Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  13 Sha'aban 1440 Na: 1440/029
M.  Ijumaa, 19 Aprili 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Kwa Watu Wetu wa Sudan na Algeria

Tangazeni kuwa: Ni Kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, sio Mashariki au Magharibi, bali ni kwa Serikali ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Hakuna tofauti baina ya mzozo ulioko Sudan na Algeria. Matukio yote yanafanana na yale yaliyotokea Misri kwa namna ambavyo maafisa wakijeshi wachache walivyokuwa makini kusimamisha nguzo za utawala utakao wawezesha kudhibiti shingo za nchi na watu wake. Wanafanya kama ambaye ni abiria walioko ndani ya meli ambayo inakaribia kuzama na hawaoni madhara wakidondosha baadhi ya uzito ili kupunguza mzigo wa viongozi walio na sura za kutisha. Chini ya utawala uliopita (ambao wao ni nguzo zake), maafisa hawa walipora utajiri na kudhibiti watu huku wakimakinisha nguvu zote za mabwana zao kutoka Magharibi ili kupora utajiri wa nchi na wakati huo huo wakiweka vikwazo dhidi ya kurudi kwa Shari'ah ili kuondosha masanamu ya Sykes-Picot.

Naam, kazi ya huduma ya usalama ni kumakinisha usalama wa taifa na watu na kuwafurusha maadui wa Dini na nidhamu yetu, na jukumu la jeshi ni kutekeleza jihadi ambacho ndio kilele cha nundu ya Uislamu.

Kujihusisha kwao na mipango ya nidhamu ya kisiasa sio jukumu lao, na hawana haki ya kudhibiti eti hali ya mpito, ambayo tumeshuhudia matokeo ya kutisha ndani ya Misri kutoka kwa wanajeshi wenzao. Yote hayo yanatokea mbele ya macho, masikio na uungwaji mkono wa Amerika na muongozo wake. Amerika haikuona tatizo lolote la kumpindua Mohammad Morsi kwa kuunga mkono mapinduzi yaliyo fanywa na kibaraka wake Sisi licha ya vilio vyote na kupigania demokrasia. Amerika ili nyamaza juu ya mauaji ya kutisha yaliyo fanywa na kibaraka wake Bashar ndani ya Syria.

Hivyo basi, imekuwa wazi kwa Waislamu wote kuwa uchungu wao ni mmoja kwa kupitia kwa kutawaliwa na watawala majangili ambao matokeo yake ni fungamano la kuwategemea na kuwa watumwa kwa wakoloni makafiri Wamagharibi. Pia imekuwa wazi kwa Waislamu kuwa tumaini lao ni moja nalo ni kukata minyororo hii. Wale ambao wanafanya kazi ya kukazanisha minyororo hii ni viongozi wa Wamagharibi ambao wako makini kuhakikisha kuwa umoja wa Ummah haupatikani na kwamba hauwezi kuishi kwa mujibu wa sheria za Muumba wao, ili waweze kurudi kama awali kuwa ni Ummah bora kwa wanadamu.

Hivyo basi, tunawasisitiza watu wetu na ndugu zetu wanao andamana ndani ya Algeria na Sudan kwamba lazima warudie mafunzo ya awali, wafahamu waqi'ah unaohusiana na mzozo waliomo na wajue nani rafiki na nani adui. Lazima wasikubali kufanywa wapuzi kwa kupewa ahadi tupu kutoka kwa kundi la wanajeshi, ima ndani ya Algeria au Sudan ambao wanafanya kazi kufikia katika mchoro wa Misri. Ummah umeungana katika mapambano ya kuvunja minyororo ya utegemezi wa Makafiri Wamagharibi na umeamua kunali radhi za Muumba wao.

Twasema kwa kinywa kipana; hakuna uhalali wowote kwa kundi lolote liwe litakavyo jiita na kutabbani kinyume na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya kazi kuvuruga Sheria Zake. Hakuna uhalali kwa yeyote anayerudia sanamu la Sykes-Picot kama marudio yake, bali marudio ya Ummah ni kwa sheria za Muumba wao zinazotokana na mfumo wa Mwenyezi Mungu mmoja kwa shahada ya: "Hapana Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu." Ujumbe huu wa Kiislamu ambao uliwahamisha Waarabu kutoka katika enzi ya ujinga hadi katika hali ya kuwa Ummah bora kwa wanadamu na waliweza kueneza Uislamu mabara yote kwa miongo kadhaa, baada ya kuziangusha falme za Fursi na Rome na majeshi yake kufika hata Uchina.

Enyi Watu wetu wa Sudan na Algeria:

Musifanywe wapuzi na yeyote ambaye hajifungi na Uislamu, ambao Mwenyezi Mungu ametupa utukufu kupitia ujumbe wake: ujumbe wa haki, uwongofu na rehema kwa walimwengu sio tu kwa Waislamu pekee. Kuweni macho dhidi ya njia zenye kuhadaa ambazo zinatumiwa na kundi la wanajeshi pamoja na wafuasi wao ambao ni wanasiasa waliopotoka na nyuma yao ni huduma za kijasusi za Kimagharibi; na hakikisheni kuwa hawana dori yoyote kwa kuwa hawana uhalali na haki yoyote ya kufanya hivyo. Jeshi na vikosi vya usalama lazima vitekeleze jumuku walilopewa nalo ni kuulinda Ummah na kuuwezesha kutawala kwa mujibu wa sheria za Muumba wao. Na tangazeni kwa sauti: Ni Kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, sio Mashariki au Magharibi, bali ni kwa Serikali ya Khilafah kwa njia ya Utume.

Munaweza kushinda kwa utukufu wa kupata ushindi mkubwa kupitia mikono yenu:

يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ * هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿

“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila atimize Nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia. Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [ At-Tawba: 32-33]

Na ichukuweni kauli ya Mtume (saw) kwa ammi yake kuwa ndiyo msukumo wenu:

«يَا عَمُّ، وَاَللَّهِ لَوْ وَضَعُوا الشَّمْسَ فِي يَمِينِي، وَالْقَمَرَ فِي يَسَارِي عَلَى أَنْ أَتْرُكَ هَذَا الْأَمْرَ حَتَّى يُظْهِرَهُ اللَّهُ، أَوْ أَهْلِكَ فِيهِ، مَا تَرَكْتُهُ»

"Ewe ammi yangu! Kwa jina la Mwenyezi Mungu lau wataweka jua katika mkono wangu wa kulia na mwezi katika mkono wangu wa kushoto kwa sharti kwamba niwachane na njia hii, ima ni mpaka Mwenyezi mungu anipe ushindi au Nife nikiwa nimo ndani ya njia hii sitoiwacha."

Mnusuruni Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu atawanusuru na fanyeni kazi na wafanyikazi wa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, ni ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara ya Mtume Wake (saw):

«... ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha kutakuweko na Khilafah kwa njia ya Utume."

 

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu