Jumamosi, 19 Jumada al-awwal 1445 | 2023/12/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Enyi Waislamu! Demokrasia Tata Haiafikiani na Uislamu wenu, Kwa hivyo Msishiriki katika Matambiko Yake Yasiyo na Maana!
(Imetafsiriwa)

Uchaguzi wa ubunge umeitishwa nchini Denmark, na hii ina maana kwamba vyama mbalimbali vya kisiasa na baadhi ya wagombea watajaribu kujishindia kura za baadhi ya Waislamu na kuwasihi kushiriki katika uchaguzi huo.

Katika wakati ambapo shinikizo dhidi ya Waislamu linazidi, mchanganyiko wa hofu na kutoelewana unaweza kupelekea baadhi ya watu kupiga kura katika uchaguzi huo, wakiwa na matumaini ya uongo kwamba kushiriki kwao kutaboresha hali za Waislamu, au kuzuia hali kuwa mbaya zaidi... Hivyo basi, tumeona ni muhimu kufafanua mambo yafuatayo:

1. Demokrasia, kama fikra na mfumo wa serikali, kimsingi haiafikiani na Uislamu. Demokrasia kimsingi imejengwa juu ya wazo la kutenganisha dini na maisha, na wazo hili linasema kwamba mwanadamu ndiye anayeamua lililo sawa na lililo baya, na sio Muumba ... Kwa hivyo, sio sahihi kutabanni demokrasia na kuifanya kuwa muundo wa jamii, wala kuiruhusu iwe marejeo kwa Waislamu.

2. Kwa sababu hiyo hiyo, kuwachagua wagombea au vyama kwa ubunge katika mfumo wa kisekula kimsingi ni kinyume na imani yetu. Kumpigia kura mgombea wa chama cha kisekula kunachukuliwa kuwa ni kuidhinisha utungaji kanuni na sheria isiyokuwa ile iliyoteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni kitendo ambacho kimeharamishwa katika Uislamu. Aidha, ni lazima isisitizwe kuwa ni haramu kuunga mkono chama cha kisekula, kwa sababu kuunga mkono chama cha kisekula kunachukuliwa kuwa ni msaada kwa chama hiki kueneza na kutekeleza mawazo yake yanayogongana na Uislamu, na hili linahusu vyama vyote vya kisiasa vilivyoteuliwa nchini Denmark.

3. Demokrasia kwa hakika ni mfumo wa dhulma ya kila aina inayofanywa na walio wengi dhidi ya Waislamu katika ulimwengu wa Magharibi, hasa barani Ulaya, na sababu ya hali hii ni kwamba tawala hizi zinaona ongezeko la uwepo wa Waislamu na kushikamana kwa Waislamu na kitambulisho chao kuwa ni tishio kwa thaqafa ya mujtamaa zao. Hivyo basi, wanatunga sheria za kibaguzi dhidi ya Uislamu na Waislamu na kuongoza kampeni za uzushi za chuki zinazochochea misimamo mikali ya rangi miongoni mwa raia wao na kuhakikisha wanazitenganisha jamii hizi. Sera hii dhidi ya Uislamu imekuwa sera ya kudumu bila kujali aina ya serikali au vyama vinavyounda serikali. Picha ilionekana wazi katika uchaguzi huu kuliko chaguzi zengine, ni sawa na kuchagua kati ya tauni au kipindupindu, bila kujali vyama vitakavyounda serikali baada ya uchaguzi.

4. Ni upotoshaji na nia fikra finyo kudai kuwa kutoshiriki kwa Waislamu katika chaguzi hizi au kutokuwa na hamu nazo kunachukuliwa kuwa ni hasi au uzembe. Sio sahihi kudunisha ushiriki changamfu wa Waislamu katika jamii hadi suala la kutoa sauti katika chaguzi zisizo na thamani.Tunatakiwa kujihusisha na jamii kwa njia chanya, lakini kwa misingi ya Uislamu ambapo Uislamu umetuonyesha misingi na jinsi ya kufanya vitendo vya kisiasa. Moja ya mafunzo muhimu tunayopata katika wasifu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika kipindi cha da'wah ya Makkah ni namna mahususi ambayo vitendo vya kisiasa vinafanyika, ambavyo vinapambana na kila jambo linalopingana nao na kuwasilisha njia mbadala.

[قُلْ هَـذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللّهِ عَلَى بَصِيرَةٍ أَنَاْ وَمَنِ اتَّبَعَنِي وَسُبْحَانَ اللّه وَمَا أَنَاْ مِنَ الْمُشْرِكِينَ]

“Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.” [Yusuf 12:108]

5. Tupende tusipende, kushiriki katika uchaguzi kunachukuliwa kuwa ni kuupa imani mfumo wa kisekula, na kwamaanisha kukubali mawazo batili yanayotenganisha dini na siasa, jambo ambalo haliruhusiwi kwa Muislamu kulikubali, achilia mbali kufanya kazi kwalo au kuliunga mkono. Ni kwa sababu hii hasa kwamba Waislamu wanashinikizwa kushiriki katika chaguzi kama sehemu ya sera ya ujumuishwaji kisiasa. Suala hili halihusiani tu na kujizuia kufanya yale yaliyo haramishwa, bali ni kuhusu kitambulisho chetu kama Waislamu, na mfumo wowote wa maisha na mtazamo wa maisha ambao tunathibitisha uaminifu wetu kwao.

Enyi Waislamu: Jahazi la demokrasia linakaribia kuzama, uchaguzi mmoja baada ya mwingine umethibitisha kuwa wadau ndio washindi. Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa imani ya Wadenmark kwa wanasiasa wao imefikia viwango vya chini kabisa, na pia imani yao katika mfumo wa kidemokrasia wenyewe. Hali kadhalika katika nchi za Magharibi kwa jumla, wao wanatafuta njia mbadala ya mfumo dhalimu wa kirasilimali. Na nyinyi Waislamu munayo njia hii mbadala! Hivyo basi, si sahihi kwenu kuukubali kwa maneno au kwa vitendo utawala wa kidemokrasia wa kafiri, ambao umefanya udanganyifu kwa wanadamu kwa karne mbili.

Nyinyi kama waungaji mkono wa ulinganizi wa Uislamu, mnaobeba mtazamo wa kweli wa maisha na sheria za Mwenyezi Mungu, mnatakiwa kuulingania Uislamu kwa fikra na mfumo, na kutotambua fikra na mifumo ya kikafiri.

Badala ya kukimbilia vyama vya kisekula na wagombea wao, tunapaswa kufanya kazi pamoja mbali na vyama hivi, kuwahifadhi Waislamu, na kuzingatia misingi ya Uislamu na kujali maslahi ya Waislamu sisi wenyewe. Badala ya kuuamini mfumo wa kisiasa wa kisekula, ni lazima tufanye kazi ya kujenga imani katika mfumo wa Uislamu, na kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa mujtamaa wa Magharibi ambao unateseka sana na mfumo unaoudhibiti na kwa sababu yake migogoro ya kiuchumi, kijamii na kisiasa uwepo wake ni wa daima.

Enyi Waislamu: Ushindi mkubwa katika maisha ya dunia na Akhera uko katika kujisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Utiifu wetu hauamuliwi kamwe na mahali tulipo katika ulimwengu huu. Bali, unapaswa uwe kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Ummah wetu wa Kiislamu.

Njia ambayo ni lazima tuichukue kama Waislamu ni kulinda maadili yetu na kitambulisho chetu, na kusimama dhidi ya sera ovu ya uoanishaji inayotekelezwa na serikali mtawalia. Ni lazima tusimame pamoja kama walinzi wa maadili ya Kiislamu dhidi ya propaganda dhidi ya Uislamu na kuulingania Uislamu ndani ya mujtamia unaotuzunguka. Kama Waislamu, lazima tuzingatie kwamba Uislamu ni muanga unao angaza njia ya kila mtu, hasa wale wanaotafuta maadili halisi na ufumbuzi wa kivitendo.

Sisi katika Hizb ut Tahrir tunawalingania nyote kwa ikhlasi kujiweka mbali na demokrasia ya kisekula inayogongana na dini yenu ya haki, na mufanye kazi nasi kisiasa na kifikra katika kuulingania Uislamu kamili na jumuishi, na kufanya kazi ya kuhifadhi kitambulisho chetu cha Kiislamu, na kushiriki katika kazi ya kuregesha mfumo wa utawala katika Uislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 8-24]

H. 11 Rabi' I 1444
M. : Ijumaa, 07 Oktoba 2022

Hizb-ut-Tahrir
Denmark

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu