Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  6 Muharram 1444 Na: 1444 H / 001
M.  Alhamisi, 04 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani Inaua Waislamu, Inakiuka Matukufu Yao, na Kupora Nchi Yao Kwa Sababu Waislamu Hawana Mlinzi!
(Imetafsiriwa)

Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza alfajiri ya Jumanne, tarehe 2/8/2022 kwamba wamemuua Dkt. Ayman al-Zawahiri mnamo Jumamosi, 30/7/2022, katika shambulizi la anga lililotekelezwa na droni kwenye makaazi yake jijini Kabul, mji mkuu wa Afghanistan, na kwamba hili lilijiri baada ya kufuatilia mienendo yake tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wakati alipohamia kuishi na familia yake katikati mwa mji mkuu huo wa Afghanistan.

Dkt. Ayman al-Zawahiri alitambua lengo lake kwa kujishindia mmoja ya mema (Husnayain) mawili, wakati alipouawa shahidi mikononi mwa ujasusi wa Marekani, taasisi ya Marekani yenye uadui zaidi dhidi ya Uislamu na Waislamu na hatari zaidi kwao ... Amerika inaua na kuchinja watoto wa Waislamu, inakiuka matukufu yake, na inakiuka ardhi, bahari na anga, haipati mtu yeyote wa kusimama usoni mwake, na hapa tunauliza:

Je, Marekani ingeweza kutekeleza operesheni kama hiyo na kumuua mmoja wa watu wake iliyokuwa inamsaka jijini London, Beijing au Moscow? Jibu ni bila shaka, hapana.

Kwa nini, baada ya kujiondoa kutoka Afghanistan baada ya karibu miaka 20 ya vita, kwa nini Amerika bado inatenda kana kwamba Afghanistan ni eneo la vita linaloendelea?! Jibu ni: Marekani ni nchi ya kikoloni ambayo bado haijashiba kupora mali za nchi za Kiislamu. Ama kuhusu kujitoa kwake katika ardhi zetu, ni kujitoa kwa muda tu hadi kumaliza migogoro yake na China na Urusi, kisha kuregea kukamilisha uporaji wake!

Afghanistan na nchi nyingine za Kiislamu bado ziko chini ya moto wa majeshi ya Amerika kwa sababu hakuna vikosi vilivyopangiliwa ndani yake vinavyoweza kuizuia Amerika. Uko ulinzi wa anga ili kuweka marufuku kwa ndege za Marekani kupaa juu ya anga ya Afghanistan? Na ziko wapi huduma za kijasusi, ili kuyatoboa macho majasusi huko Kabul na maeneo mengine?

Wokovu wa Afghanistan na watu wake kutokana na mitego ya kisaliti ya Kiamareka bado haujapatikana. Watu wa Afghanistan bado hawajapata usalama kutokana na madhara na ulafi wa Magharibi. Wokovu na usalama hautapatikana isipokuwa Waislamu wawe na dola ya Khilafah itakayoifanya Marekani na wafuasi wake kusahau minong'ono ya Shetani, mithili alivyofanya Abu Bakr As-Siddiq, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alipojibu uvumi wa Warumi, na kuwafanya kuwa historia.

Waislamu wa Asia ya Kati na Kusini ya Kati wana kiu ya siku ya kuregea Khilafah ambayo itakuwa kitovu chao cha madaraka, ambayo nyoyo zao zitaipenda, hivyo watapanua uwezo na uwezo wao, maisha, fedha na watu ndani yake. kwake. Mwenyezi Mungu (swt) ameitayarisha Afghanistan na Pakistan na maeneo ya pambizoni mwao kwa ajili ya jambo hili, na kuzibariki kwa fadhila na nafasi nzuri ya kisiasa ya kijiografia, na akawabariki watu wao kwa mapenzi imara ya Uislamu.

Ama Magharibi mkoloni kafiri, inayoongozwa na Amerika, bado ingali inaingia kwenye handaki la mifarakano ya kijamii, ikitangaza kuzuka kwa migogoro ya ndani. Imefika mahali vyama vya Marekani vimeanza kuleta watu wenye uwezo wa kutiliwa shaka madarakani; kuanzia kwa Trump, ambaye alizidisha kupagawa na uadui wa kihalifu katika sehemu ya msingi wa Chama cha Republican, hadi Biden, ambaye walimchagua licha ya kujua kwamba alikuwa akionyesha dalili za shida ya kiakili ...

Ulengaji muda wa mauaji haya ya rais wa Marekani kuwa hivi sasa, yaani, miezi michache kabla ya uchaguzi wa bunge la Congress, ni dalili ya kiwango cha mkanganyiko na hofu ya chama cha Democratic kupoteza madaraka. Kwa hivyo, wanasiasa nchini Amerika wanaiburuza nchi katika mpasuko wa kijamii ambao umekuwa mgumu kuepukika.

Kwa kumalizia, tunatoa wito kwa Waislamu nchini Afghanistan na Pakistan kuweka mikono yao mikononi mwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itawapa kitovu cha madaraka, kuunganisha Asia ya Kati na Kusini ya kati, kuanza ukurasa mpya wa izza katika historia ya Umma wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu asema:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ)

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].

 Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu