Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kwa Amri ya Balozi wa Jumuia ya Ulaya, Serikali ya Mpito imbioni kutafuta Uugwaji mkono!!

(Imetafsiriwa)

Mwanachama wa kamati ya Uchumi ya Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko (Sidqi Kaplo) ametangaza kufanyika kwa mkutano wa mabalozi kutoka nchi za Ulaya nchini Sudan, mikutano na vyama vya kisiasa ili kuwashawishi umuhimu wa kuwaunga mkono kwa haraka na kufutilia mbali uungaji mkono kwa Marafiki wa Sudan kwa Serikali ya Mpito, juu ya pendekezo la Benki ya Dunia pekee, na kutabikisha masharti yake ya ukombozi wa kiuchumi! (Al-Jareeda Toleo Na. 3025)!

Inaonekana kana kwamba Waziri wa Fedha, ambaye ni mtaalamu wa uchumi wa kirasilimali, haelewi uchumi huo isipokuwa kupitia uongozi wa Taasisi ya Fedha ya Kimataifa, hivyo mtu huyu aliendelea kusisitiza nguzo ya dawa hii mbovu; kusitisha ruzuku juu ya bidhaa, haswa mafuta na mkate! Kulifungua athari ya shinikizo kwa mitaa iliyo haribiwa kwa gharama ya juu, jambo lililoingiliwa kati awali na Majeshi ya Tangazo la Uhuru na Mabadiliko, na kukubaliana kuakhirisha usitishaji wa ruzuku hadi kongamano la uchumi lijalo, litakalo fanyika Machi mwakani, lakini shinikizo kutoka kwa balozi za Ulaya, waundaji halisi wa tawi la utendakazi la serikali, ndilo lililo kuwa kauli ya mwisho ya uamuzi katika kuanzisha kusitisha usaidizi kwenye bidhaa hizi mbili mara moja. Hivyo basi, serikali ikaanza kusitisha ruzuku kijanja, kwa kuweka bei mbili tofauti kwa Petroli na Mkate, kama vile Waziri wa Kawi na Madini alivyo tangaza kwamba itaongeza bei ya gasolini ya inayo uzwa kibiashara kuanzia katikati ya Februari. Lita moja itauzwa kwa 28 badala ya Pauni 6. Waziri wa Viwanda na Biashara pia alitangaza: “Serikali ndani siku 45 pia itatekeleza sehemu za uokaji mikate ya kibiashara ambazo zitauza mikate isiyo na ruzuku” (Al-Sharq Al-Awsat,14/02/2020).

Na kwa kuwa serikali ina ukiritimba kwa bidhaa za gasolini na mkate, na inaamiliana na raia wake kwa mtazamo wa mfanyibiashara mlafi, kama serikali ya kirasilimali, serikali ya kutoza ushuru, bidhaa zilizo pewa ruzuku hazito patikana, na natija yake itakuwa ni milolongo mirefu itakayo panua njia ya bidha za kibiashara, hili litawasukuma watu katika bidhaa hizo za kibiashara, hivyo Waziri wa Fedha atatangaza kwa wafadhili wake, Muungano wa Ulaya na Taasisi ya Fedha ya Kimataifa, kufaulu kwake katika kuibua uungwaji mkono unao daiwa!

Waziri wa Fedha, ambaye alitangaza mnamo mwezi Septemba 2019 moja kwa moja baada ya kula kiapo kwamba, moja ya vipengee vya mpango wake wa dharura wa siku 200 (kutabikisha udharura, udhibiti na hatua za kinidhamu ili kumakinisha bei na kuondoa ugumu wa maisha)!! Lakini kila atakaye itazama hali halisi atakuta kwamba ugumu wa maisha umezamisha makucha yake katika shingo za watu, bei za bidhaa zinapanda kila uchao, na pauni ya Sudan imepoteza zaidi ya asilimia 30 ya thamani yake, mpaka roho zimefika kooni, kisha Serikali ya Mpito itakuwa imejiandaa kwa watu wa kawaida kuanza kukusanya ruzuku ili kuwaridhisha wakopeshaji, kama alivyo sema Waziri wa Fedha!!

Enyi Watu wa Sudan: Majeshi ya Tangazo la Uhuru na Mabadiliko ambayo yameyateka nyara mapinduzi yenu na kubandikiza wanasiasa juu yenu wanaomiliki vyeti vya usafiri vya kigeni, wanawaongoza katika kuwaridhisha maadui zenu kwa sera kama zile za serikali iliopita: utabikishaji wa mapendekezo ya Taasisi ya Fedha ya Kimataifa ambayo yatapelekea kuongezeka kwa mateso na wao wangali hawatosheka na hilo. Bali, wanatafuta, chini ya kisingizio cha uwekezaji, kuukabidhi utajiri na rasilimali za nchi hii, katika ukulima, mifugo, madini na kadhalika, wa kampuni za kirasilimali, ili mubakie ndani ya umaskini, njaa na uchochole. Serikali hii na vikosi vya wanasiasa ambao wanaotoa maagizo ya amri za balozi za kigeni ni wakala wa ukoloni mamboleo, na ombi aliloliomba Waziri Mkuu kwa Umoja wa Mataifa mnamo 01/29/2020, la kuiweka Sudan chini ya udhamini wa misheni ya kisiasa kutoka Umoja wa Mataifa, chini ya sura ya sita, si kingine ila ni ufunuo inaotoa maelezo kuhusu matoleo haya!

Mabadiliko ya kweli ni kupitia kuung’oa ukoloni kwa mizizi yake, na hilo sio chini ya mfumo wa kirasilimali, bali kwa kupitia kutabanni Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, utakao tabikishwa na Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, hapo, Mungu akipenda, ndipo mutakapo furahia utajiri wenu, nje ya mikono ya wakoloni na amri za taasisi na balozi zao. Viongozi wacha Mungu chini ya Khilafah, watawaongoza kwa wahyi mtukufu, watatabikisha Uislamu, na kuubeba kote ulimwenguni. Ili kupata wema hapa ulimwenguni na Akhera, Hizb ut Tahrir inawaalika, muwe miongoni mwa wanaofanya kazi.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa mwenyezi mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake yeye tu mtakusanywa” [Al-Anfal:24]

H. 22 Jumada II 1441
M. : Jumapili, 16 Februari 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu