Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  10 Dhu al-Hijjah 1442 Na: 045 / 1442 H
M.  Jumanne, 20 Julai 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pongezi Kutoka kwa Hizb ut Tahrir kwa Idd Al-Adha Al-Mubarak

Allahu Akbar Allahu Akbar Allahu Akbar La Ilaha Ila Allah Allahu Akbar Allahu Akbar Wa Lilahi Alhamd

(Imetafsiriwa)

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote, Anayeleta bishara njema ya ushindi na tamkini, na Muonyaji kwa Aya Tukufu. Rehma na amani zimshukie yule aliyeturithisha sheria ambayo kwayo nyoyo ziling'aa, akili kuangazwa, na hali kutengea, na kutuwekea Khilafah ambayo kwayo nchi zilipanuka, maisha yalinawirika, na jamii ziliunganishwa kama ndugu… Bwana wetu, Bwana wa viumbe vyote Muhammad na jamaa zake na maswahaba zake.

Furaha ya wale wanaopeana mikono baada ya swala ya Idd, furaha ya watoto katika nyumba za Waislamu, furaha ya waja watiifu na matunda yao ya siku kumi za Dhu al-Hijjah, utolewaji sadaka kwa Al-Aziz Al-Jabbar, na furaha ya kumaliza ibada kwa wale walioweza kufikia njia ya Nyumba Takatifu.

Kongoni kwa Idd Al-Adha… Kongoni kwa furaha ambayo huleta utulivu wa nyoyo… Kongoni kwa bishara ya faraja iliyo karibia...

Katika mnasaba huu uliobarikiwa, ninafuraha kutoa pongezi maalum kutoka kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir, kwa Ummah bora ambayo ilioletwa kwa watu, Ummah wa Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, tukimuomba Mwenyezi Mungu aifanye furaha ya Idd hii iwe ni bishara za karibu na ushindi dhahiri.

Pia natoa pongezi maalum kwa niaba yangu na kwa niaba ya mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wafanyikazi wake wote, kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, tukimuomba Mwenyezi Mungu amwafikie katika kuiongoza dawah na kuomba Nusra (msaada wa kijeshi) kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Enyi Waislamu:

Mwenyezi Mungu amewachagua watu ndani ya mataifa ambao wanaweza kutambua uhalisia wao, wakiwasiliana na hisia zao, na kuelezea hali yao. Wakati wale ambao Mwenyezi Mungu amewajaalia na uwezo huu wanapoongoza njia katika kuwahutubia na kuwashauri watu wao, huziteka nyoyo na akili za watu, na kuwa ndio wanaounda rai jumla kwa watu wao. Kwenye Iddi hii, tutawahutubia wao haswa, kuwakumbusha umuhimu wa dori yao, na kwa Ummah kujua haki yake kwao.

Kwa Waundaji wote wa Rai Jumla katika Umma wa Kiislamu:

Mnayo majukwaa, wavuti, kalamu, kurasa, vituo, magazeti, vipindi na majukwaa ya vyombo vya habari, majukwaa ya Dawah na yasiyo ya Dawah, na aina zote za watengenezaji maalumati kwenye vyombo vya habari, wale miongoni mwenu ambao wamekuuzwa katika mambo ya Uislamu, na wale miongoni mwenu ambao wamekuuzwa juu ya maswala ya maisha na maswala ya watu na ambao hufanya mambo mazito ya kimaisha na hata burudani: Tunawahutubia nyinyi nyote katika Idd hii katika wadhifa wenu kama wale waliokubali jukumu la kushauri, kutoa maoni na kuziongoza hisia za watu Umma wa Kiislamu. Mtume (saw) asema:

«أَيُّمَا دَاعٍ دَعَا إِلَى شَيْءٍ كَانَ مَوْقُوفاً مَعَهُ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ، لَا يُغَادِرُهُ وَلَا يُفَارِقُهُ، وَإِنْ دَعَا رَجُلٌ رَجُلًا. ثُمَّ قَرَأَ: ﴿وَقِفُوهُمْ إِنَّهُمْ مَسْئُولُونَ»

Pindi mtu anapolingania kitu, kitakuwa pamoja naye hadi Siku ya Kiyama, hakitamuacha wala kutengana naye, hata kama mtu atamlingania mtu mwengine. Kisha akasoma: Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa.” [As-Saffat: 24].

Tunauhakika na uhalisia wa mambo matatu kwamba utambuzi jumla na rai jumla ya watu wa Umma wa Kiislamu zimeyafikia:

Uhalisia wa kwanza: ni kwamba Umma umetambua barabara kwa Uislamu ndio njia anayoiridhia Mwenyezi Mungu (swt) kwa maisha ya wanadamu.

Uhalisia wa pili: ni kwamba Umma, baada ya karne moja ya mapambano ya gharama kubwa, umetambua barabara kuwa izza yake ufanisi wake hauna budi zimefungamana na uwepo wa Khilafah ya Kiislamu.

Uhalisia wa tatu: ni kwamba Umma wa Kiislamu una hamu ya kurudi kwa utawala muongofu wa Uislamu kama ilivyokuwa wakati wa Maswahaba watukufu. Bali, uko tayari kupambana na kutoa roho zake na roho za watoto wake kwa ajili ya jambo hili endapo utadiriki na una yakini kuhusu njia ya kupata hilo.

Tunahakika na uhalisia huu kuhusu rai jumla ya sasa ya Umma wa Kiislamu, lakini uhalisia huu hautoshi kudhibiti maendeleo ya Ummah kwenye njia ya wokovu. Badala yake, inahitaji mtu kuusaidia kujua ufafanuzi wa mfumo wa Kiislamu wakati unapokabiliwa na njama na changamoto. Hapa inakuja dori ya waundaji wa rai jumla kutoka kwa wana wa Umma wa Kiislamu. Kuupatia Umma maelezo ya fikra ya Kiislamu. Hapa lazima tutaje mifano inayoonyesha umuhimu na uzito wa jukumu hili.

Mfano wa hili ni wakati muundaji rai - anayependa na kutamani umoja wa Umma wa Kiislamu - anapopuuza wakati uzalendo unapowasilishwa kama fikra ya kisiasa katika nyenzo anazowasilisha kwa hadhira yake, au kwamba anaunga mkono wajibu wa kuheshimu ubwana wa mataifa katika nchi za Kiislamu, kama sheria za kutoa na kunyima uraia na visa za usafiri, kwa Waislamu kutoka nchi zengine na anasahau kuwa fikra ya utaifa na sheria zinazotokana na ubwana wa kitaifa sio chochote ila ni fikra hatari za kisiasa, kusudi lao ni kuigonga fikra ya umoja wa Umma wa Kiislamu. Badala yake, alipaswa kutaja uharamu wa uzalendo na kuonya umma wake juu ya hatari yake. Badala yake, hakupaswa kulegea kujielimisha kwa kina kinachostahili ili kuwasilisha kwa umma wake ufahamu wa utiifu wa kibinadamu kwa watu wa nchi yake na maslahi yao kulingana na njia ya Shariah ya Kiislamu na sio njia ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Mfano mwengine wa uzembe kama huo ni wakati moja ya miji ya nchi za Kiislamu inapoingia chini ya shambulzi la kijeshi, watengenezaji wa maalumati ya vyombo vya habari, kwa ikhlasi yao, wanamshambulia mvamizi na kuonyesha mshikamano na yule anayeshambuliwa, lakini badala ya kuelekeza Ummah katika majibu ya kurudisha shambulizi la kafiri kupitia kuhamasisha majeshi ya Waislamu, badala ya marekebisho haya, wanaizingira rai jumla katika Umma wa Kiislamu kwa kampeni ambazo zinaifedhehi rai jumla huko Magharibi, halafu wanatoa wito kwa nchi za ulimwengu, haswa za makafiri na nchi za wakoloni za Magharibi, kuingilia kati kusitisha vita! Wakati lilikuwa jukumu lao kuhamasisha rai jumla katika Ummah kutambua kwamba ulinzi wa miji ya Waislamu unapaswa kufanywa na majeshi ya Waislamu yaliyowekwa katika kambi zao.

 Enyi Waundaji Rai Jumla katika Umma wa Kiislamu:

Sisi katika Hizb ut Tahrir tunakumbusheni wajibu mlio nao kwa Umma wa Kiislamu kwa kuusaidia kwa kuupatia fikra safi ya Kiislamu. Hizb ut Tahrir inaweka mikononi mwenu maalumati ya kifikra ya kisiasa, yaliyovuliwa kwa njia ya nguvu ya dalili kutoka kwa machimbuko ya sheria ya Kiislamu. Ndani yake, yanawasilisha maoni ya Shariah kuhusu changamoto za kifikra na kisiasa na yanawasilisha masuluhisho ya Shariah kwa maswala ya kisasa yanayoukabili Ummah. Kwa hivyo kuweni waangalifu, Enyi wamiliki wa majukwaa na waundaji wa rai jumla, kuweni waangalifu msiupatie Umma uzoefu wa kisiasa ambao roho zinautamani, ambao utazipotosha nafsi mkapotea na watu wakapotea pamoja nanyi. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ أَلاَ سَاء مَا يَزِرُونَ

“Ili wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanao wapoteza bila ya kujua. Angalia, ni maovu mno hayo wanayo yabeba! [An-Nahl: 25]. 

Allahu Akbar Allahu Akbar Allahu Akbar La Ilaha Ila Allah… Allahu Akbar Allahu Akbar Wa Lilahi Alhamd

Eid Mubarak, Wassalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Mh. Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu