Jumanne, 01 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kuunganishwa kwa Matukio ya Kimataifa ya Njama dhidi ya Mapinduzi ya Ash-Sham
(Imetafsiriwa)

Tawala za Kiarabu zilikubali kwa kauli moja, baada ya mpasuko wa dhahiri na utawala dhalimu wa Bashar Assad uliodumu kwa miaka kumi na mbili, kumregesha kwenye Umoja wa Kiarabu.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu walikutana mjini Jeddah mnamo siku ya Jumapili, tarehe saba ya mwezi huu wa Mei, kujadili kuregea kwa utawala wa kihalifu katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu baada ya kusimamishwa uanachama wake miaka kumi na mbili iliyopita, hasa tangu tarehe 16 Novemba 2011. Uamuzi wa kuuregesha utawala huo ulifanywa kwa kauli moja. Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Sameh Shoukry, ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, alisema katika hotuba yake wakati wa mkutano huo, kama ilivyoripotiwa na idhaa ya Jordan Al-Mamlaka, akisema: "Hatua zote za mgogoro wa Syria zimethibitisha kwamba hakuna suluhu ya kijeshi juu yake, na kwamba hakuna mshindi au mshindwa katika mzozo huu."

Aliongeza, "Tuna hakika kabisa kwamba njia pekee ya kufikia suluhu ni kupitia suluhu ya kisiasa na ubwana wa Syria, isiyo na maagizo ya kutoka nje, na kwa kutekeleza taratibu zinazohusiana na kufikia makubaliano ya kitaifa kati ya ndugu wa Syria, kujenga uaminifu, na kuendeleza mikutano ya Kamati ya Katiba kwa kuzingatia maregeleo ya kimataifa na Azimio nambari 2254 la Baraza la Usalama, kwa namna ambayo inakidhi matarajio ya watu wa Syria na kutambua matumaini yao halali ya mustakabali mwema."

Tarehe kumi mwezi huu kulifanyika mkutano jijini Moscow wakiwemo mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi, Iran na Uturuki pamoja na waziri wa mambo ya nje wa utawala huo wa kihalifu.

Kilichotokea katika siku chache zilizopita ni kilele cha mpango wa njama wa muda mrefu ambao Marekani na vyombo vyake kutoka kwa tawala za kihaini imeanzisha ili kuyaondoa mapinduzi ya Ash-Sham tangu kuasisiwa kwake.

Marekani iligawanya dori na kupanga mipango ya kuyaondoa mapinduzi ya Ash-Sham, ambayo yaliibuka dhidi ya kibaraka wake huko Damascus, kwani ilitambua kwamba mafanikio ya mapinduzi haya na kufikiwa kwa malengo yake ya kumpindua kibaraka wake Bashar na kuanzisha utawala wa Kiislamu juu ya magofu yake yangetishia maslahi yake na hata uwepo wake, na yangesababisha tawala vibaraka katika eneo hilo kuporomoka mmoja baada ya mwingine, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Marekani inataka kuyamaliza mapinduzi ya Ash-Sham kupitia suluhisho la kisiasa inalotaka kulazimisha. Mbele yake ilikuwa ni Azimio 2254 na mikutano ya njama iliyofuata huko Geneva, Sochi, na Astana, ambayo ililenga kuchukua hatua mtawalia ili kudhibiti chimbuko la mapinduzi na kukuza hali ya kukata tamaa nyoyoni mwake, kukubali suluhu zilizowekwa juu yake, ambazo zingeweza kuzalisha upya utawala wa kihalifu na kuyamaliza mapinduzi ya Ash-Sham na wafuasi wake wanyoofu.

Mipango hii ya njama ilibidi ijumuishe zana za ndani, ambazo zilitekelezwa na ujasusi wa baadhi ya makundi, yakiongozwa na ujasusi wa ile iitwayo Hay'at Tahrir al-Sham (HTS), chini ya maelekezo ya uongozi wake shirikishi.

Haya yanafafanua kile ambacho ujasusi wa ile inayoitwa "Tahrir al-Sham" ulifanya asubuhi ya siku ambapo tawala za Kiarabu ziliregesha utawala wa kihalifu kwenye shirika lake, kupitia kukamatwa kwa Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Syria na idadi ya wanachama wa Hizb, katika jaribio la kutapatapa la kunyamazisha sauti zinazolingania haki, wale wanaofanya kazi ya kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu duniani, wakibeba liwa' (bendera) ya kurekebisha njia ya mapinduzi na kuregesha nia yake.

Namna ya kikatili ambayo walivamia nyumba, kuwatisha watoto, na kukiuka matukufu ni ushahidi wa kukengeuka kwao kutoka kwa misimamo ya mapinduzi ya Ash-Sham na jaribio lao la kutuma ujumbe kwa yeyote anayepinga dori yao na sera ya mabwana zao katika kufanya kazi kuelekea kuhalalisha mahusiano na utawala wa kihalifu na kutafuta suluhisho hatari la kisiasa.

Enyi Watu Wetu Wanyoofu Katika Mapinduzi ya Ash-Sham

Ukweli kuhusu dori ya zana za ndani na nje umefichuka. Hakuna kilichobaki kwenu isipokuwa kuregea kwa Mwenyezi Mungu, kumtegemea Yeye, kuinusuru Dini yake, kukusanyika pamoja kutafuta hifadhi katika kamba yake peke yake, na kukabiliana na majaribio yote ya kufanya njama dhidi ya mapinduzi na kuyatawala. Fanyeni kazi kwa bidii na uthabiti kuuangusha utawala wa kihalifu na kusimamisha utawala wa Uislamu kwenye magofu yake kwenye kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Basi, baada ya Tawakkul (kumtegemea kwenu) Mwenyezi Mungu, msiogope vitimbi vya wapangaji, vitimbi vya walaghai, au uadui wa wenye kiburi. Kuweni na hakika kwamba ushindi wa Mwenyezi Mungu unakuja, na ahadi yake kwa Waumini wa kweli itatimia, na ushindi wake uko karibu.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi. [Ghafir: 51].

#منتهك_الحرمات_عراب_المصالحات

H. 21 Shawwal 1444
M. : Alhamisi, 11 Mei 2023

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Syria

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu