Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Allahu Akbar... Allahu Akbar... Allahu Akbar
(Imetafsiriwa)

Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko Mayahudi na ufisadi wao na uadui wao... Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko Marekani na kiburi chake... Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko watawala vibaraka wa Waislamu na uatelekezaji na khiyana zao.

Allahu Akbar... Katika siku zilizobarikiwa, damu yetu inamwagika na nyumba zetu zinavunjwa, na watawala wa fedheha hutoa kauli za kukashifu tu.

Allahu Akbar... Je, ni lini ari ya wanaume katika majeshi ya Kiislamu watasonga mbele kuona majeshi yao yakikua katika nyua za Msikiti wa Al-Aqsa?!

Allahu Akbar... Je, jeshi la Misri halina uwezo wa kulitokomeza umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake katika saa moja ya siku?! Je, jeshi la Jordan halina uwezo wa kuliponda umbile la Kiyahudi na kuliondoa? ... Je, majeshi ya Uturuki na Pakistan hayana uwezo wa kuikomboa Jerusalem na kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume Wake?!

Allahu Akbar... Je! nafsi zao hazitamani Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuuawa kishahidi katika Ardhi Iliyobarikiwa?!

Enyi Waislamu: Mjini Jenin, ardhi ya ushujaa, Mujahidina wachache mashujaa walisimama kidete mbele ya ndege, magari ya kivita, na maelfu ya askari, na hawakuziacha silaha zao, basi vipi kuhusu nyinyi enyi askari wa majeshi ya Kiislamu?!

Uimara wa hawa Mujahidina ulimkasirisha adui yenu, ambapo alitoka akiwa amevaa aibu, na hili linadhihirisha nguvu na dhamira ya waumini katika kukabiliana na maadui zao.

Uimara wa mashujaa hao, licha ya uchache wao na zana zao, unawaanika wazi watawala madhalimu wanaoyafunga minyororo majeshi ya Ummah kutekeleza wajibu wao wa kuunusuru Uislamu na Msikiti wa Al-Aqsa.

Wale waliokasirikiwa wanaunajisi Msikiti wa Al-Aqsa asubuhi na jioni, wanavunja nyumba na kumwaga damu, kisha mtu anatujia akisema tunaionya "Israel" dhidi ya kuvuka mistari mekundu! Unazungumzia mistari gani mekundu?!

Je, kuna mistari mekundu iliyobakia baada ya kuvunjwa nyumba, watu kuhamishwa, kumwaga damu, na kuchafuliwa kwa Msikiti wa Al-Aqsa?!

Ama walio katika nafasi mbaya zaidi ni wale wanaoviomba vyombo vya kimataifa na kuvitaka vitoe ulinzi wa kimataifa, ili Uingereza na Marekani zitoe ulinzi kwa watu wa Palestina?!... Kwa nini msiwahutubie wamiliki wa sababu ili wahamasike kuwalinda watu wa Palestina, au je, ulaji njama na khiyana zinakuzuieni kutafuta msaada wa Umma wa Kiislamu na majeshi yake ili kuikomboa Bayt Al-Maqdis?!

Kwa nini taarifa zote zinatolewa na hotuba zote zinachapishwa na vyombo vya habari vinazifunika kabisa, ama kuhusu hotuba ya kweli ya ukombozi na wito wa Umma wa Kiislamu na majeshi yake, hauna nafasi kwao?! Je, vyombo vya habari vitafikisha ujumbe wetu katika misimamo hii kwa Umma wa Kiislamu na majeshi yake? Au vitafanya ubadhirifu na kuegemea upande wa maadui wa Uislamu ambao hawataki sauti hii ipazwe katika nchi za Kiislamu?!

Enyi Waislamu: Kuna njama ya kimataifa na ya kikanda juu ya kuwamaliza Mujahidina katika Ardhi Iliyobarikiwa, na yale yanayotokea mjini Jenin, Nablus na maeneo mengine ni moja ya matunda ya mikutano ya usalama iliyofadhiliwa na Marekani katika kanda hii, ni matunda ya Mkutano muovu wa Aqaba.

Ni makosa ya jinai ya mataifa ya kikanda na Mamlaka ya Palestina, ambayo viongozi wao wanadai kuwa wamesimamisha uratibu wa usalama.

Kwa nini vyombo vya Mamlaka ya Palestina vinaingia katika makao yao makuu, na kila kampeni inayoanzishwa na umbile la Kiyahudi?! Na vipi nafsi za washirika wao zinakubali kudhalilishwa wakiwa wamekaa katika makao yao makuu huku adui akiwaua ndugu zao na kuzihamisha familia zao?! Wanawezake kujisikia wameridhika kupitia kuwakamata Mujahidina na kuwanyang'anya silaha zao?!

Nchi za Magharibi na za Kiarabu zinawataka watu wa Palestina wajisalimishe kwa umbile la Kiyahudi na kuishi nalo kwa udhalilifu na unyonge. Watawala wetu hawajali Msikiti wa Al-Aqsa, wala hawajali watu wa Palestina. Kwa hiyo, wanaichukulia kila harakati ya mapambano katika Ardhi Iliyobarikiwa kuwa ni harakati inayosumbua usingizi wao na kuamsha ari ya mapambano wanayofanya usiku na mchana kuua nyoyo za Waislamu.

Enyi Ummah wetu wa Kiislamu: Sisi kutoka Palestina tunakuhutubieni na kukuambieni, lau watu wa Palestina wangekuwa ndio viongozi, je Ummah ulio hai ungekubali kuvunjwa mkuki wake?! Na ikiwa mashujaa wa Jenin ni watoto wenu, je Ummah utawaangusha watoto wake mashujaa?! Je, usaliti hauadhibiwi kwa kutelekezwa na Mwenyezi Mungu?! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«مَا مِنَ امْرِئٍ يَخْذُلُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلَّا خَذَلَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ وَمَا مِنْ أَحَدٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلَّا نَصَرَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ»

Hakuna mtu (Muislamu) atakayemtelekeza Muislamu mahali ambapo heshima yake inatwezwa na utukufu wake unadunishwa bila ya Mwenyezi Mungu naye kumtelekeza mahali anapotaka msaada wake; na hakuna mtu (Muislamu) ambaye atamsaidia Muislamu mahali ambapo heshima yake inatwezwa na utukufu wake kuvunjwa bila ya Mwenyezi Mungu kumsaidia mahali anapotaka msaada wake.” (Imesimuliwa na al-Tabarani kwa isnad hasan).

Je, mutaiacha Aqsa yenu na Masrah yenu, watoto wenu na ndugu zenu katika Dini na imani chini ya mashambulizi ya umbile la Kiyahudi na uhalifu na dhulma yao huku mkitazama tu?!

Enyi Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa: vumilieni, na mustahamili; kuweni wamoja, na mtakuwa watukufu kwa imani yenu na uthabiti wenu, na ugeukieni Ummah wenu na mtafute msaada wake kwa ajili ya ushindi wenu, na kuwa kichocheo cha mwamko wake na chanzo cha izza. Itegemeeni Dini yenu na Ummah wenu, mtegemeeni Mola wenu, Ambaye mkononi Mwake uko ushindi wenu pekee, na achaneni na miradi ya usaliti na tawala vibaraka, wala msikate tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu.

[إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِنْ رَوْحِ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ]  “Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri.” [Yusuf 12:87]. Msikate tamaa na Ummah wenu kwani wao ndio asili ya mashujaa na wanaume, kwani miito ya Ardhi iliyobarikiwa inayotafuta msaada (Nusrah) ya Umma wa Kiislamu na majeshi yake ili kusimamisha Khilafah na kuikomboa Ardhi iliyobarikiwa, Mwenyezi Mungu atawatolea njia ya kuzifikia nyoyo za Waislamu, ambapo nyoyo zinazotamani Siku ya Ushindi na Tamkini zitawasikiliza. Msiache kuwalingania kwa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawbah 9:38-39]. Kuhamasika kwa majeshi ya Ummah na kukombolewa kwa Bayt Al-Maqdis kutatokea, Mwenyezi Mungu akipenda, hiyo ni ahadi ya dhati.

Ewe Mwenyezi Mungu tufikishie kheri hii kwa niaba yetu na uzifungue nyoyo za Waislamu kwa yaliyomo ndani yake ya kheri na hekima, na utupe kiongozi mshindi kutoka Kwako, Ewe Mwenyezi Mungu, wapokee mashahidi wetu na uwaponye majeruhi wetu, na tupate ushindi wako uliotuahidi.

Ewe Mwenyezi Mungu, waadhibu wale waliokasirikiwa na Mwenyezi Mungu na wale waliokula njama nao. Ewe Mwenyezi Mungu, yajaalie maangamizo yao katika usimamizi wao, na udanganyifu wao dhidi yao, na ulinde Ummah wetu na Dini yetu, na utujaalie tuwe miongoni mwa wale uliowachagua ili kuisimamisha Dini Yako na kunyanyua hadhi ya wito wako. Alhamdulillah Rabb Al Alamin.

H. 17 Dhu al-Hijjah 1444
M. : Jumatano, 05 Julai 2023

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu