بسم الله الرحمن الرحيم
Enyi Waislamu, Ngao ya Frati, Tawi la Mzeituni na Chemchem ya Amani Zote ni Hatua katika Msururu wa Kufufua Muundo wa Utawala!
(Imetafsiriwa)
Aliyoyafanya na anayoyafanya Erdogan ni kutekeleza yale ambayo Amerika inayataka; kuimarisha utawala wa kidhalimu ndani ya Syria kwa kutumia mikono miovu ya kimataifa, kimaeneo na mashinani. Hii ni baada ya kelele za watu na uasi wao uliposhtua utawala na Amerika nyuma yake na washirika wake kutoka Urusi, Iran na Erdogan wa Uturuki na makundi yake na kupanga njama ili kutekeleza mipango ya Amerika ili kuimarisha nidhamu iliyokita ya Kisekula ndani ya mji wa Ash-Sham! Tayari tulitoa Jibu la Swali mnamo 7/12/2016 kuhusu njia za udanganyifu za Erdogan katika Ngao ya Frati na Tawi la Mzeituni ambalo lilifichua uhalisia wa wale waliodanganywa na kuvutiwa na matamshi ya Erdogan wakifikira kuwa anawaunga mkono dhidi ya dhalimu wa Syria, lilisema: (Kuongezea hili ni muendelezo wa kampeni ya Erdogan ya Oparesheni ya Ngao ya Frati na jaribio lake la kuvutia makundi mengi ya kijeshi upande wa Uturuki katika vita vya Al-Bab baada ya Jarablos yote haya ni kwa ajili ya kudhoofisha safu za kweli za Aleppo ambayo yalitegemewa ili kuiondosha na kuiokomboa kutoka katika kizuizi cha kuzungukwa). Na hivyo basi Aleppo ikapotezwa! Makundi hayo yalitakiwa yawe yamejifunza lakini kwa mara nyingine yameumwa tena katika tundu linalomilikiwa na Erdogan! Waliungana naye kwa mara nyingine katika Tawi la Mzeituni na tukatowa Jibu la Swali wakati huo mnamo 24/1/2018, ambalo lilisema: (Hivyo basi Erdogan anarudia hali ya Ngao ya Frati ili kuuwezesha utawala kuingia Idlib. Oparesheni ya Tawi la Mzeituni ikapangwa ili kuuwezesha utawala kuingia Idlib).
Jibu la Swali jengine lilitolewa mnamo 29/07/2018 lilisema: (Ngome ya pili: iliongozwa na Uturuki katika vita vya Ngao ya Frati kaskazini mwa Aleppo mnamo 24/08/2016 na kisha Tawi la Mzeituni mnamo 20/01/2018 ikaifanya kuwa ni rahisi kwa utawala kuingia Aleppo na kusini mwa Idlib. Ni kwa sababu makundi haya yaliamrishwa na Uturuki na kuondoka vitani dhidi ya utawala na kwenda kupigana katika kampeni ya ngao na tawi, Aleppo na Idlib kusini zikapotezwa au zikakaribia kupotezwa!) Hivi sasa makundi yamefanywa wajinga kwa mara ya tatu kwa Oparesheni ya Chemchem ya Amani! Kampeni hii imeufufua utawala na kuuzidishia kufaulu kwake kwa agizo la Trump na uungaji mkono: [(Muandishi na mchanganuzi wa kisiasa wa Uturuki, Javad Gok, alisema kwamba "pasina na uungwaji mkono na Amerika" Uturuki haiwezi kusonga mbele ndani ya mashariki ya Frati… (tamuz-net 6/10/2019)]. White House ilitangaza kwamba [(Majeshi ya Amerika yatajitoa kutoka Syria kaskazini huku Uturuki ikijiandaa kuzindua oparesheni ya kijeshi huko, hii ni baada ya mazungumzo ya simu baina ya Rais wa Amerika Trump na mwenziwe wa Uturuki Erdogan. (CNN Arabic 7/10/2019)]. Akithibitisha maagizo ya Amerika na kutafuta kuiridhisha: [Msemaji wa White House alitangaza mnamo Jumanne, ziara inayotarajiwa ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwenda Amerika mnamo 13 Novemba…(Al-Mashhad Al-Araby, 8/10/2019)]
Ama kuhusu kauli ya Trump kuhusu vikwazo na vitisho [Rais wa Amerika Donald Trump aliiwekea Uturuki vikwazo mnamo Jumatatu na kuitaka kwamba isitishe uvamizi wake wa kijeshi ndani ya Syria kaskazini…(Reuters 15/10/2019)], kauli hizi ni za kudanganya tu na kupotosha kwa sababu inawezekana vipi Trump kumuunga mkono Erdogan na aendelee na kampeni yake kisha amtishie kwa vikwazo na kumuagiza kusitisha kampeni yake? Isipokuwa ni maagizo ya Trump kwa Erdogan yanakaribia kuisha na hivyo basi vikwazo ni njia ya kutokea tu! Hivyo basi Erdogan alitekeleza kampeni yake kwa maagizo ya Amerika na atasitisha kwa mujibu wa mipaka aliyowekewa kufika, ima amejipatia kitu au la kwa kuwa lengo ni kutekeleza mipango ya Amerika kwa kuyarudisha maeneo ambayo yalikuwa hayadhibitiwi na utawala kuyarudisha kwa utawala. Na hivyo rasmi kutambuliwa kama umbile kieneo na kimataifa! Kauli za watu zinadhihirisha hilo kwa uwazi: Muungano wa kimataifa ulithibitisha mnamo Jumanne kwa mujibu wa Kanali Myles B. Caggins, msemaji wa Oparesheni Asili ya Kutatua (OIR) katika ya muungano huo katika Twitter…(Arabi21, 15/10/2019)].
Kwa mujibu wa kauli ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi kwamba (jeshi la serikali ya Syria linaudhibiti kamili wa mji wa Manbij na viunga vyake…(France 24 / AFP 15/10/2019))…Erdogan alizingatia kuingia kwa jeshi la Syria ndani ya Manbij kuwa ni jambo zuri na sio baya! [(Erdogan alisisitiza kwamba kuingia kwa jeshi la Syria ndani ya mji wa Manbij sio vibaya…... (Al-Arabiya 16/10/2019)]...Makamu wa Rais wa Amerika alisema kwamba: [ataongoza ujumbe kwenda Uturuki hivi karibuni, na kwamba Rais wa Amerika amezungumza na mwenziwe wa Uturuki Erdogan na kumtaka kusitisha mara moja uvamizi wa Uturuki ndani ya Syria…(Al-Ghad Channel 15/10/2019)]...
Gazeti la Uturuki la Jumhuriyat lilisema kwamba Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Akar aliripoti [kwamba Ankara inatafuta njia za kuwasiliana na utawala wa Syria…(Arabi21 15/10/2019)]. Moscow ilitangaza kwamba [serikali za Damascus na Ankara zimo katika mazungumzo kufuatia oparesheni za kijeshi za Uturuki kaskazini mwa Syria…(Petra) Ammon Agency 15/10/2019)]. Hivyo basi kampeni ya Oparesheni ya Chemchem ya Amani inaipatia utawala mafanikio mapya, na kuliimarisha umbile lake na kuweka utangulizi kuhusiana na mazungumzo juu yake ambayo yote hayo yasingelifaulu isipokuwa kupitia kampeni hizi ovu!
Yote hayo yanaonyesha kutolewa muhanga kwa watu wa Syria na damu zilizomwagwa na heshima ilivyokiukwa na wahalifu, wanaowafuata, wanaowaunga mkono na zana zao…hazina uzito wowote wala thamani kwa watu ambao wanakwenda mbio kuiridhisha Amerika na mipango yake! Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali inakuwaje wanahadaika. Wanafikiria kwamba kupitia vitendo hivi watawarudisha tena nyuma watu wa Syria katika mikono ya madhalimu washirika wa makafiri wakoloni…Bali kundi la urongo litavunjwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na watakimbia ilhali hawajafaulu chochote kwa sababu walionyanyuka wanataka kuleta nuru inayolingania: "Ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu…" Watu kama hao hawato shtushwa kwa dhiki bali watapa nguvu juu ya nguvu na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu wako katika njia iliyonyooka na hawatojisalimisha katika ukandamizaji na hawatojisalimisha katika fedheha lakini ni wanaume wa wanaume wanafahamu kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja nao katika hali nzuri na mbaya. Na wanapata motisha kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na maisha (Seerah) ya Nabii Wake (saw) kama walivyo Maswahaba katika kuendelea kufanya kazi kuwaondosha madhalimu na kusimamisha Sheria ya Mwenyezi Mungu, Khilafah Rashidah. Kila maisha yanapokuwa magumu kwao, yanafuatiwa na wepesi; kila uzito hufuatiwa na wepesi. Kila Amerika na wanaomuunga mkono wanapofikiria kwamba ushindi upo mikononi mwao, mara wanazinduka na kuona kwamba mambo ni makubwa kuliko walivyofikiria na kwamba vitendo vyao vimechanganyikiwa na kauli zao zinakinzana!
(إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ اللْأَشْهَادُ) “Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi” [Ghafir: 51]. Ushindi sio tu unapeanwa kwa Mitume, lakini pia (والَّذِينَ آمَنُوا) “na wale walioamini.” Ushindi sio tu kwa Akhera, lakini pia (فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ) “wakati wa maisha ya duniani na Siku ambayo mashahidi watasimama”. (إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً) “Hakika, Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake” [At-Talaq: 3].
H. 17 Safar 1441
M. : Jumatano, 16 Oktoba 2019
Hizb-ut-Tahrir