بسم الله الرحمن الرحيم
Serikali ya Uswidi Yawataka Waislamu Waachane na Uislamu!
(Imetafsiriwa)
Vituo vya televisheni vya Uswidi vya SVT na TV4 viliripoti mnamo Jumamosi usiku kwamba Waziri wa Usawa, Paulina Brandberg (wa Chama cha Kiliberali), anataka wafanyikazi wa mashule waripoti wasiwasi wote kwa Huduma za Jamii kuhusu wasichana kuvaa hijabu.
Waziri huyo wa Usawa alitangaza mnamo Jumamosi kwamba wafanyikazi wa shule hawana chaguo na ni lazima waripoti wasiwasi kwa Huduma za Jamii kuhusu wasichana wanaovaa hijabu, na kwamba wafanyikazi ambao hawatatii watakabiliwa na matokeo kwa kushindwa kwao kutii.
Naibu Waziri Mkuu Ebba Busch (wa chama cha Christian Democrats) aliandika kwenye jukwaa la X chini ya wiki moja iliyopita kuhusu mpango mpya ambapo alionyesha sera hiyo hiyo ya oanishaji kama ya serikali: “Idadi ya watu wanaotekeleza Uislamu nchini Uswidi na Ulaya, kama ilivyo kwa nchi za kiimla, ni kubwa mno. Hili lazima likome. Uislamu lazima ujichanganye na maadili yetu msingi ya kawaida.
Kinachomuudhi na kumkasirisha Ebba ni kwamba Waislamu nchini Uswidi wanatekeleza Uislamu, wanashikamana na kitambulisho chao cha Kiislamu na kutekeleza ibada zake, ikiwemo kuvaa hijabu. Ebba anataka kukomeshwa kwa hili.
Hii sio habari ya kupotosha inayolenga kuharibu sifa ya Uswidi ulimwenguni. Haya ni maneno ya mawaziri wenyewe, na majaribio duni ya kusema kwamba hii ni sintofahamu hakuwadanganyi Waislamu.
Waislamu hawaamini kwamba madai ya kejeli ya Ebba Busch anafanya hivyo kwa manufaa ya Waislamu “wazuri” na kwamba anafurahia kuwa upande wao. Hii ndiyo sura halisi ya serikali ya Uswidi na hii ndiyo sera yake dhidi ya Uislamu ambayo kwayo inabeba jukumu la kimataifa!
Sera za serikali hususani hila za vyama hivi haziwawakilishi watu wa Uswidi, na hivyo hili linawapa jukumu kubwa zaidi wananchi kutangaza kuwakataa wawakilishi wao wa vyama kwa kutumia sera hizo zinazoifanya nchi ya Uswidi kuwa mbaya zaidi.
Sera ya serikali ya Uswidi ya kuwaoanisha watoto wa Kiislamu inalenga kufuta kitambulisho chao cha Kiislamu, ikiwa ni pamoja na wajibu wa kibinafsi wa Kiislamu kama vile hijabu. Serikali ya Uswidi inazidisha vita vyake dhidi ya maadili na kitambulisho cha Waislamu kwa kuharamisha hijabu na kuwateka nyara watoto kutoka kwa wazazi wao ikiwa watasisitiza kuwalea kwa mujibu wa maadili ya Kiislamu.
Enyi Waislamu: Kujihifadhi kibinafsi, familia ya mtu, na kudumisha kitambulisho cha Kiislamu ni wajibu wa Kisharia. Anasema Mola wetu Mlezi (swt):
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَاراً وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ]
“Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe.” [At-Tahrim: 6].
Tunayoyapitia sisi Waislamu ni kwa sababu sisi ni madhaifu na tunatenda kama watu waliogawanyika. Ni lazima tutende kama kundi moja, yaani, kama kundi muhimu katika jamii ambalo linachangia kwa njia chanya. Nchini Uswidi, kuna Waislamu zaidi ya milioni moja ambao wanahitajika na jamii ya Uswidi na hawawezi kuishi bila wao. Wao ni sehemu muhimu ya sekta ya usafiri, afya, elimu na kadhalika. Wanatii utaratibu wa umma katika jamii na hawaleti tishio au tatizo lolote kwa jamii, na wanakataa kutendewa hivyo. Ikiwa watatenda kama mwili mmoja, wanaweza kukomesha sera hii ya uoanishaji.
Njia ya kufikia hili si kwa kupitia uwiano, ambao una maana ya kuachana na maadili ya Kiislamu na kukumbatia maadili ya Kimagharibi au kushiriki katika mfumo wa kisekula. Mambo haya ni kinyume cha hayo, mangati ambayo baada ya muda mrefu yanapelekea Waislamu kusambaratika katika thaqafa ya Kimagharibi. Wajibu wetu ni kujipanga kifikra na kisiasa; kifikra kwa kupitia kujenga mwamko baina ya vizazi vipya kuhusu mfumo na fahamu za Uislamu ili kuhifadhi kitambulisho cha vizazi hivi na kuzuia majaribio ya kuviingiza usekula. Katika ngazi ya kisiasa, Waislamu lazima wazingatie sera hizi kama suala la kutisha ambalo linawaathiri Waislamu wote nchini Uswidi na kutishia imani na kitambulisho chao. Upinzani wa kisiasa lazima uwakilishwe na Waislamu wanaofanya kazi kama mwili mmoja kupitia shughuli zinazoathiri rai jumla.
Tuna nguvu kubwa na tunaweza kushawishi rai jumla ya Uswidi, ambayo inapotoshwa na kutumiwa vibaya na uongozi fisadi wa kisiasa kwa uwongo na hila. Endapo tutaupa mgongo wajibu wetu, hali ya Waislamu nchini Uswidi itazidi kuwa mbaya. Anasema Mola wetu Mlezi (swt):
[وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّى يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا]
“Wala hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza.” [Al-Baqara: 217]. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللهِ هُوَ الْهُدَى]
“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu.” [Al-Baqara: 120].
H. 6 Rabi' I 1446
M. : Jumatatu, 09 Septemba 2024
Hizb-ut-Tahrir
Sweden