Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Jitihada za Hamdok Kuiweka Sudan chini ya Udhamini wa Kimataifa Zinaweza Kukoleza Kasi Mapinduzi ya Kijeshi Badala ya Kuyazuilia!!

(Imetafsiriwa)

Katika kauli iliyotolewa Ijumaa, 24/4/2020, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha ombi la Sudan kuidhinisha Umoja wa Mataifa kuzindua mpango wa kisiasa, chini ya sura ya sita, kuanzia Mei, (Sudan Tribune). Mpango huu uliombwa na Waziri Mkuu Hamdok katika hotuba yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mnamo 26/1/2020, ambayo alisema, kwa mujibu wa Gazeti la Al-Quds Al-Arabi mnano tarehe 09/02/2020:

 “Sudan iliuomba Umoja wa Mataifa kutafuta mamlaka ya Baraza la Usalama ili kuasisi operesheni ya msaada kwa mpango wa amani, chini ya Sura SITA haraka iwezekanavyo, katika muundo wa mpango maalumu wa kisiasa ulio na sehemu madhubuti ya kujenga amani. Mamlaka ya mpango unaotazamiwa lazima ishughulikie eneo zima la nchi ya Sudan.” 

Ama nguvu za mpango huu, kulingana na chanzo hicho hicho, ni kama ifuatavyo: “kusaidia katika kuhamasisha msaada wa uchumi kimataifa ndani ya Sudan, kuwezesha msaada wa kibinadamu Sudan yote, kupeana msaada wa kiufundi katika kuandika katiba na marekebisho ya kisheria na kimahakama, marekebisho ya utumishi wa umma na sekta ya usalama, na kusaidia kurudisha wakimbizi wa kindani na wakimbizi kutoka nje, na kuwaregesha makwao na kuwaunganisha tena na jamii, na maridhiano baina ya jamii za kindani, kufaulisha amani, haki ya mpito, ulinzi kwa raia, na kujenga uwezo kwa jeshi la kitaifa la polisi kwa mbinu mbalimbali, ikiwemo kupelekwa washauri kutoka Umoja wa Mataifa na polisi wa Muungano wa Afrika.”

Barua ya Hamdok kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliwekwa kama siri kwa wiki mbili mpaka ilipovuja kwa magazeti na ikawekwa wazi. Kisha upande wa kivitendo ukaanza: Uingereza ikapeana, baada ya kuiacha Ujerumani kushiriki nayo, rasimu ya azimio kwa Baraza la Usalama mwisho wa mwezi Machi, na magazeti kuunasibisha mradi huo na hotuba ya Hamdok. Kama Al-Intihaba (gazeti la mtandaoni) ilivyo ripoti mnamo 30/3/2020:

“Rasimu ya azimio la Umoja wa Mataifa ambayo Uingereza imeisukuma baada ya Ujerumani kuhusika katika kuitayarishia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ili kuzindua mpango wa kisiasa kuhifadhi na kujenga amani ndani ya Sudan, inaashiria upana wa juhudi za serikali ya Hamdok kuiweka Sudan chini ya udhamini wa kimataifa na kuiregesha tena katika Taji la Mamlaka.”

Kufikia hatua hiyo, balozi wa Uingereza jijini Khartoum alipoteza akili yake na kuonesha kukasirika kwake kwa kuvuja kwa hotuba ya Hamdok, na wale walio inasibisha na kielelezo cha azimio hilo. Balozi huyo alisema, kwa mujibu wa tovuti ya TagPress: “kuvujisha kielelezo cha azimio hilo wakati huu ni uzembe mkubwa sana, na kufanya uidhinishaji wa kielelezo hicho cha azimio katika Baraza la Usalama kuwa vigumu.”

Akaongezea: “Kama mulivyo fuatilia, kuvuja kwa kielelezo cha azimio hilo na kuchapishwa katika vichwa vya habari vya magazeti Khartoum kulisababisha kampeni ya vurugu ya kiupinzani dhidi ya Serikali ya Sudan. Ningependa kuwa wazi. Ni rasimu azimio ya awali ambayo inaashiria mawazo ya Uingereza na Ujerumani, na hatujaionesha serikali ya sudan, serikali ya Sudan haina mchango wowote kwa hilo, na haiwezi kudaiwa kuwa inaashiria maoni ya serikali ya Sudan, ama ina uungaji mkono wake.

Kwa mtazamo wa uhalisia huu, sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan tungependa kuweka bayana ukweli ufuatao:

Kwanza: Waziri mkuu Abdullah Hamdok, ambaye anafuata amri ya ubalozi wa Uingerza, anatafuta, kwa msaada wa Uingereza , kuiregesha Sudan katika ukoloni wa jadi; kupeana mamlaka kwa mataifa juu ya nchi nzima, kwa kuhamisha nguvu zote za katiba ya serikali kwa mpango wake; ombi hili linapeana Baraza la Usalama nguvu za mahakama ya kikatiba na kufanya mahakimu kutabikisha hati za kikatiba, na kufanya taasisi zote vibaraka wa serikali ya mpito kwa uongozi wa mpango wa Umoja wa Mataifa! Je, huu sio ukoloni wenyewe?

Je, matendo ya Hamdok na serikali yake ya mpito yanawapa nguvu wakoloni juu ya nchi, kutupilia mbali madai ya uhuru na kujitawala?

Pili: Kuficha kwa Hamdok hotuba yake kutoka tarehe 26/1/2020 mpaka ilipo fichuka baada ya kuvuja tarehe 9/2/2020, kisha kukasirika kwa balozi wa Uingereza kuhusiana na kuvuja kwa hotuba hio kutoka kwa Afisi ya Hamdok. Yote haya ni ushahidi wa njama inayo pangwa na Waziri Mkuu akisaidiwa na Balozi wa Uingereza na serikali yake kuiweka chini ya udhamini wa kimataifa!!!

Tatu: Hamdok, ambaye anaongozwa na Uingereza, anataka kuiweka Sudan chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa ili kuukatilia mbali uongozi wa wanajeshi unao nasibishwa na ubalozi wa Amerika, kutokana na mapinduzi dhidi ya serikali yake, hususan kwa kuwa serikali yake imeshindwa kutatua shida zote za watu nchini, katika upande wa kimaisha, ama kutoa malalamishi na kufanikisha haki katika faili za wale walio uwawa, ukiukaji wa taasisi za Bashir ama kesi ya kuvujwa kwa vikao na mengineo.

Nne: Mwenendo wa Hamdok unaweza usiwe na natija nzuri kwamba utaongeza kasi ya mapinduzi ya kijeshi badala ya kuyazuilia, haswa onyo la mara kwa mara la serikali ya mpito ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya kuongezeka kwa amri ya kutotoka nje katika mji mkuu, kwa muda wa wiki tatu kwa sababu ya mkurupuko wa Janga la Korona, ikiwemo nukuu ya Arab ukurasa wa 21 kutoka katika New York Times kwamba afisa wa Amerika amesema, kwa sharti kutotambulishwa:

 “Viongozi waoga wa kiraia wa Sudan, ambao umaarufu wao umetingishika katika miezi ya karibuni huku uchumi ukipata pigo, mara kwa mara wamekuwa wakionywa juu ya uwezekano wa mapinduzi ya kijeshi jijini Khartoum kwamba wamekuwa sawa na mvulana aliyelilia mbwa mwitu” na ikiwemo jana jioni katika mahojiano ya televisheni ya Sudan TV 25/04/2020 na Rais wa Baraza Huru, Abdel Fattah Al-Burhan; ambapo alishutumu vyama vya kisiasa kwa kuunda vikundi ndani ya Jeshi, akisema: [Baadhi ya vyama (ambavyo hakuvitaja) vinajaribu kuwasiliana, na kuwasiliana na wafanyikazi wa taasisi za kijeshi, na akaongezea kwamba kuna viini vya baadhi ya vyama, akiashiria kwamba mapinduzi yote yaliyo tokea Sudan hayakufanywa na vikosi vya kijeshi pekeyao]”

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tumejitolea kuukomboa Ummah kutokana na Ukoloni, na hilo lahitaji kuweka wazi yote yanayo tokea nyuma ya pazia ya mipango ya wakoloni makafiri na ala zao zinazo tabikisha mipango hii. Ummah hautakombolewa kutokana na ukoloni isipokuwa kupitia sheria za Kiislamu, zinazo tabikishwa na serikali ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, inayo ongozwa na viongozi wanaojifunga na Uislamu, watiifu kwa itikadi yao na ummah wao, walioimarishwa na ufahamu wao wa kisiasa, ambao watawang’oa wakoloni makafiri katika nchi yetu, na ambao watabeba Uislamu kwa Walimwengu.

Tunawalingania wenye ikhlasi katika watu wenye nguvu na ulinzi, katika siku hizi za utiifu na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu; katika mwezi huu mtukufu, kutekeleza jukumu zito mabegani mwao, ili watafute kujiweka huru (kutokamana na madhambi) kwa kukabidhi mamlaka kwa Hizb ut Tahrir, ambayo inafanya kazi katika nchi nyingi za Waislamu  kupokea nguvu ili iunde kitovu imara cha dola ya Kiislamu. Kuunganisha ulimwengu wa Kiislamu katika dola ya Khilafah Rashida ya pili, ambayo Mtume wa uongofu (saw) alitoa bishara yake njema, ili kupata ushindi mkubwa. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

(وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَداً ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ)

Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

 

H. 3 Ramadan 1441
M. : Jumapili, 26 Aprili 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu