Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali

Uhakika wa Harakati ya Eneo la Kusini na Utiifu Wake

 (Imetafsiriwa)

Swali:

Je, Harakati ya Kusini (Al-Hirak Al-Janoubi) bado ni Amerika? Au wakala wa baraza hilo uligeuka kuwa wa Uingereza kutokana na kudhibitiwa na Imarati na kugeuka kuwa mfuasi wa Imarati, na Imarati inawakilisha Uingereza nchini humo? Kwa maana nyengine, je, Amerika ilishindwa kuidumisha Harakati hii ya Kusini na Uingereza kupitia Imarati kuweza kuivuta upande wake? Au bado ingali ni mfuasi wa Amerika katika hatua zake, na Imarati kutokana na nguvu ya jeshi lake mjini Aden, kuweza kuishawishi pekee pasi na Harakati hii ya Kusini kuwa na utiifu kwa Uingereza?   

Jibu:

1- Uingereza ilipata wasiwasi kugundua kuwa Amerika iliweza kuwashawishi Ali Salem Al-Beidh na Ali Nasir Mohammed kwa njia za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kupitia Misri na Saudi Arabia katika enzi za Fahd katika miaka ya tisini mwanzoni ingawa Uingereza ndiyo iliyo unda, kupitia vibaraka wake, ile iliyoitwa “Harakati ya Kitaifa ya Ukombozi Eneo la Yemen Kusini” na kuikaribisha katika majadiliano jijini Geneva kuanzia mnamo 20/11/1967. Kisha Uingereza kulipa uhuru eneo la Kusini mwa Yemen mnamo 30/11/1967 baada ya kuondoka kwa vikosi vya Uingereza, na Al-Beidh kuwa gavana wa eneo la Kusini kwa usaidizi kutoka kwa Uingereza. Hivyo basi, uhusiano wake na Amerika ulikadiriwa na Uingereza kuwa kama fedheha! Hivyo, Uingereza ikaamua kumuondoa mamlakani, hususan kwa kuwa inao uwezo wa kufanya hivyo, kwa kule kuwa mtu wake Ali Saleh ana nguvu inayo tambulika eneo la Kusini.  

Hivyo basi, vita vikazuka baina ya majeshi ya sehemu mbili hizi mnamo 1994, miaka minne tu baada ya kuunganishwa kwa sehemu mbili hizi za Yemen! Ambapo vita vilimalizika kwa kushindwa kwa majeshi yaliyo tambuliwa kama “ya Kusini”, Ali Salem al-Beidh na Ali Nasser Mohammed wakatoroka, na kujitenga kando kiasi.

Wakati huo serikali ya Saleh mjini Sanaa ilikuwa imeanza kuwatesa na kuwaandama wanajeshi wa eneo la Kusini kwa miaka kadhaa. Hatimaye, shirikisho la wanajeshi wastaafu likaanzishwa eneo la Kusini, kwa hivyo kikawa ni chama chenye matakwa yanayo husiana na ugandamizaji, mateso na kunyimwa haki. Kwa kuendelea kudumu kwa dhulma hizi, hisia ya kujitenga ikapenya katika wakongwe hawa wa kijeshi waliomo ndani ya shirikisho hili, na hivyo basi kugeuka kuwa jukwaa moto la hisia ya kutaka kugawanywa kwa nchi, na kitovu cha kikundi cha wanaotaka kujitenga ambao harakati zao zilipelekea kuibuka kwa ile inayo julikana kama Harakati ya Kusini (Al-Hirak Al-Janoubi), ambayo ilijitangaza rasmi eneo la Kusini mwa Yemen mnamo 2007 kuongezea pia harakati nyenginezo zisokuwa na umuhimu sana na zenye athari hafifu ambazo hatutaziangazia juu yazo.  

2- Amerika iliitumia hali hii ya eneo la Kusini kutia mguu wake eneo la Kusini mwa Yemen, kama ilivyo tia mguu wake mwengine katika eneo la Kaskazini mwa Yemen kupitia harakati ya Mahouthi na usaidizi wa Iran kwake. Hivyo basi, kwa mujibu wa mzozo wa kimataifa, Harakati hii ya eneo la Kusini imegura kutoka kwa matakwa ya kuondolewa kwa dhulma na sasa kugeuka kuwa kifaa kipya cha Amerika cha kuingilia mambo nchini Yemen ambayo serikali yake ni tiifu kwa Uingereza.

Dola kuu kama desturi yazo zimekuwa zikipatiliza hali za kindani na mivutano katika nchi ndogo kujipatia ushawishi ndani yake. Amerika, kupitia Huduma ya Ujasusi ya Mfalme Fahd nchini Saudi Arabia, ilijaribu kuwasiliana na wanamgambo eneo la Kusini mwa Yemen katika miaka ya tisini baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo 1994. Ingawa Salem Al-Beidh alikuwa mmoja wa wafuasi wake wakati huo, kujitenga kwake kando wakati huo na kulingania kwake shughuli ya kisilaha dhidi ya utawala wa Saleh, akiwa mafichoni mwake, hakukuifanya Amerika kuliona hilo pekee kama mafanikio na ikaanza kumtafuta mtu mwengine atakaye tabanni mapambano imara ya kisiasa ili kuwakusanya watu wa eneo la Kusini kuwa pote litakalo tia shinikizo kali na kuathiri utawala wa Saleh vilivyo. Amerika ilipata njia yake kupitia mwanaharakati wa upinzani, Hassan Baoum, ambaye alikuwa anakwenda kwa kasi mno katika kuitisha kujitenga kwa eneo la Kusini mwa Yemen, na kuraukia mji mmoja hadi mwengine, na kuyazungukia makabila kwa bidii akiyarai kumuunga mkono yeye na matakwa yake ya kujitenga. Yote hayo ni athari ya mateso na kutelekezwa kwa watu wa eneo la Kusini. Baoum alikuwa akifanya tukio moja hadi jengine ili kujenga rai jumla ya kutaka kutengwa kwa eneo la Kusini kutoka kwa Yemen, kwa kufuata mwelekeo wa amani na kupinga ghasia. Ilionekana kuwa harakati za Hassan Baoum zilikuwa zinapaza sauti na wakati mwengine kupanda kasi katika maeneo ya Kusini ambako fikra ya kutelekezwa ilikuwa imekita mizizi kama sera imara.  

Alikamatwa na kushtakiwa na serikali ya Sana’a, ambapo alikamatwa mara kadhaa kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja baina ya mwaka wa 2007 na 2008. Alikamatwa tena mnamo 2010 na kuachiliwa baada ya miezi miwili mnamo 2011 na kukamatwa tena mwaka huo huo. Hivyo basi, mwanaharakati wa kujitenga, Baoum, akawa nembo kuu ya Al Hirak, harakati ya kujitenga eneo la kusini, kwa juhudi zake zisochoka, kuchochea kwake wakongwe wa kijeshi, makabila na wanaharakati dhidi ya serikali kuu jijini Sana’a, kwa kule kupanda kwake na kumakinisha matakwa ya kujitenga, mafungamano yake na Amerika na kukubali kwake usaidizi wa Iran. Baoum amesifiwa kwa harakati za kasi, hivyo akaunda Baraza Kuu la Harakati ya Eneo la Kusini na kuwa Raisi wake. Baraza hilo Kuu la Harakati ya Amani ya Ukombozi wa eneo la Kusini ni sehemu kuu ya Al Hirak, ambayo pia inajumuisha makundi mengine yakiwemo Baraza Kuu la Kitaifa la Uhuru wa eneo la Kusini, Baraza Kuu la Ukombozi na Kuregesha Dola ya Yemen Kusini, Jumuiko la Kidemokrasia la Eneo la Kusini na Muungano wa Vijana na Wanafunzi wa Eneo la Kusini… mkoa wa Dhale ni moja ya mikoa michangamfu na maeneo moto zaidi ya Al Hirak… (Chanzo: tovuti ya Al Jazeera Net 3/3/2011). Tovuti nyenginezo zilimsifu waziwazi kuwa kibaraka wa Iran kama ilivyo tajwa katika tovuti ya hunaaden.com mnamo 13/9/2016. Hivyo basi, Harakati ya Kujitenga ya Eneo la Kusini inayo ongozwa na Hassan Baoum, aliye patiliza utelekezaji, ni harakati ya kisiasa inayo husishwa na usaidizi wa mwanzoni wa Amerika na kuwa kitovu ambacho kwacho Amerika inaweza kukitumia kuingia Yemen kupitia eneo la Kusini vile vile. Harakati hizi, matukio na mashambulizi haya yalitekelezwa na Al Hirak, na kitovu chake kilikuwa mji wa Dhale. Ingawa Hassan Baoum Hadhrami anatoka Mukalla, na sio Dhale, harakati zote hizi zimehudumu kama vituo vya mafunzo ya kazi ya kisiasa kwa kundi hili. Serikali ya Sana’a mwanzoni haikuiona harakati hii kuwa hatari kwa sababu kazi zake kuu zilikuwa za kisiasa, na hivyo basi, ilikuwa tu ikizikamata nembo zake pekee kama Hassan Baoum, Ahmed bin Farid, Ali al-Gharib na Ali Manasra kwa muda fulani, na kisha kuwaachilia.   

3- Hivyo basi, vibaraka wa Amerika katika Harakati ya eneo la Kusini wamepewa ujuzi na kumakinishwa katika wazo la kujitenga, ambayo imekuwa fikra kwao. Huku, wengine waliovutwa na matendo ya Harakati ya eneo la Kusini, inayo chochewa na hisia ya kutelekezwa; baadhi yao ni wanaharakati wa kieneo, na wengine wako chini ya ushawishi wa Uingereza na vibaraka wao nchini Yemen, na mfano wa hawa walikuwa wakati mwengine wakiunga mkono umoja wa nchi na wakati mwengine wakiunga mkono kujitenga kwa nchi, ambapo kujitenga kwa nchi haikuwa fikra yao. Serikali jijini Sana’a ilikuwa ikinufaika na haya kwa kupunguza chachu fikra ya kujitenga kwa nchi ambayo imezungukwa na vibaraka wa Amerika, na ilikuwa ikipenya katika baadhi ya vibaraka wake kwa lengo hilo hilo. Kama tulivyo sema, serikali jijini Sana’a haikuwaona kuwa hatari, lakini ilipo dhihirika kwa serikali ya Raisi Saleh jijini Sana’a na Waingereza nyuma yake kwamba harakati hii inaongeza kasi na kwamba matishio yake yanazidi kuongezeka hususan kwamba vibaraka wa Amerika wako mstari wa mbele katika harakati hii, dola jijini Sana’a, pamoja na Waingereza na wafuasi wao wa kieneo, waliitulizia makini harakati hii ili kuidhibiti, hususan kwa kuwa ilionekana kuwa vigumu kuimaliza huku hisia za kutelekezwa zikikua eneo la Kusini. Mpango “Waingereza” wa kuidhibiti ni kuundwa kwa mujibu wa matukio ya harakati eneo la Kusini, kutokana na majaribio hatari ya kupenya katika kuandama ambayo hayakufungika tu na ukamataji, bali pia kuhusisha ghasia. Hili liliendelea mpaka Imarati ilipo ingia na majeshi yake ya ardhini, kwa kutumia kisingizio cha kuwemo ndani ya muungano wa Waarabu na kisha kushambulia vikali baada ya kufariki kwa Saleh ambapo ushawishi wa Uingereza eneo la Kaskazini ulififia na kuogopea kuwepo kwa pengo endapo Mahouthi watafanikiwa katika kupanua athari yao eneo la Kaskazini. Hivyo basi, ilianza kufikiria kwa makini jinsi ya kuwa na nguvu Kusini itakayo tia shinikizo la kuwepo kwake katika utawala wa Yemen; au hata angaa eneo la Kusini. Kwa hivyo, ilianza kufikiria kwa makini juu ya kumakinisha athari yake eneo la Kusini, hususan kwa kuwa haikuwa ikimtegemea Hadi pekee, kwa kuzingatia kuwa ametawaliwa na Saudi Arabia, hivyo basi ililishughulikia hili kupitia Imarati, pamoja na kuanzisha majeshi ya aliyekuwa Raisi wa Yemen, aliye uwawa na Mahouthi mwishoni mwa mwaka jana mnamo 4/12/2017, yaliyoanza kurudi Kusini na kupangwa na majeshi ya Imarati katika kupigana na Mahouthi. “Duru kutoka kwa serikali ya Yemen zimethibitisha kuwa Tarek Saleh, mpwa wa Ali Saleh, alikuwa mjini Aden chini ya hifadhi ya majeshi ya Imarati. Duru za kidiplomasia zimesema kuwa Imarati inatia juhudi kubwa kuondoa vikwazo vilivyo ekewa juu ya Ahmed bin Ali Saleh ili kucheza dori ya kisiasa siku za usoni”. (Chanzo: Nass Times, tovuti ya Yemen 5/2/2018), “Tutamuunga mkono Tariq Saleh na tutasimama na yeye katika eneo la Kaskazini na katika maeneo yote mpaka Sana’a itakapo kombolewa kikamilifu”, alisema kamanda wa majeshi ya Baraza la Mpito la eneo la Kusini (30/1/2018, France 24). Hii yamaanisha kuwa Uingereza inacheza mchezo eneo la Kusini na kutia nguvu athari yake pamoja na vibaraka wake kutoka kwa jamaa za Ali Saleh wenye ushawishi katika Kikosi cha majeshi ya Kijamhuri ya Yemen na chama cha General Congress. Wanaharakati wa kujitenga walisaidiwa na Imarati, wakijua kuwa Imarati inashiriki kwa majeshi ya angani na ardhini, huku Saudi Arabia ikishiriki kwa majeshi ya angani pekee.

4- Kwa hivyo, Uingereza ilianza kuhudumu eneo la Kusini kupitia Imarati ili kupenya ndani ya Harakati asili ya eneo la Kusini au kuipiga teke kupitia kuunda harakati mpya itakayo ongoza mandhari. Imarati ilianza na mrengo wa Ali Saleh Al-Beidh ingawa Uingereza ilijua uzito wa majaribio ya Amerika ya kumuunga mkono Ali Saleh Al-Beidh na Ali Nasser. Majaribio hayo ya Amerika yanajumuisha kuisaidia Iran, huduma za Misri, kama mkutano wa Harakati ya eneo la Kusini jijini Cairo chini ya uongozi wa Ali Nasser Mohammad mnamo 2014, na huduma za Lebanon, ambapo Beirut imempa Ali Saleh Al-Beidh makao na jukwaa la vyombo vya habari ambavyo alinyimwa na Oman tangu alipo taka hili mnamo 1994. Halafu, kwa kuzuka kwa kimbunga cha Saudia mnamo 2014, alikwenda Riyadh, ambako alipewa chungu ya pesa. Lakini, kama tulivyo tangulia kusema, Imarati imeanza kuujaribu ushawishi wa mrengo wa Al-beidh na Nasser. Ama kuhusu ni kwa nini imeanza na mrengo huu, ni kwa sababu mbili: Kwanza, kwa sababu anatabanni ghasia, na ya pili ni historia ya utiifu wake kwa Waingereza, kwani walikuwa nyuma ya kuundwa kwa chama chake cha National Front na kuukabidhi utawala wa Yemen Kusini kwake yeye. Kwa hivyo, walimtaka aishi kwa kumbukumbu za enzi hizo, ili wamrudishe kwake au kumkaribisha nao na kuuimarisha. Kufuatia kuanzishwa kwa operesheni za muungano wa Waarabu nchini Yemen mnamo 2015, Al-Beidh alipewa uhamisho kutoka Saudi Arabia hadi Imarati ambako kwa sasa anaishi Abu Dhabi, anaingia katika nchi ambazo ni tiifu kwa Amerika, kwa hivyo ameishi nchini Lebanon kwa takriban miaka miwili (2012 na 2013) akiungwa mkono na Iran na kuhifadhiwa na chama chake huko, kisha kwenda Saudi Arabia na hatimaye kuchukuliwa na Imarati kwa kuwemo kwake ndani ya muungano huo, na kumhamisha kwake kama tulivyo taja awali ambapo anaishi Abu Dhabi na kumzunguka na mazingira ya heshima. Inajulikana kuwa Salem Al-Beidh ni kigeugeu katika utiifu wake; alikuwa mtiifu kwa Waingereza alipo kuwa raisi wa Yemen Kusini na kisha mwanzoni mwa miaka ya tisini alitongozwa na Amerika na kubakia katika utiifu wake huu huku akisafiri katika nchi vibaraka wa Amerika, na sasa yuko Imarati ambayo inajaribu kumtongoza tena, ambapo si ajabu kwake kubadilika tena, na kama itatokea, mambo yaweza kuwa moto baina yake na Imarati. Lakini, msimamo wake uko karibu na Baraza la Mpito na amelisifu: “Aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Yemen, Ali Salem Al-Beidh, ametangaza kuunga mkono kwake kuundwa kwa “umbile la kisiasa la eneo la Kusini”, siku moja baada ya magavana watatu katika majimbo ya Kusini kumuunga mkono gavana wa Aden, Aideros Zubaidi kuunda umbile hilo. Al-Beidh alithibitisha, katika taarifa iliyo pokewa na gazeti la “Al-Arabi Al-Jadeed”, kuwa angeunga mkono mwito huu “kwa njia zozote ziwezekanazo” na kuzisihi nguvu kadha wa kadha za kisiasa eneo la kusini na watu binafsi “kuamiliana kwa uzuri na mwito huu na kujitoa kutoka katika hali ya matarajio, ikhtilafu na kutegemea hatua mpya”. Taarifa ya Al-Beidh imekuja siku moja baada ya magavana watatu, gavana Abyan, Khidr al-Saidi, gavana wa Lahi, Nasser Al-Khange, na gavana wa Dhale, Fadl al-Jaadi, kujiunga na mwito huu wa gavana wa Aden, Aidarous al-Zubaidi, wa kuundwa kwa “umbile la eneo la kusini” (16/9/2016). Vile vile, rafikiye, Ali Nasser Mohammed, ambaye wakati mwengine anaunga mkono kujitenga na wakati mwengine anataka serikali moja nchini Yemen lakini kwa masharti ayaonayo yeye! Alipoulizwa kuhusu suluhisho nchini Yemen 4/10/2017 (yaani, kabla ya mashambulizi ya Ali Saleh dhidi ya Mahouthi mwishoni mwa mwaka wa 2017), alisema: “Kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na maafikiano, kuondolewa kwa chembe kuu zinazo sababisha vita pande zote mbili “Mahouthi na serikali ya Hadi” katika vyeo vyovyote rasmi wakati wa kipindi cha mpito na kuondolewa kwa silaha kwa vyama na pande zote na kukabidhiwa Wizara ya Ulinzi kwa kuwa Yemen inahitaji raisi mmoja, serikali moja, waziri mmoja wa ulinzi na kuamua kwenda katika uchaguzi katika hatua ya mbeleni. (Chanzo: Al-Ahram Al-Arabi 4/10/2017). Ni Dhahiri kutokana na haya kuwa Waingereza wamefaulu kupitia Imarati kufikia kiwango cha ushawishi kwa watu na mirengo yao, ambao hawakuichukulia kwa nguvu fikra ya kujitenga ambayo hawatajiondoa kutokana nayo kwa kuwa imetokamana na Harakati ya eneo la Kusini, bali kulingana na dhurufu zinazo wazunguka.

5- Mrengo wa Hassan Baoum kimsingi ulikuwa ni mrengo wa kifikra wa kisiasa wa kujitenga. Waingereza walitambua kuwa masuluhisho yoyote ya kuridhisha, kuvutia au kutawala sio muwafaka, kwa hivyo wakajaribu kumzingira nchini Oman kwa kifungo cha nyumbani kwa staili ya kimatata, pasi na uamuzi rasmi, na alikuwa ashaazimia kwao kwa sababu ulikuwa ukijionesha kutoegemea upande wowote, kana kwamba hakujua kuwa unakwenda sambamba na Waingereza kwa mujibu was dori ulioagizwa kwayo! Kwa hivyo, kupitia vibaraka wake nchini Oman, misumari ilikazanishwa juu ya Hassan Baoum na alikuwa chini ya kifungo cha nyumbani katika mji wa Salalah kwa muda mrefu. Kwa kukosekana huku kwa mtu kinara wa Amerika katika Harakati ya eneo la Kusini, makundi tiifu kwa Amerika katika Harakati hiyo yamedhoofika kwa kiasi fulani. Hivyo basi, Waingereza walichukua fursa ya kupitia Imarati na kuangazia juhudi za kuunda harakati sambamba eneo la kusini ili kuupiku mrengo wa Baoum eneo la Kusini, na kuzima kiu yao kupitia kwa Aidarous al-Zubaidi, ambaye ni kiongozi maarufu katika Harakati ya eneo la Kusini, na mwanzilishi wa Harakati ya kujitenga na kujiamulia wenyewe “HATAM” mnamo 1996. Na kwa ukaribu wake na kundi la Waingereza, aliteuliwa na Raisi Hadi kuwa gavana wa Aden mnamo 7/12/2015, miezi michache baada ya kuanzishwa kwa mashambulizi ya Saudi (Machi 2015). Hii ilikuwa ni ishara yenye nguvu kwa ajili ya kujenga Imani ya vibaraka wa Uingereza kwake yeye. Aidarous al-Zubaidi amezungukwa na mazingira mazito eneo la Aden na alikuwa ni gavana mwenye mafanikio wa mji huo. Aliregesha umeme mjini humo na kuyafurusha magenge ya kisilaha. Alipigana na Mahouthi na kupinga mapendekezo ya mjumbe wa Amerika, Ould Sheikh. Yote hayo ni kwa kupitia usaidizi wa moja kwa moja wa kiraia na wa kifedha na kijeshi kutoka kwa Imarati. Kwa kuwa alikuwa mpiganaji katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo 1994 na kiongozi anaye husika na harakati ya kujitenga tangu mwanzoni mwa kuundwa kwake na kufukuzwa na utawala wa serikali ya Ali Saleh jijini Sana’a tangu kuweko kwake mafichoni nchini Djibouti mnamo 1994, na kwa kuwa ni mtoto wa eneo la Dhale, kitovu cha harakati ya eneo la Kusini na nukta ya amali zake, ikiongezewa na mafanikio yake kama gavana wa Aden na vita vyake dhidi ya Mahouthi, umaarufu wake umeongezeka eneo la Kusini kama mtu mwenye usemi wa kisiasa anaye shindana na uongozi wa jadi wa Hassan Baoum katika Harakati ya eneo la Kusini. Kijeshi, Aidarous al-Zubaidi anamtegemea Hani Ben Breik, mwanzilishi wa Ukanda wa eneo la Kusini, anaye sifiwa pakubwa kuwa mtu wa Imarati eneo la Kusini. Hani Ben Breik, aliye jitokeza katika uwanja wa Yemen kama mpiganaji anaye kabiliana na Mahouthi, na kisha katika mandhari ya kisiasa kama waziri aliye lazimishwa na Imarati kwa nguvu kwa sababu ya ushawishi aliopata kutokana na kusaidiwa kwa ukarimu kutoka Abu Dhabi, na kuanzisha ule unaoitwa “Ukanda wa Usalama”, wanamgambo wanasaidiwa hadharani na Imarati eneo la Kusini mwa Yemen. (Chanzo: Sasa Post, 2/11/2017). Kwa hivyo, al-Zubaidi na Breik walikuwa na maslahi eneo la Kusini, lakini kwa sababu walikuwa katika serikali ya Hadi na utiifu wao kwa Uingereza kufichuka hii haitawapatia umaarufu katika kulingania Harakati ya eneo la Kusini, kwa hivyo hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwaondoa kutoka katika serikali ya Hadi katika njia itakayo onesha, hususan al-Zubaidi, sintofahamu nzito na kambi ya Hadi na kisha watu wa eneo la Kusini watakusanyika nyuma yao kuunda harakati mpya ya Hirak, na ndivyo ilivyo kuwa.        

6- Mnamo Aprili 27, 2017, Raisi wa Yemen alitoa amri ya kutimuliwa kwa Aidarous al-Zubaidi, Gavana wa Aden na Hani Ben Breik, Waziri wa Serikali huku Hani akiagizwa kufanyiwa uchunguzi. Maelfu ya Wayemeni walishiriki katika maandamano katika mji ulioko kusini wa Aden, wakipinga maamuzi ya Hadi, na makundi katika Harakati ya eneo la Kusini yaliotangazwa katika “Tangazo la Aden” mnamo 4 Mei 2017 uamuzi wao wa kumteua Aidarous al-Zubaidi kuunda na kuongoza kundi kusimamia na kuwakilisha Kusini ili kupata malengo na matamanio yake, kuongezea pia na kumpa mamlaka kamili kuchukua hatua zozote muhimu za kutekeleza vipengee vya tangazo hilo. Wiki moja baada ya Harakati ya eneo la Kusini kumpa kazi hiyo al-Zubaidi ya kuunda uongozi wa kisiasa na kusimamia na kuwakilisha Kusini, al-Zubaidi alitangaza uraisi wake kwa Baraza la Mpito eneo la Kusini katika mji wa Aden, mnamo 11 Mei 2017, na kumteua Ben Breik kama naibu wake ikiongezewa na uanachama wa watu 26. 

Kutokana na mlango wa kushindana na Baoum, alitoa hotuba huku akiiweka iliyokuwa bendera ya Kusini ubavuni mwake (huku akiwa na bendera ya iliyokuwa dola ya Yemen Kusini, al-Zubaidi alisema, katika hotuba iliyo peperusha na runinga mnamo Alhamisi kuwa chini ya “tangazo la kihistoria la Aden”, “uongozi mkuu wa kisiasa wa eneo la Kusini unaoitwa Uraisi wa Baraza la Mpito la eneo la Kusini utakamilisha mipangilio yote ya kubuni asasi za Baraza la Mpito la eneo la Kusini, na usimamizi na uwakilishaji wa eneo la Kusini kindani na kinje” (Chanzo: Shirika la habari la CNN Arabic 11/5/2017).

Hivyo basi, al-Zubaidi na Ben Breik na nyuma yao Imarati (Muingereza) wamekuwa ndio nguvu za kuundwa kwa uongozi eneo zima la Kusini. Magavana wa mikoa wanateuliwa na Raisi wa Yemen; yaani, wao ndio vibaraka wa duara la Uingereza nchini Yemen, na waliosalia katika viongozi wa Baraza la Mpito ni wafuasi wake. Aliweza hata kuwajumuisha baadhi ya watu wa mrengo wa Baoum, mithili ya Ali al-Saadi na Nasser al-Khubji, hata kwa kipindi fulani, hivyo ikiwa ukweli utadhihiri, ima wataondoka au kufurushwa, au yaweza kutumiwa kama njia ya kuwatenga. Hivyo basi, Nasser Al-Khubji chini ya mpango wa “kumtenga” Baoum kutoka katika mandhari amekuwa mfuasi wa mwanzo wa al-Zubaidi!

Huku baraza la mpito linalo ongozwa na Aidarous al-Zubaidi likiwa na udhibiti nusu mjini Aden, umiliki wa nguvu wastani za kijeshi zikiongozwa na Ben Breik katika mikoa mengine ya kusini na hata mjini Marib, mkusanyiko wa magavana wa mikoa pambizoni mwa uongozi wa Aidarous al-Zubaidi, usaidizi kwa waliokuwa wafuasi wa ujamaa wa “Dola ya Kusini”, kama vile Ali Salem al-Beidh, aliye tangaza mapema uungaji mkono wake kwa al-Zubaidi, usaidizi wa Tariq al-Fadhli na staili yake ya Kiislamu iliyo ongezea uzito katika msimamo wa kabila lake mjini Abyan, msimamo wa kifedha, kisiasa na kijeshi wa Imarati katika upande wake, kwa yote haya, Uingereza ilimakinisha kadhia ya Harakati ya eneo la Kusini pambizoni mwa kibaraka wake Aidarous al-Zubaidi kwa kiwango kikubwa. Ikiwa dhurufu hizi za kisiasa zitaendelea kuwepo kama zilivyo, hususan uwepo wa uzito wa Imarati katika eneo la Kusini, udhibiti huu utaendelea kuwepo.     

7- Amerika imetambua kuchelewa kwake, na kuonyesha kuchukizwa kwake, na kile kinacho ashiria kutoridhika kwa Amerika kwa kuundwa Baraza la Mpito ni upinzani wake kwa mjumbe wake wa kimataifa Ould Cheikh kwa Baraza hilo (mjumbe wa UM nchini Yemen, Ismail Ould Cheikh, aliye tumwa kumtimua gavana wa Aden, Aidarous al-Zubaidi, ujumbe “unaotishia wazi” juu ya historia ya tangazo lake la kuundwa kwa baraza la mpito kwa ajili ya kulitenga eneo la Kusini, kwa mujibu wa duru ya kuaminika. Al-Mashad al-Yemen ilinukuu duru ya kuaminika ikisema kuwa Ould Cheikh alikutana na al-Zubaidi na kutuma ujumbe wazi wa vitisho endapo atasisitiza kulishikilia baraza hilo alilolitangaza, ambalo limepingwa na Raisi wa Yemen, Baraza la Ushirikiano wa Ghuba, kundi la Mahouthi na wengine wengi ndani ya Harakati ya eneo la Kusini. Endapo al-Zubaidi atasisitiza, Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama litamjumuisha miongoni mwa wale wanaozuia mpangilio wa amani nchini Yemen na utekelezaji wa azimio nambari 2216, chini ya sura ya VII, na atachukuliwa kama Mahouthi na Saleh kama “waasi” … (Chanzo: Russia Today 14/5/2017).

Inaonekana kuwa Amerika imerekebisha jambo hili, kwa hivyo ikaisisitiza Oman kumuachilia huru Baoum. Baada ya kuachiliwa kwake, Hassan Baoum alichukua hatua kali dhidi ya Baraza la Mpito, akisaidiwa na Imarati katika mzozo mkubwa uliojitokeza wa Kiamerika nchini Yemen, na inaoneka kuwa harakati zake zilikuwa na usaidizi wazi wa Saudia. Hivyo basi, chini ya macho na uoni wao Bunge la kwanza la Baraza la Harakati ya Mapinduzi, likiongozwa na yeye, lilifanywa mjini Aden 17/8/2017, wafuasi wake mia sita wakishiriki, wakiituhumu Imarati kwa kuikalia Yemen Kusini. Taarifa ya kongamano hilo alisema: “Tunapinga wazi unyanyasaji wa watu wetu wa kusini na uenezaji urongo na kuwaathiri kihisia ili kuvutia uungaji mkono na kisha kupindua matakwa hayo ya watu wa Kusini … Tunathibitisha kuwa kiongozi Hassan Baoum, Raisi wa Baraza Kuu la harakati ya mapinduzi, ndiye kiongozi na nembo ya eneo la Kusini ambayo tunajivunia nayo na kujifakhiri kwayo … Yanayo jiri leo eneo la Kusini ya ushindani wa kifujo baina ya majeshi ya nje, kama Imarati, ambayo imekuwa ni nchi inayo nyakua bandari za eneo la kusini na bidhaa zake, na kudhibiti hatma ya watu wetu na mielekeo yao na kisha inakuja kuwapa kipote cha wafuasi wake kiasi kidogo cha makombo.” (Chanzo: Adan Al-Ghad 17/8/2017). Yaani, kundi la Baoum linaonesha uadui wazi kwa Imarati na kuitaka kuondoka nchini Yemen, na kongamano la Baoum kuliita kundi la al-Zubaidi “wafuasi wa Imarati, inayowapatia kiasi kidogo cha makombo”.         

Ni wakati huo ambapo kongamano la pili la Baoum, lililo fanywa mnamo 11/112017, na ilisemwa katika tangazo la mwisho la kongamano hilo la Baoum la pili la kila mwaka la “Baraza la Harakati ya Mapinduzi”, lililofanywa mjini Aden na Al-Arabi Al-Jadeed kupata nakala yake, “Tunatoa wito kwa ule unaoitwa Muungano wa dola za Kiarabu kuweko na mazungumzo ya moja kwa moja na Baraza Kuu la Harakati hiyo baada ya kuondoa majeshi yake yote kutoka eneo letu, na tunathibitisha umakinifu wetu katika mafungamano ya kijamii na ya kidini baina yetu. Baraza hilo linaloongozwa na Baoum liliutaja muungano huo kama “dola vamizi” na kuongeza, “Tunathibitisha haki yetu kamilifu ya kukabiliana na uvamizi kwa njia na mbinu zote za halali na kwa wakati na mahali muwafaka kulingana na maslahi yetu ya kitaifa”. Taarifa hii ilisisitiza kuwa majadiliano au suluhisho yoyote itakayo iweka kando kadhia ya eneo la kusini na wawakilishi wake halali hayatafaulu kwa sababu wawakilishi hawa halali ndio walioiongoza harakati hii tangu siku yake ya mwanzo na sio wale walioingizwa kibahati, kwa pesa au kufinyangwa na uvamizi wa kigeni” … (Chanzo Al-Arabi Al-Jadeed 11/11/2017). Taarifa hii, ingawa ilizungumzia kuhusu muungano wa Waarabu, kimsingi ilielekezwa dhidi ya Imarati kwa sababu kongamano hilo lilifanywa chini ya ulinzi wa Saudia!    

8- Kwa kutamatisha: baada ya Ali Salem Al-Beidh na Ali Nasser Mohammed kushindwa mnamo 1994 na Ali Saleh kunyakua rasilimali za Yemen Kusini, kutelekezwa kwa watu wa Kusini na kuteswa kwa wanajeshi wengi wa eneo la Kusini … yote haya yame sababisha kuzuka kwa harakati nyingi za upinzani kuanzia wakati huo, zenye kuonekana zaidi ni harakati tatu:

- Harakati ya eneo la Kusini, mrengo wa Ali Salem Al-Beidh usio aminika: wakati mwengine ukiwa na Amerika na vibaraka wake, na wakati mwengine ukiafikiana na Uingereza na vibaraka wake.

-  Harakati ya eneo la Kusini, mrengo wa Hassan Baoum unaosaidiwa na Amerika na vibaraka wake, hususan Iran.

- Harakati ya eneo la Kusini, mrengo wa Al-Zubaidi unaosaidiwa na Uingereza na vibaraka wake, hususan Imarati.

- Kama tulivyo taja juu, tumeangazia misimamo yao muhimu juu ya kadhia za sasa za Yemen, na inatia uchungu kuwa kadhia zetu zinaingiliwa na wakoloni makafiri kwa kutumia ala za kutu kutoka kwa wenzetu! Hivyo basi, damu yetu inamwagwa nchini Yemen na kwengineko kwa manufaa ya makafiri kwa kutumia ala za ndani ya eneo. Na watu hawa wamesahau au kujifanya kusahau mambo ambayo lau watayatafakari watalia machozi ya damu kwa yale waliyo yafanya:

Allah, Mwenye nguvu, Mwenye uwezo wa juu, amewaharamisha Waislamu kutokana na kuwategemea makafiri:

وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنْصَرُونَ ﴿

“Na wala musiwategemee wale waliodhulumu ukakuguseni Moto. Na wala nyinyi hamuna mlinzi badala ya Allah, kisha wala hamutanusuriwa.” [Hud: 113].

Na Mtume wa Allah (saw) asema kuhusu kumwaga damu pasi na haki kuwa ni jambo kubwa kwa Allah kuliko kuangamia dunia nzima. Tirmidhi amesimulia kutoka kwa Abdullah bin Amr kwamba Mtume (saw) amesema: «لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عَلَى اللَّهِ مِنْ قَتْلِ رَجُلٍ مُسْلِمٍ» “Kuangamia dunia nzima ni sahali mbele ya Allah kuliko kumuua Muislamu mmoja.”

Na Ibn Assaker ameisimulia katika Muajam yake na kusema: Hii ni hadith Hasan, sasa vipi basi itamwagwa kwa manufaa ya wakoloni makafiri? Hakika, ni kosa juu ya kosa;

 ﴾سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ ﴿

“Itawafika wale walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Allah kwa vile vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Al-A’nam: 124]

Lakini, Yemen, iliyosifiwa na Mtume wa Allah (saw) kuwa biladi ya Iman na hikma haikosi wanaume wenye ikhlasi, ukweli na uaminifu ambao watasimama dhidi ya wale wanao watii wakoloni makafiri. Watairudisha Yemen, kwa idhini ya Allah, kuwa Dar Islam, chini ya kivuli cha bendera ya Uislamu, chini ya Khilafah Rashida itakayo regesha hadhi yake kuwa kama Mtume (saw) alivyo isifu katika hadith iliyo simuliwa na Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Abu Hurayrah (ra) kutoka kwa Mtume (saw): «أَتَاكُمْ أَهْلُ الْيَمَنِ هُمْ أَرَقُّ أَفْئِدَةً وَأَلْيَنُ قُلُوبًا الْإِيمَانُ يَمَانٍ وَالْحِكْمَةُ يَمَانِيَةٌ»“ Watu wa Yemen wamewajia na ni watulivu na wepesi mioyoni. Iman ni Yemen na Busara ni Yemen…”

8 Jumada II 1439 H

Jumamosi, 24/02/2018 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 21:21

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu