Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuchochea Migogoro ya Kimadhehebu ni Mtazamo Uliofichuliwa wa Mayahudi katika Kushinikiza Mauaji na Suala la Kuhama Makao!
(Imetafsiriwa)

Mauaji nchini Lebanon yanaendelea tangu Mayahudi walipoanza uvamizi wao wa kikatili na wa kinyama dhidi yake na watu wake kwa jumla, na dhidi ya watu wa kusini haswa, hadi idadi ya wahasiriwa nchini Lebanon ikazidi 3200, na idadi ya waliojeruhiwa ikafikia 14,000, na karibu watu milioni 1.2 wamelazimika kuyahama makaazi yao, katika sera inayotekelezwa na adui huyu mnyakuzi nchini Lebanon, na alifanya hivyo hapo awali na anaendelea kufanya vitendo hivi katika Ukanda wa Gaza unaoheshimika kwa zaidi ya mwaka mmoja! Katika kipindi hiki, serikali za makafiri za Magharibi, zikiongozwa na Marekani, zinaunga mkono uvamizi huo na kuziba masikio kwa aina zote za vifo na maangamizi yanayowapata Waislamu, na zikatuma wajumbe, wasuluhishi na mawaziri ambao walisisitiza kutangaza Uzayuni wao hata kama hawakuwa Mayahudi! Kwa hivyo, madai yote ya ubinadamu na uhuru na madai ya kuhifadhi haki na sheria za kimataifa yameanguka, madai haya ambayo makafiri, wanafiki, wakoloni wa Magharibi hawaachi kudai kuwa waanzilishi na kututaka tuyatekeleze katika nchi zetu!

Ama watawala wa nchi za Waislamu hawana haya mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, wala Mtume wake, rehema na amani ziwe juu yake, wala Waumini! Wanakusanyika ili kuibua lawama, kila mwaka, katika kumbi za kifahari, huku nyumba, majengo ya makaazi, na maeneo yakibomolewa juu ya vichwa vya wakaazi wake huko Lebanon na Gaza! Kisha wanatoa kauli na kutamka maneno yanayochukiza na kumtia kichefuchefu msikilizaji! Huku majeshi yakiwa yamejikunyata katika kambi zao na zana zao zote, yanazuiwa kucheza dori yao halisi! Badala yake, wanawaamuru kuwakandamiza watu na kuwazuia kukaribia mipaka, badala ya kuwaamuru kupigana na Mayahudi!

Katika uhalisia huu wa aibu na wa mapuuza, Mayahudi hupata muda mwingi wa kufanya mauaji ya kutisha zaidi, kuunda hali ya kusikitisha ya kuhama makaazi, na kisha kuwalenga watu ambao wamehamishwa ndani ya nchi hadi Sidon, Beirut, milimani, na kaskazini mwa Lebanon... na kisha kuwafuata watu hao waliofurushwa na mikusanyiko yao katika maeneo mbalimbali ya watu waliohama makaazi yao, kupiga mabomu maghorofa na kuharibu majengo ya chini kwa kisingizio kuwa miongoni mwa watu hao wanatafutwa viongozi wa Chama cha Iran nchini Lebanon. Watoto na wanawake wanauawa, na familia zinaangamizwa, na watu wa maeneo yaliyowapokea ambayo yanapaswa kuwa maeneo salama ya uhamisho wanaangamizwa! Hili linadhihirisha kuwepo kwa mpango ovu wa umbile la Kiyahudi unaolenga kuzusha mizozo ya ndani ya kimadhehebu na kidini (fitna) nchini humo kwa kueneza hali ya mifarakano na migogoro ya ndani kati ya waliokimbia makaazi yao na umma kwa jumla nchini Lebanon, na kwa kuunda hali ya hofu katika kuwakaribisha waliohamishwa na kutekeleza wajibu unaotakiwa kwao! Hii inasababisha migogoro na mizozo ya kimadhehebu ambayo umbile la Kiyahudi inaitaka, na kuona kwamba migogoro hii inachangia kushambulia nchi hiyo kwenye mipaka yao, kuisambaratisha, na kuidhoofisha juu ya kile ambacho tayari ni dhaifu.

Enyi Watu wa Lebanon kwa jumla, na enyi Waislamu wa Lebanon hasa: Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon, tunaharakisha kuonya dhidi ya kufuata yale ambayo Mayahudi wanataka. Mumepata uzoefu kwa miaka mingi jinsi maadui wa Umma huu kutoka Magharibi, Mayahudi, na watawala vibaraka walivyoishi kutokana na mizozo baina yenu hapo awali, na bado wanafanya hivyo! Tunakukumbusheni kwamba moja ya matendo makuu yenye fadhila ni kuwasaidia walio katika dhiki. Na ni nani mwenye dhiki zaidi kuliko yule ambaye nyumba yake imevunjwa, familia yake imeuawa, na ambaye mali yake imefujwa kutoka kwa watu wetu waliohamishwa ... na kina nani? Na maadui zenu wakubwa, Mayahudi?! Al-Bukhari na Muslim wamepokea kutoka kwa Abu Musa al-Ash'ariy kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ صَدَقَةٌ، قَالَ: أَفَرَأَيْتَ إِنْ لَمْ يَجِدْ؟ قَالَ: يَعْمَلُ بِيَدِهِ فَيَنْفَعُ نَفْسَهُ وَيَتَصَدَّقُ، قَالَ: أَفَرَأَيْتَ إِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ أَنْ يَفْعَلَ؟ قَالَ: يُعِينُ ذَا الْحَاجَةِ الْمَلْهُوفَ، قَالَ: أَرَأَيْتَ إِنْ لَمْ يَفْعَلْ؟ قَالَ: يَأْمُرُ بِالْخَيْرِ، أَوْ بِالْعَدْلِ، قَالَ: أَفَرَأَيْتَ إِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ أَنْ يَفْعَلَ؟ قَالَ: يُمْسِكُ عَنِ الشَّرِّ، فَإِنَّهُ لَهُ صَدَقَةٌ».

“Kila Muislamu lazima atoe sadaka.” Akasema: “Itakuwaje kama hana chochote?” Akasema: “Afanye kazi kwa mkono wake, hivyo ajinufaishe nafsi yake na atoe sadaka.” Akasema: “Itakuwaje ikiwa hawezi kufanya hivyo? Akasema: Amsaidia masikini na wenye shida.” Akasema: “Itakuwaje kama hawezi kufanya hivyo?” Akasema: “Aamrishe mema au uadilifu.” Akasema: “Itakuwaje kama hawezi kufanya hivyo?” Akasema: “Ajiepusha na shari, kwani hiyo ni sadaka kwake.” Basi jihadharini na kuingia katika mtego ambao Mayahudi wanakuwekeeni, kwa kukufanyeni kuwa ni kadhia yenu na ndugu zetu waliohama badala ya kuwahusu Mayahudi wahalifu na wale waliowapatia silaha na vifaa, lakini kwa mamlaka ya Lebanon ambayo inaomba kutekelezwa kwa maazimio ya kimataifa, ambayo matokeo yake si chochote isipokuwa kuhalalisha mahusiano na Mayahudi, ambayo yanamakinisha misingi ya uwepo wa umbile hilo nyakuzi, saliti katika eneo hili, umbile hili ambalo halikuheshimuni wala haikuheshimuni Magharibi iliyo nyuma yake kwa mapatano au agano lolote. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

[لَا يَرْقُبُونَ فِي مُؤْمِنٍ إِلّاً وَلَا ذِمَّةً وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُعْتَدُونَ]

“Hawatazami kwa Muumini udugu wala ahadi; basi hao ndio warukao mipaka.” [At-Tawba:10].

H. 11 Jumada I 1446
M. : Jumatano, 13 Novemba 2024

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu