serikalini, na ‘uangalizi na mizani’ uimarishwe ili kuhakikisha kwamba viongozi wa serikali wanabaki waaminifu kwa umma.

Dhana hii, bila shaka, inagongana na maumbile ya mwanadamu. Juhudi zote za pamoja zinahitaji mtu mmoja kuziongoza na kuziratibu, iwe serikali, jeshi, biashara, au nyenginezo. Kwa hivyo, licha ya nadharia hiyo, mawaziri wakuu na maraisi wengi huishia kuwa viongozi wenye nguvu zote. Fauka ya hayo, ‘uangalizi na mizani’ kwa kweli hufanya kazi ili kuwezesha maslahi yaliyopo nje ya serikali. Uwajibikaji halisi unatokana na kumpa mamlaka kamili mtawala mmoja mmoja ili umma ujue ni nani haswa wakumuelekezea masuala yao yote.

Nchini Australia, kuna shida zaidi, ambayo ni kutawaliwa kwake na Amerika na Uingereza. Katika karne ya 20, Chama cha Liberal cha mrengo wa kulia kilibakia kuwaunga mkono Waingereza huku chama cha Labour cha mrengo wa kushoto kikiunga mkono Marekani. Lakini katika karne ya 21, mzozo wa Marekani na Uingereza umeenea ndani ya kila chama, kama inavyoonekana katika mapambano kati ya Kevin Rudd na Julia Gillard katika Chama cha Labour, na mapambano kati ya Malcolm Turnbull na Tony Abbott katika Chama cha Liberal. Scott Morrison alikuwa mgombea wa maridhiano katika pambano la mwisho. Ni mapambano haya ya ndani ya makundi yaliyokabiliwa na Morrison ndiyo yaliyomlazimisha kujinyakulia mamlaka ya mawaziri wengine kwake.

Fahamu za Kimagharibi kama vile demokrasia na dola ya kitaifa ya Westphalia zimewahadaa wanadamu. Kiuhalisia dunia haijaundwa kwa dola nyingi huru; mfumo wa kiulimwengu unatawaliwa na dola kubwa chache ambazo hufanya maamuzi mengi kwa ajili ya wanadamu wote, dola hizo kubwa zenyewe zinatawaliwa na kipote cha warasilimali wachache. Kwa kweli hili ndilo linaloelezea viwango vya jumla vya ukosefu wa usawa na unyonyaji katika ulimwengu wa sasa. Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt) Ummah wa Kiislamu hivi karibuni utanyanyuka na kusimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) ambayo itaziunganisha ardhi za Waislamu, kukomboa ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu, kutabikisha sharia ya Kiislamu, kurejesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu na kubeba nuru ya Uislamu kwa ulimwengu mzima. Dola ya Khilafah itatabikisha mfumo wa utawala wa Kiislamu badala ya fikra za Kimagharibi za demokrasia na udikteta, ambapo Khalifa atalazimika kimkataba kutabikisha Uislamu kupitia kiapo cha utiifu (bay’ah) anachokichukua kutoka kwa Umma wa Kiislamu. Dola ya Khilafah, tangu kuanzishwa kwake, itajiunga na safu za dola kuu kutokana na ukubwa wa eneo lake, idadi kubwa ya watu wake, rasilimali zake nyingi, jiografia yake isiyo na kifani na mfumo wa kipekee wa Kiislamu. Kwa hivyo itakuwa katika nafasi ya kupambana na mfumo wa kiulimwengu unaotawaliwa na Magharibi na kufichua uhalisia wake mbaya kwa wanadamu wote. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika Hadith moja iliyoripotiwa na Thawbaan (r.a.) na iliyokusanywa na ibn Maajah:

«إِنَّ اللَّهَ زَوَى لِيَ الأَرْضَ فَرَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا وَإِنَّ أُمَّتِي سَيَبْلُغُ مُلْكُهَا مَا زُوِيَ لِي مِنْهَا»

“Mwenyezi Mungu alinikundulia pembe zote za ardhi pamoja, basi nikaona mashariki yake na magharibi yake. Na hakika Umma wangu utawala wake utafika katika pembe zote za ardhi iliyo kunduliwa kwangu.”

Mkutano wa Kisiri wa Uongozi wa China huko Beidaihe Wamalizika

Kwa mujibu wa BBC:

Rais wa China Xi Jinping alizuru mkoa wa kaskazini mashariki wa Liaoning mnamo Jumanne, vyombo vya habari vya serikali viliripoti, wakati yeye na viongozi wengine walipozuka baada ya kutoweka kutoka kwa shughuli za umma kwa wiki mbili, na kueleza walikuwa kwenye mkutano wao wa kiangazi wa kila mwaka ...

Kabla ya Jumatano, hakukuwa na ripoti za vyombo vya habari vya serikali kuhusu shughuli za Xi kwa muda wa wiki mbili - kwa kawaida shughuli zake huangaziwa kila siku - ishara kwamba yeye na viongozi wengine wakuu walikuwa na mkutano wao wa kawaida wa kisiri wa kiangazi katika hoteli ya baharini ya Beidaihe mashariki ya Beijing.

Wageni wa Beidaihe na wakaazi walisema usalama umekuwa mkali sana huko katika wiki za hivi karibuni.

Kongamano la mwaka huu la Beidaihe litakuwa muhimu sana, kwani viongozi wanatarajiwa kujadiliana kuhusu hatua za wafanyikazi kabla ya kongamano la chama tawala cha Kikomunisti la mara moja katika miaka mitano litakalofanyika baadaye mwaka huu.

Xi anatarajiwa sana kupata muhula wa tatu wa uongozi wa miaka mitano katika mkutano ujao wa chama.

Waziri Mkuu Li Keqiang pia aliibuka tena wiki hii baada ya kutoweka kutoka kwa shughuli za umma kwa wiki mbili. Alitembelea mji wa kusini wa Shenzhen na kufanya mkutano kwa njia ya video mnamo Jumanne kuhusu uchumi pamoja na viongozi kutoka baadhi ya mikoa mikubwa zaidi ya China.

Vyombo vya habari vya Magharibi vinapenda kumuonyesha Rais Xi Jinping wa China kama mtawala dikteta anayeweka matakwa yake juu ya watu wa China. Nchi za Magharibi daima zimewaonyesha wapinzani wake kwa njia hii tangu Montesquieu alipofanya hivi kwa Sultan wa Kiuthmani, kama ilivyotajwa hapo juu. Lakini ukweli ni kwamba China inakabiliwa na makundi ya ndani kama nchi zengine. Kwa upande wa China kuna makundi mawili kila moja likiongozwa na watangulizi wa hivi punde wa Rais Xi Jinping, kipote cha mabwenyenye na Kikundi cha Shanghai mjini kinachoongozwa na Jiang Zemin, na Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa vijijini unaoongozwa na Hu Jintao. Makundi haya mawili ya China yote yalikutana na kukubaliana juu ya uteuzi wa Xi Jinping muongo mmoja uliopita. Na makundi yote mawili lazima yaungane sasa ili kupata muhula wa tatu wa rais Xi Jinping ambao unatarajiwa kutangazwa kwenye hafla ya kongamano la miaka mitano baadaye mwaka huu.

Kuwepo kwa makundi ya ndani ni saratani kwa mfumo wowote unaotawala. Makundi ya China yalitokea kwa sababu ya kutabanniwa kwa kikomo cha muhula wa rais na kiongozi wa China Deng Xiaoping kabla ya kufariki. Deng na warithi wake kama rais, Jiang na Hu, wangeacha dori yao rasmi lakini wangebaki na nguvu za kutosha kukuza makundi yao ndani ya serikali. Kama vile uangalizi na mizani yaliyo hapo juu, vikomo vya muda ni kifaa kingine ambacho kinasemekana kunufaisha watu lakini kwa hakika kinawanufaisha kipote cha wachache. Dola ya Khilafah hailazimishi vikomo bandia vya muhula kwa mtawala wake. Anaendelea maadamu ana uwezo wa kutekeleza majukumu yake, na maadamu anabaki ndani ya mipaka ya Uislamu. Mdhibiti wa Khalifa ni Uislamu wenyewe, ambao Shariah yake isiyobadilika isiyoweza kutumiwa vibaya na mtawala yeyote hata awe na nguvu kiasi gani. Zaidi ya hayo, hata hivyo, Dola ya Khilafah inapaswa kufanya kazi ya kujenga mazingira ya kisiasa yenye nguvu, ya wazi, safi, na ya siasa za umma yenye vyama changamfu vya kisiasa na mabaraza mahiri ya uwakilishi ili wale wenye uwezo wapeleke mawazo yao kwa Ummah badala ya kuishi katika vivuli, wakijaribu kutumia vibaya korido za utawala. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ameshajiisha misimamo ya kijasiri ya kisiasa na kupinga matumizi mabaya ya mamlaka katika Hadith iliyopokelewa na Jabir:

«سَيِّدُ الشُّهَدَاءِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حَمْزَةُ بْنُ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ وَرَجُلٌ قَامَ إِلَى سُلْطَانٍ جَائِرٍ فَأَمَرَهُ بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَاهُ عَنِ الْمُنكر فَقتله»

“Bwana wa mashahidi wote Siku ya Kiyama ni Hamza bin ‘Abdil Muttalib, na mtu atakayesimama kwa Sultan jeuri akamwamrisha mema na akamkataza maovu kisha (Sultan) akamuua.”

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu