Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  15 Rajab 1440 Na: 1440/027
M.  Ijumaa, 22 Machi 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Khilafah Itakomboa Turkestan Mashariki

Na kuwanusuru Uyghur kutoka kwa Ukandamizaji wa Kihalifu wa Uchina

(Imetafsiriwa)

Viongozi wahalifu wa Uchina wamepata nguvu kutokana na majibu dhaifu ya watawala wa Waislamu; ambao wamechagua mikataba ya kifedha kuliko kuwanusuru Waislamu wa Turkestan Mashariki kwa mujibu wa ushahidi wao wa kunyamaza kimya dhidi ya uhalifu wa kupindukia unaoendelezwa na utawala wa Uchina katika majaribio ya kukata tamaa kwao kwa kuwatenga Waislamu na Dini yao, Dini ya Uislamu ambayo imejaa ndani ya vifua vya watu na mapenzi ya tangu mababu zao walioongozwa kwa nuru yake na kuikubali itikadi yake katika karne ya kwanza ya Hijra (uhamiaji).

Huku utawala wa Uchina ukiendelea kuwahangaisha Waislamu wa Uyghur kwa kutumia kila mbinu ya kidhalimu ikiwa ni pamoja na kuwawekea vikwazo wasitekeleze ibada zao na wasihudhurie misikiti kwa kuifunga, kuwalazimisha wasifunge katika mwezi wa baraka wa Ramadhan, na kupiga marufuku ibada aina yoyote ya Kiislamu mpaka hivi majuzi wamezindua kambi kubwa na kuwafunga Waislamu zaidi ya milioni 1 ndani ya kuta zake eti ni kampeni inayodaiwa kulenga "kupambana na ugaidi" kwa kisingizio cha mwito wa: "mafunzo ya kitaaluma" na huku ikiwashika wasomi, wanasayansi, wanafikra na maprofesa wa vyuo. Yote haya ili kueneza wasiwasi na kutia hofu katika mioyo ya Waislamu ili kujisalimisha kwa udhaifu wa ushikamanaji wa Dini yao ya Kiislamu. Jarida la Intelligence limechapisha tangazo la Uchina kwamba Uislamu ni maradhi ya kuambukiza ambayo yanatakiwa kutibiwa kwa njia yoyote hata kama ni kwa njia ya kutesa na kuua. Shirika la Human Rights Watch liliripoti kwamba utawala wa Uchina una walazimisha Waislamu kuritadi kwa kuwatishia kwa mateso ya kiakili na kimwili. Utawala wa Uchina unadai kuwa wamelazimishwa kuchukua hatua hizo ili kupambana na maovu matatu: ugaidi, itikadi kali na mwito wa kujitenga, kama ilivyotiwa na BBC. Ili kupambana na miito hii ya kirongo, utawala wa Uchina umetumia kila mbinu za ukandamizaji.

Wakati utawala wa Uchina ukiendeleza kampeni zote hizi, hawaoni chochote isipokuwa uungwaji mkono kutoka kwa watawala wa Waislamu, ikijumuisha kauli ya Naibu wa Rais wa Indonesia Jusuf Kalla mnamo 17/12/2018 kwamba serikali ya Indonesia haiwezi kuingilia kati katika matatizo ya kindani wanayopitia Waislamu wa Uyghur ndani ya Turkestan Mashariki na kusema kuwa hilo ni suala la ubwana wa Uchina. Hivyo basi, vijidolari vilivyowekezwa na Uchina ndani ya Indonesia, Malaysia, Pakistan na vijimikataba vya kibiashara na Uchina vimewanyamazisha watawala Waislamu ambao wamefeli kutenda kwa mujibu wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu, ambayo yanawaamrisha kuwanusuru Waislamu wa Uyghur walioko Turkestan Mashariki.

Tunahakika kuwa hawa watawala Ruwaybidha (wasaliti) hawawakilishi Ummah wa Kiislamu. Tunawapa onyo watawala wa Uchina kwa hasira za Ummah wa Kiislamu ambao utajibu kwa maamrisho ya Mwenyezi Mungu, na kuzikata nyororo za watawala hawa na kuinuka na kulipiza kisasi  kwa wale waliowakosea na kuwakandamiza ndani ya Turkestan Mashariki, Myanmar, Kashmir, Palestina na ardhi nyingine za Waislamu…

Utawala wa Uchina lazima ujifunze kutoka kwa hatima ya watawala waliowatangulia ambao hawakupata mwanya wa kutorokea kutoka kwa kiongozi shupavu Qutaybah bin Muslim, kiongozi wa majeshi ya Waislamu, kwamba ataingia ardhi ya Uchina. Mfalme wa Uchina akamtumia mawaziri wake na jopo lake. Wakamwambia "Usiingie ardhi yetu. Tutakufurahisha kwa chochote unachotaka… tutalipa chochote unachotaka katika Jizya." Akawaambia: Niliapa kuwa nitaingia ardhi ya Uchina. Wakasema: Tutalipa chochote kitakachoweza kuondosha kiapo chako, hivyo jopo la Mfalme wa Uchina likarudi na kuchukua mchanga kutoka katika ardhi ya Uchina na kumpelekea Qutaybah, akasimama juu yake na kuchukua Jizya kutoka kwao katika hali ya kuwa wamefedheheka.

Waislamu hawatosahau dhuluma wanazopitia na janga hili linalowakumba  hivi sasa ni kama wingu la msimu wa joto. Khilafah Rashidah (Khilafah iliyoongoka) kwa njia ya Utume ambayo itasimama hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu italeta ushindi kwa ndugu zetu waliokandamizwa ndani ya Turkestan Mashariki na itawahesabu wote walio wakandamiza na kuwatenga, Mtume (saw) alisema: «إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Kiongozi ni ngao, nyuma yake mnapigana na kujilinda”

Na wakati huo si Uchina wala mwengine atakayejaribu kuwadhuru Waislamu kwa sababu watajua kuwa chochote watakacho kifanya kitaregeshwa kwao mara dufu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu na Muweza.

Dkt. Osman Bakhach

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu