Jumamosi, 19 Dhu al-Qi'dah 1446 | 2025/05/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Swali

Mazungumzo kati ya Marekani na Iran

(Imetafsiriwa)

Swali:

Ufalme wa Oman, ambao unaendesha upatanishi katika mazungumzo ya Marekani na Iran, ulitangaza mnamo Alhamisi (kuakhirishwa kwa raundi ya nne ya mazungumzo ambayo yalipangwa kufanyika mnamo Jumamosi katika mji mkuu wa Italia, Roma, "kwa sababu za kiufundi," bila kutaja tarehe mpya. Al-Sharq, 1/5/2025). Mazungumzo ya awali yasiyo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran yalianza mnamo tarehe 12 Aprili 2025 katika mji mkuu wa Oman, Muscat, kwa upatanishi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr Al-Busaidi. Raundi ya pili ilifanyika mnamo tarehe 19 Aprili 2025 katika ubalozi wa Oman jijini Roma, pia kwa upatanishi wa Waziri huyo. Raundi ya tatu ilifanyika mnamo tarehe 26 Aprili 2025 katika ufalme wa Oman, chini ya upatanishi huo huo wa Oman. Swali ni: je, kwa nini Trump sasa anataka kurudia kusaini mkataba wa nyuklia na Iran, ilhali yeye binafsi alijiondoa kwa upande mmoja mwaka 2018 kutoka mkataba uliotiwa saini mnamo tarehe 14 Julai 2015? Na kwa nini raundi ya nne imeakhirishwa? Je, maana ya “sababu za kiufundi” ni nini? Na je, kuakhirishwa huku kuna maanisha kuwa mazungumzo yamevunjika?

Jibu:

Lazima kwanza tuangalie mazingira yaliyokuwepo mwaka 2015 wakati Marekani ilipotia saini mkataba wa nyuklia na Iran, kisha tuangalie muktadha wa kujiondoa kwa Trump kutoka mkataba huo mwaka 2018 na hali ya wakati huo, halafu tusimame juu ya mabadiliko ya karibuni kuhusu mazungumzo kati ya Marekani na Iran:

1. Sababu zilizolifanya Marekani kusaini mkataba wa nyuklia na Iran mwaka 2015: Tulisema katika jibu la swali la tarehe 22 Julai 2015 kuhusu utiaji saini wa Marekani katika mkataba huo: (“… Rais wa Marekani alisimamia mazungumzo hayo kwa karibu sana, akihusisha Waziri wake wa Mambo ya Nje kwa wiki tatu mfululizo, bila kuhesabu mawasiliano ya awali, jambo linaloonesha umuhimu mkubwa wa mkataba huu kwa Marekani, kwa maslahi yake na ya utawala wa Obama. Mkataba huu uliifunga Iran na kuizuia kutengeneza silaha za nyuklia... Maelezo ya viongozi wa Marekani kuhusu umuhimu wa dori ya kimkakati ya Iran katika eneo hili, pamoja na kauli za viongozi wa Iran wakionyesha ushirikiano wao na Marekani nchini Iraq na Afghanistan pamoja na nia yao ya kufanya kazi pamoja nayo katika kupambana na ugaidi na misimamo mikali, na tunaona kuhusiana na makubaliano fiche kwa yale ambayo Iran na chama chake (nchini Lebanon) inafanya nchini Syria, tunaona kwamba yote haya yanaonesha kuwa Marekani ililenga kupitia mkataba huu kurahisisha na kuwepesisha mambo na Iran kupitia kuondoa vikwazo na kumakinisha uhusiano wa wazi nayo, ili iendelee kucheza dori ambayo itaifanya rahisi kazi ya Marekani, kukazanisha mizigo yake na kufinika michezo yake kwa watu dola na watu katika eneo hilo. Hivyo basi, Iran itatekeleza sera ya Marekani kivitendo kama ilivyo nchini Iraq, Syria na Yemen lakini badala ya hili kutekelezwa nyuma ya pazia yenye kuziba macho kama ilivyokuwa (kabla ya makubaliano), sasa litafanyika nyuma ya pazia inayoonyesha au bila ya pazia yoyote ...”).

Kwa hivyo, Obama alihitimisha mkataba wa nyuklia na Iran mnamo tarehe 14/7/2015 kwa ajili ya kuimarisha dori ya Iran nchini Syria.

2. Sababu zilizopelekea utawala wa Trump kuufutilia mbali mkataba huo wa nyuklia na Iran mwaka 2018:

a. Marekani ilikuwa imeanza kuwaingiza washirika wengine kama Saudi Arabia na Uturuki katika mgogoro wa Syria. Uturuki ilianzisha operesheni ya kijeshi “Euphrates Shield” mwaka 2016 na “Olive Branch” Machi 2018. Hii ni pamoja na dori ya Saudi Arabia ya kikanda. Matokeo yake hakukuwepo tena na haja ya Iran kucheza dori kuu nchini Syria, na ilibidi kupunguzwa. Hivi ndivyo haswa Trump alivyofanya; alipunguza dori ya Iran katika eneo, kuigeuza kutoka kuwa ni mchezaji mkuu hadi dori ya pili au ya ziada.

b. Nchi za Ulaya zilikuwa sehemu ya makubaliano hayo ya nyuklia ya 2015 na zilifaidika sana nao. Trump hakutaka Ulaya ivune mafanikio yaliyotokana na makubaliano yaliotiwa saini wakati utawala wa Obama, hivyo aliufutilia mbali.

Kwa hivyo, Trump alitangaza kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia na Iran, kwani ilikuwa ni kwa maslahi ya Amerika kujiondoa katika makubaliano hayo ili kujiandaa kwa masharti mapya ambayo yatapunguza dori ya Iran katika eneo.

3. Sababu zinazomfanya Trump kurudi kwenye makubaliano ya nyuklia mwaka 2025 aliyoyafutilia mbali mwaka 2018:

Kwa kuzingatia matukio yaliyofuatia kuapishwa kwa Trump mnamo tarehe 20/1/2025, motisha zilizoifanya Marekani kuregea kwenye makubaliano ya nyuklia zinadhihirika:

a. Ni wazi kwamba utawala wa Trump ndio ulioanzisha kuregelea mazungumzo ya Nyuklia na Iran. Trump alituma barua kwa Iran kupitia Oman mnamo tarehe 7 Machi, akieleza hamu ya wazi ya kuregea mezani kwa mazungumzo ili kufikia makubaliano mapya. (Rais wa Marekani Donald Trump alisema katika mahojiano na Mtandao wa Biashara wa Fox kwamba alituma barua kwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei mnamo siku ya Alhamisi, Machi 6, akielezea upendeleo wake kwa mazungumzo ya makubaliano na Tehran. Trump aliongeza katika mahojiano yake, ambayo yamepangwa kurushwa siku moja baada ya kesho, Jumapili: “Chaguo jingine ni kwamba hatua lazima ichukuliwe, kwa sababu Iran lazima isipate silaha ya nyuklia” kuhusu maandishi ya barua aliyoitumia Khamenei, Trump alisema: “natumai mtajadiliana, kwa sababu hilo lingekuwa bora zaidi kwa Iran.”... Iran International, 7/3/2025.).

b. Mnamo  2018, Trump alibatilisha makubaliano ya nyuklia kwa sababu mafanikio makubwa kutokana na makubaliano yaliyotiwa saini mwaka 2015 kati ya wanachama watano wa kudumu na Ujerumani yalikwenda kwa Wazungu. Kwa hiyo, Trump aliziondoa nchi za Ulaya katika mazungumzo ya nyuklia na Iran, tofauti na ilivyotokea mwaka 2015, na hakushauriana nao au kuwajulisha juu ya mazungumzo yaliyofanyika Oman, ili kuzuia jitihada za Ulaya kufanya mazungumzo ya nyuklia na Iran. (Wanadiplomasia wa Ulaya waliiambia Reuters kwamba wanatafuta kufanya mkutano mpya na Iran, lakini jitihada hizo zinaonekana kukwama wakati Tehran ilipoanza mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kuhusu mpango wake wa nyuklia na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump mapema mwezi huu. Marekani haikujulisha nchi za Ulaya juu ya mazungumzo ya nyuklia katika Ufalme wa Oman kabla ya Trump kutangaza ... Asharq, 24/4/2025) hata chaguo la Italia, inayoongozwa na Waziri Mkuu wa mrengo wa kulia, Melonia, aliyepokea uungwaji mkono kutoka kwa utawala wa Trump, kwani mahali patakapofanyika raundi ya pili ni ujumbe unaoelekezwa kwa nchi za Ulaya ambazo zimeingia katika mzozo na upinzani nazo, haswa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, kwa kisingizio cha NATO.

c. Marekani inataka kuelekeza umakini wake wote na rasilimali zake zote kukabiliana na ushindani wa kilimwengu na China. kwa hiyo, inatafuta kuondoa vipengee vyovyote vinavyoleta tatizo kwake na kupotoa nguvu yake. Majadiliano yanayoendelea na Urusi yanaweza kuelezewa kwa mantiki hiyo hiyo: wanalenga kuvutia Urusi kwenye meza ya mazungumzo kupitia mgogoro wa Ukraine, na hivyo kuitenganisha na China, kwa lengo la kudhoofisha mhimili wa Sino-Urusi. Kwa hivyo, Trump anaifanya China kuwa kipaumbele cha kimkakati.

d. Tamaa ya umbile la Kiyahudi kuishambulia Iran kwa kisingizio cha kuizuia kupata silaha za nyuklia. Kama tunavyojua, umbile la Kiyahudi lilianzisha shambulizi dhidi ya Iran mnamo Oktoba 2024. Iran ilijibu kwa mashambulizi ya makombora ili kuonyesha nguvu zake, baada ya kufahamisha Marekani na umbile la Kiyahudi mapema. Sasa, Marekani haitaki kukengeushwa na mashambulizi hayo huku ikilenga China. Kwa hiyo, inataka kuhitimisha makubaliano ya nyuklia na Iran, ambayo yatahakikisha usalama wa umbile la Kiyahudi na kuondoa kisingizio cha mashambulizi kutoka kwao. Kwa hatua hii, baada ya kuhitimisha makubaliano ya nyuklia na Iran, Trump, muungaji mkono zaidi wa umbile la Kiyahudi katika Ikulu ya White House, ataondoa kisingizio cha mzozo kutoka kwa umbile la Kiyahudi na ataondoa hoja yao. Wakati huo huo, ataweka maslahi ya kiuchumi ya Marekani na kukabiliana na China mbele ya vipaumbele vyake, na kumwezesha kuzingatia kabisa China, bila kitu chochote kinachosumbua mwelekeo wake au kuzuiwa na kikwazo chochote.

Kwa hivyo, Trump alianza mazungumzo haya na Iran ili kuhitimisha makubaliano ambayo yangepunguza uwezo wa nyuklia wa Iran kwa kutengwa na nchi za Ulaya.

4- Kuhusu kwa nini raundi ya nne iliakhirishwa, ni kwa sababu za vifaa, kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari. Maana ya neno lojistiki, kama ilivyoelezwa katika Wikipedia, ni: (“Sanaa ya ugavi na utoaji.” Logistics, au kile kinachojulikana kwa Kiarabu kama sanaa ya vifaa, ni sanaa na sayansi ya kudhibiti mtiririko wa bidhaa, nishati, na habari... ), kana kwamba nia ilikuwa kupanga anga na kutuliza hali baada ya Amerika kuweka vikwazo kwa kushirikiana na mazungumzo yanayoendelea ya Amerika na Iran. Afisa wa Iran aliiambia Reuters [(kwamba mazungumzo ya Iran na Marekani yatafanyika katika tarehe tofauti kulingana na tabia ya Marekani, akibainisha kuwa vikwazo vya Washington kwa Tehran havisaidii mchakato wa kidiplomasia unaotaka kutatua mzozo wa nyuklia). Haya yanajiri baada ya Washington kuweka vikwazo vipya kwa taasisi inayozituhumu kuhusika na biashara haramu ya mafuta ya Iran na kemikali za petroli. Marekani (ilikuwa imeweka vikwazo siku ya Jumatano kwa vyombo vilivyovituhumu kuhusika katika biashara haramu ya mafuta ya Iran na kemikali za petroli, kama sehemu ya juhudi za Washington za kuzidisha shinikizo kwa Iran) Asharq, 1/5/2025]. Vikwazo hivi vilikuja wakati raundi za mazungumzo zilikuwa zikifanyika kwa umakini, kama ilivyoelezwa. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghaei, alisema: (Tehran itaendelea kushiriki kwa umakini na kwa uthabiti katika mazungumzo yenye lengo la kupata matokeo na Marekani. Asharq, 1/5/2025).

Kwa hivyo, haiwezekani kwamba kuakhirishwa huku ni kukatisha mazungumzo kati ya pande hizo mbili, lakini badala yake kucheleweshwa kwa wakati wa kutuliza hali kutokana na vikwazo vya Amerika wakati wa mazungumzo yanayoendelea.

5- Inashangaza kwamba watawala wa nchi za Kiislamu wanakubaliana na uingiliaji kati wa Marekani katika kubainisha nguvu, silaha, na tasnia ya Waislamu! Watawala hawa hawatambui kwamba maandalizi ya nguvu katika Uislamu ni kuwashinda, kuwaogopesha na kuwatia hofu maadui. Adui akituamulia, kwa undani, ni kushindwa kwetu, hata kabla ya tarehe yake iliyopangwa! Je, Iran inawezaje kuruhusu Marekani kuingilia kati nguvu zake, makombora yake na silaha zake za nyuklia, wakati ambapo Marekani inajaza hazina yake ya silaha za nyuklia na hata kuzipeleka miongo kadhaa iliyopita huko Hiroshima na Nagasaki?! Marekani inatangaza hadharani kwamba haitaruhusu Iran kumiliki silaha za nyuklia. Nini Iran na watawala wengine wa Waislamu wanapaswa kuwaambia Marekani kwa sauti kubwa: Angamizeni silaha zenu za nyuklia kabla ya kuwataka wengine wasizimiliki... na haribuni makombora yenu kabla ya kuwataka wengine wayaharibu makombora yao... Ama maadui wanaomiliki silaha nzito na kuwataka Waislamu wasizimiliki, hiyo ni kauli iliyozama katika ukatili, kiburi, na dharau kwa wengine, laiti wangekuwa na mantiki. Mwenyezi Mungu (swt) alibainisha hayo katika Kitabu chake, kwa kauli yake:

[وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ وَمِنْ رِبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِنْ دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ اللهُ يَعْلَمُهُمْ وَمَا تُنْفِقُوا مِنْ شَيْءٍ فِي سَبِيلِ اللهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنْتُمْ لَا تُظْلَمُونَ]

“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa.” [Al-Anfal: 60]

Katika utangulizi wa Katiba, uk. 256, [Ibara ya 69 inasema: (Ni wajibu kulipatia Jeshi silaha, vifaa na zana, pamoja na mahitaji yote, ambayo yanaliwezesha kutekeleza kazi yake kama Jeshi la Kiislamu). Kauli yake (Subhaanahu wa Ta’ala) [تُرْهِبُونَ] ndio sababu ya kisheria (Illah) ya kujitayarisha.” Matayarisho hayatakamilika isipokuwa tu kwamba sababu ya kuja kwa sheria hii imefikiwa, ambayo inawatia hofu maadui na wanafiki, kwa hiyo, ni wajibu kutoa silaha na zana zote kwa ajili ya Jeshi ili kuhakikisha kwamba kwa vitisho vyake kunatokezwa na utisho mkubwa wa Jeshi lake na kulitekeleza jambo hilo ambalo ni Jihad ya kufikisha ulinganizi wa Uislamu…].

Yote haya yanaashiria kwamba Waislamu lazima wafanye kila juhudi kuhakikisha nguvu zao ni bora kuliko za adui, na hivyo kuwatia hofu katika nyoyo zao. Ili kufikia hili, nguvu zetu lazima ziwe chanzo cha wasiwasi kwa adui, kuwashughulisha na kuwatia hofu. Yote haya hayaendani na kuingia kwenye mazungumzo na adui, ambapo silaha zetu ni chache na tunazuiwa kudhibiti nguvu zetu ili kuwatisha na kuwatia hofu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) amuwezeshe kiongozi Hizb ut Tahrir, ambaye hawadanganyi watu wake, asimamishe dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida, mapema zaidi. Haya yatawaogopesha maadui kama yalivyofanya kabla, na kueneza kheri duniani kote, na kurudisha njama za makafiri juu yao:

﴿وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

4 Dhul-Qi'dah 1446 H

2/5/2025 M

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Jibu la Swali: Dola ya Kina (Deep State)

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu