Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Al-Waqiyah TV:

Kampeni “Inatosha Miaka 100 ya Unyonge!”

Katika mwezi wa Rajab Tukufu mwaka huu, 1445 H - 2024 M, inarudi kwetu kumbukumbu ya uchungu ya miaka 103 H na 100 M ya kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu na wahalifu wa Kiarabu na Kituruki, ambayo iliasisiwa na Bwana wa Mitume Muhammad (saw), na maswahaba zake watukufu (ra), na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu mwaka 1342 H, sawia na 03/03/1924 M, na ardhi iliyobarikiwa (Palestina) ilipotea kwa kupotea Imam ambaye ni ngao, Khalifa wa Waislamu ambaye kwaye wanapigana nyuma yake na kujihami..Bali Umma wa Kiislamu ulipotea na vivyo hivyo fahari yake na adhama yake, na hata nchi yake na utajiri wake..

Leo, miaka 100 M, inarudi tena kwetu kumbukumbu uchungu na mauaji ya kikatili ya umbile ovu nyakuzi la Kiyahudi (mauaji ya halaiki) yanayoendelea dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ambao katika muda wa miezi minne tu limesababisha mauaji na kujeruhiwa kwa zaidi ya wanaume na wanawake 100,000 Waislamu, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee. Kwa sababu hiyo, Al-Waqiyah TV inaandaa, katika siku hizi ngumu, msururu wa video za amali na mahojiano chini ya kichwa:

“Inatosha kwa Miaka 100 ya Unyonge!”

Ili kuamsha azma ya Waislamu kwa jumla na watu wenye nguvu miongoni mwao haswa kufanya kazi kwa bidii na Hizb ut Tahrir kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume, kwani kupitia kwayo pekee ndio izza ya dunia na wokovu wa Akhera, na ndio pekee yenye uwezo wa kukomboa ardhi na wanadamu kutokana na makafiri wahalifu.Tunamuomba Mola Mtukufu Ajaaliye kusimama kwa Dola ya Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume iwe karibu, na atukirimu (swt) kwa kiapo cha utiifu (bay’ah) kwa Imam Muongofu, ambaye nyuma yake tutapigana. Ni Mola mwema Msaidizi mwema alioje.

Ijumaa, 28 Rajab Tukufu 1445 H sawia na 09 Februari 2024 M

Kalima ya Ufunguzi

ya Kampeni “Inatosha kwa Miaka 100 ya Unyonge!”

iliyo wasilishwa na Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Muhammad)

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Ijumaa, 28 Rajab Tukufu 1445 H sawia na 09 Februari 2024 M

- Kalima kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 100 M ya Kuvunjwa Khilafah -

[Kalima ya Ustadh Sayed Shalabi / Uswidi]

[Kalima ya Mhandisi Baher Saleh / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)]

[Kalima ya Ustadh Bilal Al-Qasrawi / Wilayah Jordan]

[Hotuba ya Ustadh Haitham Thabet / Amerika]

[Ustadh Abdulhakim Othman / Malaysia]

[Al-Hajj Naji / Denmark]

[Dada Khadija Sheikh / Wilayah Syria]

[Ustadh Khobayb Karbaka / Wilayah Tunisia]

[Ustadh Eldar Khamzin / Uzbekistan]

[Ustadh Mobin Abu Dawud / Tajikistan]

[Ustadh Abdulaziz Moneis / Wilayah Kuwait]

[Ustadh Akeel Abu Umar / Uholanzi]

[Dkt. Muhammad Ismail Yusanto / Indonesia]

#أقيموا_الخلافة

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#RealChange

#TurudisheniKhilafah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu