Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  3 Muharram 1443 Na: 1443/01
M.  Jumatano, 11 Agosti 2021

 Tunatoa Rambirambi Zetu za Dhati kwa Kuuwawa Shahidi Hamid ur Rahman Sharifi, Mbebaji Ulinganizi wa Hizb ut Tahrir!
(Imetafsiriwa)

Hamid ur Rahman Sharifi, mbebaji ulinganizi wa Hizb ut Tahrir, aliuwawa shahidi mnamo 8 Agosti kwa shambulizi la makombora lililotokana na mzozo mkali katika mkoa wa Kunduz.

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea!” [Baqara: 156]

Sharifi, mhitimu wa Kitivo cha Uchumi, alikuwa mmoja wa wabebaji wachangamfu wa Dawah wa Hizb ut Tahrir ambaye bila kuchoka alijitolea muhanga kwa dhati katika ulinganizi wa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Mwenyezi Mungu (swt) akubali kuuwawa kwake shahidi na amuweka miongoni mwa mashahidi waliotoa Nussrah kwa Uislamu hapo mwanzoni.

Vita vya sasa nchini Afghanistan ni matokeo ya miaka ishirini ya uvamizi wa Amerika ambayo, chini ya pazia la vita dhidi ya ugaidi, ukweli vilipiganwa dhidi ya Uislamu na Waislamu. Kwa hivyo, tangu mwanzo, mkakati na nia ya Amerika nchini Afghanistan haikuwa kuhakikisha utulivu na amani hapa, lakini kukabiliana na maadili ya Uislamu kwa kuwakandamiza Waislamu wa eneo hili.

Hakuna shaka kwamba Amerika imeshindwa nchini Afghanistan licha ya kutumia mabilioni ya dolari, na kufanya kila moja kuanzia George W. Bush hadi Obama na kutoka Trump hadi Joe Biden kupata mifadhaiko mikubwa. Moto wa vita katika kila barabara na kichochoro cha Afghanistan, kama vile Syria, Iraq, Yemen na Libya, unaakisi nia ya Amerika ambayo imelenga kudhoofisha nchi hii. Wale walioiamini Amerika kwa miaka ishirini iliyopita lazima watambue matokeo ya kushirikiana na uvamizi huo kwa kile ambacho uvamizi umefanyia hatma ya watu hadi sasa. Uvamizi  huo haukuleta tu vita na ukosefu wa usalama bali uliongeza wigo wa ufisadi, umaskini, ukosefu wa ajira, uhamiaji na la muhimu zaidi, ulieneza maadili ya Kimagharibi katika Ummah.

Kwa sasa, watu kadhaa na/au hata mamia ya watu wasio na hatia wanauawa au kujeruhiwa kila siku kutokana na mzozo mkali na mashambulizi ya angani ya ndege za Amerika aina ya B-52. Kwa kuongezea, idadi kubwa ya watu wanahama makaazi yao kila siku.

Viongozi wa kisiasa, watu wenye ushawishi na wanachuoni lazima wazingatie akilini miaka 20 ya uvamizi wa Amerika na Magharibi ambao umesababisha mauaji ya Waafghan na uhalifu wa kivita katika nchi hii. Simameni dhidi yao na vibaraka wao ili mfumo huu fisadi wa Kimagharibi, unaoandamana na vita, maonevu na mateso uondolewe kutoka kwa uso wa ardhi yetu. Hivyo basi, fanyeni kazi na wabebaji Dawah wa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, mfumo unaomridhisha Mwenyezi Mungu (swt) na vile vile unalinda maisha, mali, heshima na matukufu ya watu. Kwani Hamid ur Rahman Sharifi alikuwa mmoja wa wabebaji Dawah ambao kusudi lake lilikuwa kusaidia kuhuisha maisha ya Kiislamu. Kwa kweli ni kwa sababu ya muhanga wa wabebaji Dawah kwani tunawaona maelfu yao wakijitahidi kuleta maisha ya Kiislamu kote nchini Afghanistan.

]مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.”      [Al-Ahzab: 23].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu