Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  10 Ramadan 1445 Na: Afg. 1445 H / 12
M.  Jumatano, 20 Machi 2024

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji Kati ya Afghanistan na Pakistan Yanatumikia Sera za Kikanda za Marekani na India
(Imetafsiriwa)

Raia kadhaa wameuawa na kujeruhiwa kufuatia mashambulizi ya anga ya vikosi vya Pakistan katika majimbo ya Paktika na Khost nchini Afghanistan. Kujibu mashambulizi haya, vikosi vya jeshi la Afghanistan vilishambulia maeneo kadhaa ya kijeshi ya Pakistan katika Mstari wa Durand na kuwasababishia hasara. Hali ya mitandao ya kijamii inayohusu nchi zote mbili imekuwa ikitiririsha hisia za kitaifa na ulipizaji kisasi dhidi ya wao kwa wao.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/ Wilayah Afghanistan inalaani mzozo unaoendelea kati ya Waislamu wa pande mbili na kutangaza mambo yafuatayo katika suala hili:

Kwanza, sio tu kwamba inasikitisha lakini pia ni aibu kwamba jeshi lenye nguvu zaidi la ulimwengu wa Kiislamu lililo na silaha za nyuklia linalenga raia, watoto na wanawake nchini Afghanistan chini ya kivuli cha "kukabiliana na ugaidi" katika mwezi mtukufu wa Ramadhan. Wakati katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, umbile la Kiyahudi limekuwa na umwagaji damu, likiwaua Waislamu wa Palestina mbele ya macho ya majenerali wa Pakistan, jeshi la kihaini la Pakistan limekuwa likitazama tu bila ya aibu - bila ya kutoa majibu hata madogo.

Pili, Pakistan ni dola mamluki ya Marekani katika kanda hii. Kinachoifanya serikali ya Pakistan kufanya vitendo hivyo vya uoga ni kwa sababu Marekani inaonekana kuipa Pakistan dori mpya katika eneo hilo. Marekani inataka kuona wanajeshi wa Pakistan wakikabiliana na watu wake wenyewe, Waislamu wa Pakistan wanaoishi katika maeneo ya kikabila kando ya Mstari bandia wa Durand pamoja na Mujahidina wa Afghanistan. Kinaya uchungu ni kwamba Waislamu wanazusha migogoro kati yao huku serikali ya Hindutva ya Modi sio tu inawatesa Waislamu ndani ya India lakini pia inaendelea kukalia kwa mabavu Kashmir bila uoga. Juhudi hizi zote zinafanywa kwa lengo la kuiweka India bila hofu yoyote ya Pakistan ili iweze kutekeleza dori yake kuu chini ya mkakati wa Marekani wa kuidhibiti China. Kwa hiyo, mapigano ya hivi majuzi kati ya pande hizo mbili za Waislamu yanatokana na sera za kikanda za Marekani, zinazotekelezwa na watawala wasaliti wa Pakistan.

Tatu, badala ya kufyatuliana risasi wao kwa wao na kujihusisha na hisia batili za utaifa na/au uzalendo, Mujahidina wa Afghanistan, Mujahidina wa maeneo ya kikabila na watu wanyoofu katika safu ya jeshi la Pakistan lazima wazungushe bunduki zao kwenye mwelekeo sahihi. Katika kipindi hiki kigumu, hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kuwalinda watu wasio na ulinzi wa Palestina na kuikomboa Kashmir inayokaliwa kwa mabavu. Kwa hivyo, kwa ajili ya misheni hii kubwa, ni muhimu kuuondoa Mstari wa Durand wenye saratani na kuunganisha nishati na nguvu zao katika ulinzi wa Masjid Al-Aqsa na Waislamu wa Palestina na Kashmir. Masuala madogo hayapaswi kuwagawanya Waislamu na msukosuko wa sasa usiishie kwa upendeleo wa Marekani na India.

Hivyo basi, isipokuwa ramani ya kisiasa ya eneo hilo ibadilike kutoka katika mfumo wa dola ya kitaifa na kuwa wa Dola ya Khilafah, na mikono ya watawala wasaliti na majenerali ikatiliwe mbali kutokana na hatima ya Ummah, misukosuko ya aina hiyo itaendelea. Kwa hivyo, suluhisho la kimsingi la kukomesha mizozo hiyo haribifu na ya kihistoria ni kuziunganisha Afghanistan, Pakistan na Asia ya Kati chini ya mwavuli wa Khilifah moja kwa njia ya Utume - Khilafah inayounganisha na uwezo wa kifikra, kisiasa, kijeshi na kiuchumi. wa kanda hii na kuwageuza Waislamu kuwa dola kuu yenye nguvu ya ulimwenguni.

[وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلاَ تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ]

“Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu...” [Al-Anfal: 46]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu