Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  12 Jumada II 1440 Na: 1440/017
M.  Jumapili, 17 Februari 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ndoa Haramu ya Jijini Warsaw
(Imetafsiriwa)

 Hivyo basi kama ilivyo jinsi watawala wa Kiarabu walivyo ondoa sitara ya mwisho ya nyusoni mwao katika kupanga njama dhidi ya Uislamu na dhidi ya Qibla cha kwanza cha Waislamu na mahali Mtume (saw) alikofanya safari ya usiku ya Isra (Masra). Ndivyo jinsi mwito maarufu wa “Hapana Khartoum” (bila amani, hakuna utambuzi, hakuna majadaliano), ulioanzishwa na watawala wa Kiarabu katika Kongamano la Khartoum mnamo 1967, ulivyo yeyuka.  Wamefikia nukta ya kuwa mashahidi wa “ndoa ya Warsaw” kwa mujibu wa maneno ya mara kwa mara ya Waziri wa Kigeni wa Qatar na aliyekuwa Waziri Mkuu Hamad bin Jassem, katika nukuu zake katika mtandao wa Twitter: “Mimi sipingi kuishi kwa amani au kuanzisha uhusiano na “Israel”, lakini uhusiano huo ni lazima uwe wa sawa kwa sawa na sio kwa gharama ya haki za Wapalestina.”

Ndoa hii “haramu”, ambayo kupitia kwake Amerika inataka kugeuza ukurasa wa kiburi cha watawala wa Kiarabu, ambao, hadi kongamano la mwisho lililofanyika katika jiji la mashariki la Dhahran mnamo Aprili 15, 2018, waliwapotosha watu wao kwa kudai kuwa wachungaji wa “utambuzi batili na haramu wa Amerika wa Jerusalem kama mji mkuu wa ‘Israel’”, pamoja na usisitizaji wao kuwa Palestina isalie sababu kuu ya taifa la Kiarabu. Pia ilifikia hadi waziri wa kigeni wa Yemen kukaa karibu na Netanyahu, waziri mkuu wa umbile la Kiyahudi, na kumpa kipaza sauti baada ya kipaza sauti cha mhalifu huyo muovu kupata hitilafu, ili sauti yake iweze kusikika katika sherehe ya ndoa hiyo haramu, ambayo Amerika, kinara wa ukafiri, imeiandaa.

Katika hotuba yake ya kongamano hilo, Makamu wa Raisi wa Amerika Mike Pence alianzisha shambulizi kali juu ya Iran, akisema kuwa washiriki wote katika kongamano hilo waliafikiana kuwa tishio kubwa katika Mashariki ya Kati ni Iran, akiita kuwa mfadhili wa “ugaidi” eneo hilo. Ama Waziri wa Kigeni wa Amerika Pompeo, alitoa wito kwa kile alichokiita enzi mpya ya ushirikiano katika kupambana na changamoto katika Mashariki ya Kati na kusema hakuna nchi itakayo salia kati na kati.

Iran, upande wake, haijawacha unafiki wake na kuifanyia biashara kadhia ya Palestina; kwa kutoa hotuba tupu ya “sherehe” hiyo katika Ijumaa ya mwisho ya kila Ramadhan, na Waziri wa Kigeni wa Iran Javad Zarif, kusisitiza katika mahojiano na jarida la Kifaransa la ‘Le Point’ mnamo Disemba 2018, kuwa nchi yake kamwe haikusema kuwa italifuta umbile la Kiyahudi katika ramani, akiuliza swali: “Ni lini tulitangaza kuwa tutaiangamiza “Israel”? Nionyesheni afisa yeyote wa Iran aliyesema hivyo. Hakuna yeyote aliyewahi kusema hivi.”

Kati ya Siku ya Al-Quds ya Ramadhan upande mmoja, na kukana kwa Zarif kuhusu kujitolea kwa Iran kuliangamiza umbile la Kiyahudi upande mwengine, watawala hao wa Tehran hawakujizuia kuchochea moto wa mauwaji na uharibifu nchini Iraq, Syria na Yemen, na kuchochea Fitna ya vita vya “Sunni-Shia”, ambavyo Amerika leo inavitumia kama udhuru wa kuhalalisha mwito wake ili kuibariki “ndoa hiyo haramu” kati ya watawala wa Kiarabu na watawala wa Kiyahudi chini ya guo la kukabiliana na tishio la Iran; waziri wa kigeni wa Bahrain, Khalid bin Ahmed Al Khalifa, alisema katika video iliyo tumwa katika mtandao wa YouTube na waziri mkuu wa umbile la Kiyahudi katika idhaa yake ya YouTube, katika mkutano uliohudhuriwa na mwenzake wa Imarati Abdullah bin Zayed na Waziri wa Kigeni wa Saudia Adel al-Jubeir, “Tumekulia tukizungumzia kuhusu mzozo wa Palestina na Israel kama kadhia muhimo zaidi.  Lakini kisha katika hatua ya mbeleni, tumeona changamoto kubwa zaidi. Tumeona kadhia yenye sumu zaidi, hakika yenye sumu zaidi katika historia yetu ya hivi karibuni, ambayo imekuja kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.” (Shirika la Anatolia) 

Enyi Waislamu:

Tayari mushajua khiyana ya watawala wenu kwenu, na njama zao dhidi yenu, na unafiki wao katika kuchumbiana na maadui zenu, na kufanya biashara na ardhi iliyo barikiwa na Mola wa walimwengu aliye juu ya mbingu saba, ili kuficha makosa yao, kupata msaada wa baadhi ya wale ambao hawatashiriki katika baraka za kunyanyua bendera ya Uislamu, na haraka yao ya kuwashambulia wale wote wanaolingania kushikamana imara katika kamba ya Allah na utekelezaji Shari’ah yake, Imam At-Tirmidhi ameripoti kuwa Hudhaifah (ra) ameripoti:

Mtume (saw) amesema,

«والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَتَأْمُرُنَّ بالْمَعْرُوفِ، ولَتَنْهَوُنَّ عَنِ المُنْكَرِ، أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللَّه أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَاباً مِنْهُ، ثُمَّ تَدْعُونَهُ فَلا يُسْتَجابُ لَكُمْ»

“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, hamtaacha kuamrishana mema, wala hamtaacha kukatazana maovu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atakaribia kuwateremshia adhabu juu yenu kutoka kwake. Kisha mtamuomba wala hamtajibiwa.”

Hivyo basi pingeni ili rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu, ili mupate kujiweka huru, kupitia kuzungumza dhidi ya watawala wale ambao wamemkhini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wamewakhini nyinyi, zuieni makosa yao, kwani hakuna kheri katika maisha ya kumuasi Mwenyezi Mungu.

Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu (swt) atatimiza ahadi yake ya kuitwahirisha Ardhi Tukufu ya Palestina kutokana na najisi ya Mayahudi, pamoja na watumwa wao watawala makhaini na wale walio wepesi katika kuhalalisha khiyana zao katika wanazuoni waovu na wanasiasa wanafiki …

(وَقَضَيْنَا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ فِي الْكِتَابِ لَتُفْسِدُنَّ فِي الْأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوّاً كَبِيراً)

“Na tukawahukumia Wana wa Israili katika Kitabu kwamba: Hakika nyinyi mtafanya ufisadi katika dunia mara mbili, na kwa yakini mtapanda kiburi, kiburi kikubwa!”  [Al-Isr a’:4]

... (فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيراً)

“Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.” [Al-Isra’:7]

Kwa hivyo fanyeni kazi na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume; ambayo itawafanya Mayahudi kuisahau minong’ono ya Shetani, pamoja na viongozi wa Kimagharibi, wanaowapa nguvu kwa uhalifu wao. Na asaa iwe karibu. 

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu