Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  21 Sha'aban 1443 Na: Afg. 1443 H / 12
M.  Alhamisi, 24 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu; Shirika lisilo na Ushirikiano Wala Uislamu!

 (Imetafsiriwa)

Mkutano wa 48 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ulifanyika jijini Islamabad Machi 23, 2022 ambapo mawaziri 46 wa mambo ya nje walikuwa wamehudhuria - mkutano huo ulidumu kwa siku 2. Moja ya mada kuu ya mkutano huo ilikuwa Afghanistan. Mbali na hilo, shirika hilo lilifanya mkutano maalum kuhusu Afghanistan jijini Islamabad mnamo Disemba 2021.

Shirika hilo la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) limeeleza wasiwasi wake kuhusiana na hali nchini Afghanistan, limwaga machozi ya mamba; hata hivyo, bado halijaweza kufanya lolote kwa ajili ya Masjid-ul-Aqsa na ardhi ya Palestina, ambayo imekuwa ndiyo falsafa kuu ya kuundwa kwake. Hata hivyo, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1969 hadi sasa, dola hiyo ya Kiyahudi imepanua zaidi maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina. Kashmir ikaingia chini ya uvamizi wa kimabavu wa dola ya Kibaniani. Afghanistan na Iraq zikavamiwa, maelfu wakauawa kikatili nchini Yemen, Syria na Libya, na mamilioni ya Waislamu wa Uighur wakateswa katika kambi za mateso za Wachina; ambapo, OIC, licha ya kuwa shirika la pili kwa ukubwa duniani baada ya Umoja wa Mataifa ambayo wanachama wake ni dola kubwa za kinyuklia na mataifa yaliyoendelea, halijatatua tatizo lolote la ulimwengu wa Kiislamu bali limeendelea tu kufanya mikutano isiyo na maana, kauli zisizo na tija na masuluhisho duni.

Ukweli ni, wanachama wa OIC ni wale wanaozungumzia ukombozi wa ardhi za Kiislamu, lakini zile zinazojiita serikali na watawala wao ndio mabaki ya ukoloni yaliyoko. Kwa mfano, baadhi ya dola za Kiarabu zimesawazisha mahusiano yao na dola ya Kiyahudi huku nyengine chache bado zina dukuduku. Uturuki, ambayo hapo awali ilikuwa kitovu cha Khilafah Uthmani, sio tu kwamba inaunga mkono kwa uwazi ukaliaji wa kimabavu ardhi za Kiislamu na ukandamizaji wa Waislamu lakini pia inamkaribisha kwa dhati raisi wa dola ya Kiyahudi kwenye eneo lake. Pakistan, ambayo katika duru ya sasa ni mwenyeji wa OIC, imeiuza Kashmir kwa faida ya serikali ya India - kama ilivyoiuza Imarati ya Kiislamu kwa Marekani wakati wa muhula wa kwanza na kuendelea kuunga mkono uvamizi wa Afghanistan.

OIC daima imecheza dori kubwa chini ya muundo wa dola kuu. Wakati huu, Marekani inanuia kufikisha ujumbe wake kwa Imarati ya Kiislamu kupitia wanachama wa OIC ambao ni kufuata sera ya 'karoti na fimbo'. Nchi wanachama wa shirika hili wanajitahidi kuifanya Imarati ya Kiislamu ipunguzwe kutoka kuasisi mfumo safi wa Kiislamu ili maadili ya kisekula ya Kimagharibi yaweze kukuzwa kwa mapana. Kama ambavyo katika mkutano uliopita wa OIC, waziri wa mambo ya nje wa Pakistan alisema kuwa Pakistan inawataka Taliban kusikiliza wasiwasi wa jumuiya ya kimataifa kuhusu haki za binadamu za raia wa Afghanistan.

Ni lazima kwa Waislamu wa Afghanistan na viongozi wa Imarati ya Kiislamu kutambua sura halisi ya OIC kwani mashirika kama hayo hayajali lolote kuhusu hatma ya Ummah kwa sababu yanalenga tu kuendeleza mgawanyiko baina ya Ummah kwa kuunda vikwazo vikubwa katika utabikishaji wa Uislamu. Hakuna jema [Khair] linalopaswa kutarajiwa kutoka kwa mashirika kama hayo kwa sababu utashi wao wa kisiasa hauendi zaidi ya maslahi ya Mabwana wao, achilia mbali kutatua tatizo la Afghanistan. Ni muhimu sana kwamba ajenda kama hizo zilizofeli lazima zikataliwe na juhudi zifanywe badala yake kuukomboa Ummah (ambao umechukuliwa kama mateka na dola za kikoloni, watawala wasaliti, dola za kitaifa na mashirika yanayohusiana nazo) kwa kutabikisha Uislamu ndani ya nchi na vile vile kujitahidi kuunganisha Afghanistan, Pakistan na Asia ya Kati zote kwa pamoja.

 [وَمِنَ النَّاسِ مَن يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ]

“Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu.” [Al-Baqara: 204]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu