Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 361
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Wale Wanaompenda Kikweli Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ni lazima Wasimamishe Tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo ndiyo itakayolinda Heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).
Mnamo siku ya Ijumaa, Oktoba 15, 2021, Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia iliandaa visimamo baada ya swala ya Ijumaa jijini Tunis na katika miji ya Kairouan na Sfax ili kukabiliana na upuuzi wa kisekula na njia ya kisiasa inayoharibu nchi.
Kadhia za Ummah "Mkasa wa Waislamu nchini India"
Jumamosi, 9 Oktoba 2021, Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina iliandaa visimamo vitatu mjini Ramallah, Hebron na Tulkarm, ambapo ilitoa wito kusonga kwa uhalisi kwa majeshi ya Waislamu kujibu uamuzi wa uvamizi wa kuwaruhusu Wayahudi kutekeleza ibada zao katika makawanda ya Msikiti wa Aqsa Uliobarikiwa.
Kwa kuzingatia masaibu wanayopitia Waislamu katika biladi tofauti tofauti ya ukandamizaji, umasikini, mauaji, kuhama makaazi, mauaji ya halaiki, na uchafuzi wa heshima kwa Rohingya, Uyghur, Kashmir na India, na hali duni ya maisha ya mamilioni ya wakimbizi katika kambi na kunyimwa kwao wengi mahitaji ya kimsingi nchini Syria, Yemen na Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na kwengineko katika upande mmoja