Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  18 Dhu al-Hijjah 1442 Na: Afg. 1442 H / 16
M.  Jumatano, 28 Julai 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vita vya Uharibifu na Amani ya Fazaiko Ndio Urithi Mkuu wa Amerika nchini Afghanistan!
(Imetafsiriwa)

Ujumbe wa Usaidizi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA), katika ripoti ya hivi karibuni, ulielezea miezi sita ya kwanza ya 2021 kuwa miezi yenye umwagaji damu zaidi katika miaka 12 iliyopita. Ripoti hiyo pia ilionyesha kwamba wanawake, wavulana na wasichana ndio waathirika wakuu, wakiwa ni nusu ya majeruhi hao.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inalaani umwagaji damu wa kinyama wa Waislamu wasio na hatia wa Afghanistan kwa matamshi makali zaidi na inaviona vita vya sasa kuwa ni kinyume na maadili yote ya Kiislamu na ya kibinadamu ambavyo kwavyo Waislamu wengi wameuwawa kikatili kupitia mashambulizi ya anga yasiyokoma, milipuko na vita vya makabiliano, kwani hata maiti hazijazikwa kwa siku nyingi. Kwa kweli, Sharia ya Kiislamu hairuhusu Muislamu yeyote kuwalenga Waislamu wengine kwa sababu Uislamu unachukulia damu ya Waislamu kuwa ya thamani zaidi kuliko Ka'aba, sembuse jinsi watoto, wanawake na vijana wanavyouwawa kupitia vita hivi vichafu, na kusababisha mamia ya maelfu ya watu kukimbia makaazi yao.

Kwa ujumla, vita nchini Afghanistan vina vipimo vya kieneo na kimataifa. Amerika, kufuatia kushindwa kwake kwa kufedhehesha na kujitoa kutoka Afghanistan, imeiweka nchi hii kati ya mawe mawili ya kusaga: vita vya uahribifu na ajenda ya fazaiko ya amani, ambayo inazidi kuwa ngumu na ngumu kila uchao. Ingawa, Amerika inaonekana kutangaza kuwa ni "Vita vya wenyewe kwa wenyewe" na tatizo la Waafghan wenyewe, uhalisia ni kwamba vita vya sasa ni urithi muovu wa Amerika kwani inataka kuibadilisha kuwa zimwi la kutisha kwa eneo hilo ili kudumisha ushawishi wake wa kieneo chini ya mwavuli wa ugaidi.

Tunatoa wito kwa pande zote mbili zinazopigana kujiuliza kuwa ni lipi dhambi kubwa zaidi kuliko umwagaji damu wa ndugu na dada zenu Waislamu ?! Muogopeni Mwenyezi Mungu (swt) na zuieni Fitna ya sasa kwa kuepuka umwagaji damu wa Waislamu, ambao ni dhambi kubwa na jinai isiyosameheka. Badala yake, tunatoa wito kwa wale ambao lengo lao kuu ni kurudisha utawala wa Uislamu na kutokomeza uvamizi kumakinisha mtazamo juu ya lengo lao la kutokomeza uvamizi na ukoloni wa Kimagharibi ili sio tu ushawishi wa kijeshi wa Amerika na NATO uondolewe lakini pia ushawishi wao wa kijasusi, kisiasa, kifikra na kiuchumi uondolewa katika uso wa ardhi za Kiislamu. Kwa kuongezea, msiruhusu mamlaka za kidhalimu kutumia damu ya vijana wa Kiislamu kama kuni na njia ya kuendeleza ushawishi wao kwa sababu hii itachoma kila mtu na kila kitu!

 [وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَا تُصِیبَنَّ الَّذِینَ ظَلَمُوا مِنْكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ شَدِیدُ الْعِقَابِ]

“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Al-Anfal: 25]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu