Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  5 Muharram 1443 Na: 1443/02
M.  Ijumaa, 13 Agosti 2021

Watu Wenye Ushawishi na Viongozi wa Kisiasa Hawapaswi Kuwasukuma Waafghani Kugeuka kuwa Watu wa Mstari wa Mbele wa Nidhamu ya Kidemokrasia na Wamiliki wa Pasipoti Nyingi!
(Imetafsiriwa)

Ashraf Ghani, Rais wa Afghanistan, katika mkutano mmoja na viongozi kadhaa wa kisiasa na wawakilishi wa makabila wenye ushawishi, alisisitiza juu ya uhai na kudumu kwa 'Jamhuri' ambapo walikubaliana juu ya kuhamasisha, kuimarisha na kuyahami kwa haraka uasi wa umma dhidi ya shambulizi la upinzani wa kisilaha [Taliban].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan inawaonya viongozi wenye wa kisiasa wenye ikhlasi na watu wenye ushawishi kutowashajiisha watu wa kawaida kujihusisha katika vita vya sasa vya uharibifu kwa kupoteza damu ya vijana wa Kiislamu ili kuimarisha nidhamu uliopo uliyooza, yenye kiu ya damu na ufisadi.

Timu iliyopo ya watawala inajumuisha wamiliki wa pasipoti nyingi ambao wamekuwa wakifuja na kupora mali za watu wa Afghanistan hadi sasa; hata hivyo, wataikimbia nchi endapo hali itazidi kuwa mbaya. Kikosi hicho cha sasa hakilipi hakijali kamwe na/au kuwathamani watu wa nchi hii. Kwa kuwa wanapambana na njia ya uhai na kifo kwa sababu msingi wa nguvu zao unakaribia kusambaratika, wamewageukia viongozi na watu wenye ushawishi kutumia ushawishi wao kwa kuwafanya watu wa kawaida kushiriki katika vita hivi vichafu ili kuhifadhi mfumo wao fisadi kwani siku zao zinahesabika.

Ni wakati mwafaka sasa kwa viongozi wenye ikhlasi wa kisiasa na watu wenye ushawishi kuwa macho sana wakati huu kwani wamezungukwa na fitna ya ndani na nje kutoka pande zote, na kutambua jukumu lao kuu na majukumu ya Kiislamu ambayo ni kukomesha umwagikaji wa damu mara moja ili wasianguke ndani ya mtego wa mipango ya wageni. Kwa sababu lengo kuu la wanajeshi wavamizi, vibaraka wao na mashirika ya kijasusi ni kusababisha ghasia kwa kutekeleza mauaji [umwagaji damu] nchini Afghanistan ili kupata maslahi makubwa na/au udhibiti. Katika hali kama hiyo ya machafuko, hawapaswi kuhusika katika biashara yenye faida na ya kumwaga damu, chini ya kisingizio cha uasi wa umma, kwa kutoruhusu watu wageuke kuwa mstari wa mbele wa mfumo wa kifisadi na/au kibaraka pamoja na wamiliki wa pasipoti nyingi. Wakati huo huo, aya ifuatayo ni onyo la kutisha kwa wale viongozi ambao wanajaribu kuwashirikisha na kuwashajiisha watu kupigania njia ya mfumo wa fisadi uliopo sasa.

Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(وَمَنْ يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا)

“But whoever kills a believer intentionally - his recompense is Hell, wherein he will abide eternally, and Allah has become angry with him and has cursed him and has prepared for him a great punishment.” [An-Nisa’: 93].

Kutokana na hayo, Hizb ut Tahrir inatoa wito kwa Umma wenye ikhlasi, makundi tofauti tofauti, na watu wenye nguvu nchini Afghanistan kutambua haja muhimu mno ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume na kutambua kuwa suluhisho la kizungumkuti nchi Afghanistan na eneo hilo halitapatikana kupitia mazungumzo ya amani na kuendelea kwa vita, bali kwa kusimamisha Khilafah na utabikishaji kamili wa Uislamu. Hatimaye, unganisheni mikono pamoja na Hizb ut Tahrir na mtambue kuwa Mwenyezi Mungu (swt) huwanusuru wale wanaounusuru Uislamu.

أفغانستان#   #Afganistan   #Afghanistan

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu