Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 KUFUATIA UVAMIZI, MATESO NA MAUAJI YA WAISLAMU KATIKA MSIKITI MUSA: Kenya Inaendeleza Vita vya Kiulimwengu Dhidi ya Uislamu kwa Niaba ya Bwana Wake Amerika Anaye Tapatapa!

Mnamo Jumapili 2 Februari 2014, polisi wa Kenya walivamia Msikiti Musa mtaani Majengo eneo la Mombasa kwa kisingizio cha kirongo kuwa ndani ya msikiti huo walikuwemo vijana wa Kiislamu waliokuwa wakifunzwa mbinu za kijeshi na kusajiliwa kujiunga na Al-Shabaab ambayo imetangaza vita nchini Somalia.

Wakati wa uvamizi huo, polisi waliingia msikitini na kukiuka desturi zote msingi za kibinadamu za heshima, hadhi na utukufu wa sehemu za kuabudu. Sio hilo pekee, polisi walionyesha kiburi, uovu na ujasiri wa kuingia na viatu vyao msikitini humo. Walianza kuwapiga na kuwadhalilisha waumini katika sehemu hiyo takatifu wakiwajeruhi wengi na kuua baadhi yao. Kitendo kama hicho kwa polisi ni utovu wa nidhamu na unyama wa hali ya juu sana, lakini hili wala haliwashangazi Waislamu. Kadhia ya utovu wa nidhamu na maadili kwa polisi wa Kenya hususan wanapo amiliana na Waislamu ni jambo la kawaida. Ni nani asiyejua kwamba polisi wa Kenya wanaongoza orodha za ulimwengu za utovu wa nidhamu, maadili mabaya, ufisadi, unyanyapaa nk kama ilivyo thibitishwa katika matokeo mengi ya utafiti yaliyo chapishwa na mashirika mengi? Na hili lilithibitishwa tena kivitendo hivi majuzi wakati wa oparesheni katika Jengo la Biashara la Westgate jijini Nairobi.  

Kwa kufanya hivyo, Kenya haijapinda kutokana na mafunzo ya mabwana zake Amerika na Uingereza ambao wameweka kambi za kijeshi nchini chini ya kisingizio cha kuwapa mafunzo polisi wa Kenya ya namna ya kupigana na ugaidi, kutetea na kudumisha usalama wa dola wa ndani na nje. Tunatambua pia kwamba Amerika na Uingereza zinazodai kuwa watetezi wa haki za kibinadamu ndio wakiukaji wakubwa wa haki hizo bandia. Hili limeshuhudiwa katika nchi nyingi wanazozivamia, wakiacha msururu wa mauaji ya halaiki, ubakaji, unyanyasaji na mateso kwa wasio na hatia na udhalilishaji dhidi ya wakaazi kwa kuwadhalilisha kufikia kiwango cha wanyama au zaidi. Hii ni pasi na kutaja kambi zao za mateso kwa jina la jela ambako Waislamu wanazuiliwa. Mifano michache ni Baghram, Abu Ghuraib na Guantanamo ambako Waislamu wanateswa na kudhalilishwa pamoja na heshima yao kuchafuliwa.

Enyi Waislamu watukufu! Vita hivi vinavyo ongozwa na Amerika sio dhidi ya Msikiti Musa au Waislamu wa Kenya pekee bali ni vita dhidi ya Uislamu na Waislamu kote duniani. Amerika imechukua hadhi ya kuwa dola kuu yenye nguvu duniani na huuchukulia ulimwengu mzima kama milki na malisho yake. Huutumia mfumo wa Kirasilimali na nidhamu ya kidemokrasia kulingania kiburi chake na kumlazimisha kila mmoja kushikamana na matamanio yake. Imesema waziwazi kuwa ulimwengu wote uliosalia ima unasimama pamoja na Amerika (kukubali kuwa watumwa wake) au dhidi yake hivyo basi kuhalalisha uvamizi wa kinyama!

Sisi Waislamu tunao mfumo wetu kamili ambao kimaumbile ni tofauti na Urasilimali unao ongozwa na Amerika. Kwa msingi huu, Uislamu na Waislamu unatoa tishio halisi la utawala wake wa kiulimwengu ambao ndio chanzo cha hofu inayo idhihirisha kufikia hadi ya kukanyaga kanyaga ubinadamu na maadili ili kuzuia Uislamu usisimame tena. Kitendo hiki cha Amerika ni sawia na cha Firauni zama za Mtume Musa (as) pindi ilipotolewa bishara kuwa atazaliwa mtoto wa kiume katika nyumba ya watumwa wa Kiyahudi ambaye atakuja kumng'oa katika wadhifa wake. Hili lilimfanya Firauni kuwa na hofu na kuamuru watoto wote wa kiume wa Kiyahudi wanaozaliwa kuuliwa ili kuzuia haki hii. Lakini akashindwa!

Kwa yakini, Amerika na washirika wake wanazidanganya nafsi zao kwani pindi Mwenyezi Mungu (swt) apendapo ushindi kwa waja Wake, Hufungua njia ikawa rahisi licha ya dhuluma na vitisho vilivyoko njiani. Amerika ambaye ni Firauni wa zama hizi ana hofu kwani ni yakini kuwa Urasilimali wake uko katika kitanda cha mauti na karibuni utaangamia na kubadilishwa na Uislamu kupitia serikali ya Khilafah. Hivyo basi, Amerika inatumia mbinu na njama zote zinazowezekana kama kuusingizia urongo Uislamu na Waislamu kwa kuwabandika majina ya 'magaidi' na 'Waislamu wenye siasa kali, ikiwemo kuwaua, kuwatesa, kuwafunga, kuwabaka, nk. yote haya yanalenga kuufanya Uislamu usikaribiwe na kutia hofu katika Waislamu na pia kuwatenga licha ya Waislamu kumiliki mfumo wa kweli ambao utawakomboa Waislamu na wanadamu kutokana na unyanyasaji wote. Vilevile, Amerika na washirika wake wanafanya kazi kupitiliza kuwahusisha Waislamu katika makabiliano ya ndani kwa ndani baina yao kufikia hadi kupigana na kutengana badala ya kuja pamoja dhidi ya adui wao wote na mfumo wake wa kikafiri.  

Vita hivi dhidi ya Uislamu vimejitokeza ulimwengu mzima kupitia namna Waislamu wanavyo uawa pasi na kosa lolote ila kusema 'Mola Wetu ni Mwenyezi Mungu.' Kiulimwengu, Amerika iko mstari wa mbele kupigana na Waislamu moja kwa moja au katika hali nyingine kusaidia unyanyasaji dhidi yao kama nchini Burma. Pia inawalazimisha vibaraka wake kupigana na Waislamu kwa niaba yake kupitia kuwaahidi pesa au kupitia shinikizo. Vita nchini Iraq, Afghanistan, Somalia na mashambulizi ya droni nchini Yemen, Pakistan, vita vya kiwakala nchini Syria kupitia kibaraka wa Amerika Iran au Saudi Arabia ni mifano ya vita viovu vinavyo piganwa kutumia mbinu zote ikiwemo kijeshi, kifikra, kisiasa, kisheria nk. Barani Afrika, hakuna tofauti iwe ni nchini Kenya, Tanzania, Uganda au nchi nyingine yoyote.    

La kusikitisha, huku haya yakijiri katika eneo letu na kote ulimwenguni, serikali changa hujitangaza rasmi kuwa ziko huru kutokana na bwana wa kikoloni. Uhalisia ni kwamba serikali hizi zingali chini ya minyororo ya dola za kikoloni za kirasilimali kwani kadhia zetu zote huamuliwa kwa msingi wa matakwa yao. Hata zinapoagizwa kuwaua raia wao wenyewe, serikali hizi hutii kwa unyenyekevu kama ilivyo shuhudiwa katika orodha ndefu ya wanaharakati waliouwaa nchini Kenya kama Sameer Khan, Aboud Rogo na wengine wengi kutoka Kilindi katika mkoa wa Tanga nchini Tanzania. Hii ndio hali eneo la Afrika Mashariki na maeneo mengine.

Enyi Waislamu watukufu! Kumbukeni kuwa muko katika njia ya haki kwani munasimama na itikadi sahihi inayokinaisha akili na kuafikiana na nafsiya ya kimaumbile ya mwanadamu. Hii ndio itikadi pekee inayomtambua Muumba Mmoja ambaye hahitajii msaidizi wala mshirika yeyote na Dini (mfumo) Yake hutatua matatizo yote ya mwanadamu ulimwenguni na akhera. Tambueni kwamba ni kwa sababu ya mwamko wa Kiislamu ndio ulimwengu mzima unang'ang'ana kujenga uadui dhidi yenu. Endapo dola za kikoloni za kirasilimali zingefaulu kutufanya tuachane na Uislamu na kufuata mfumo wao wa kikafiri, hazinge tuingilia katika mambo yetu. Hivyo basi simameni imara kwa haki kwa kushikamana barabara na njia sahihi ya mabadiliko kama ilivyojitokeza kivitendo kupitia njia ya Mtume ya mabadiliko mjini Makkah hadi kuhamia kwake Madinah ili kuasisi Dola ya kwanza ya Kiislamu. Je, hamuoni kuwa wengi wa wale waliokamatwa Msikiti Musa ni vijana ambao kwa mujibu wa nidhamu ya kidemokrasia na misingi yake ya uhuru, walitarajiwa kujihusisha na vitendo viovu na kinyume na sheria? Hivyo basi, hii ni ishara kuwa kizazi chetu cha vijana kimeamka ili kubeba kadhia nyeti ya Kiislamu na pia ni dalili kuwa ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu hauko mbali. Lakini, ni lazima tufanye bidii zaidi na kukataa kuogopeshwa na vitisho kama hivi isije tukarudi nyuma kwa visigino vyetu. 

Sisi katika Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki tunatoa mwito kwa ndugu zetu Waislamu nchini Kenya na kwingineko kufanya kazi pamoja na walinganizi wenye ikhlasi ili kumakinisha imara mwamko huu juu ya njia yake sahihi ambao utaleta mabadiliko ulimwengu mzima kwa kusimamisha Uislamu kupitia nidhamu yake ya utawala ya Al-Khilafah. Tuweni ngangari na tusiruhusu tutumiwe au kukanganywa na wanasiasa na wanachuoni wa kidemokrasia ambao wameuza Dini yao kwa maslahi duni ya kidunia kupitia kuupigia debe mfumo huu muovu usiokuwa na huruma.  

Kwa kutamatisha, tunatoa rambi rambi zetu kwa wote waliofikwa na mtihani katika Msikiti Musa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awasamehe na kuwakubali wale waliouawa katika Pepo Yake ya milele, awaruzuku afya na nguvu majeruhi na walio kamatwa pamoja na subra kwa familia zao. Na twamuomba aturuzuku sote uwezo na imani na kushikamana imara na njia sahihi ya Mtume ya mabadiliko yenye kupelekea kusimama mapema kwa ngao yetu, Dola ya Khilafah, na kuenea kwa haki kote ulimwenguni. Allahumma Ameen!

يُرِ‌يدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَ‌هُ وَلَوْ كَرِ‌هَ الْكَافِرُ‌ونَ * هُوَ الَّذِي أَرْ‌سَلَ رَ‌سُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَ‌هُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِ‌هَ الْمُشْرِ‌كُونَ

"Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia. * Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia!" [TMQ 9:32-33]

H. 14 Rabi' II 1435
M. : Ijumaa, 14 Februari 2014

Hizb-ut-Tahrir
Afrika Mashariki

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu