Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  27 Jumada I 1439 Na: 1439/011
M.  Jumanne, 13 Februari 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 

  ﴾مثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا﴿

“Mfano wa waliobebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni kama mfano wa punda anaye beba vitabu vikubwa vikubwa.”

(Imetafsiriwa)

 

Kwa wepesi, swali ni: Je, majeshi, wanamgambo na mashirika yanapigania nini, kuanzia Syria mpaka Yemen mpaka Libya, Misri na Iraq? Nani anamuua nani na kwa nini? Ni dhahiri kuwa, majeshi ya nchi za kikafiri Amerika na washirika wake na Urusi hazijali kuuliwa kwa Waislamu na hazisiti kueneza uharibifu kila wanakoingia pasi na kuzingatia utu wala maadili. Lakini kisicho dhahiri, kisicho halali, na kisicho eleweka ni mauwaji yanayo fanywa na majeshi ya Waislamu nchini Yemen, Iraq, Syria, Misri na Uturuki kwa kutii maamrisho ya watawala ambao, nao pia, hutekeleza maagizo ya mabwana zao wakoloni wa kimagharibi.    

Wanamgambo wa Kikurdi wanapigana nchini Syria na Iraq kuasisi jimbo la Kikurdi, walio na ruwaza ya kulazimisha kuwepo kwa umbile huru la kitaifa katika ramani ya eneo hilo iliyo chorwa na ukoloni wa Kiingereza juu ya magofu ya dola ya Khilafah, na wala hawajali kwa ajili ya hili kuungana na shetani, awe Uingereza, Amerika au umbile la Kiyahudi! Ingawa watangulizi wao wameandika kurasa za mashindano katika kulishinda shambulizi la kimsalaba, zilizo andikwa kwa wino wa Nuru. Kwa upande mwengine, Erdogan anadai kuwa ili kuhifadhi usalama wa kitaifa wa Uturuki, jeshi la Uturuki ni lazima limwage damu ya Waislamu katika maeneo ya Kikurdi ya Kaskazini mwa Syria na Iraq, huku tukijua kwamba mababu wa jeshi hili tukufu walibeba bendera ya Jihad kwa karne nyingi ili kuenua neno la Allah mpaka wakaizingira Vienna mara mbili.

Wanamgambo nchini Yemen wanapigana wenyewe kwa wenyewe ili kuwa na udhibiti wa utawala na serikali, pasi na kujali kuhusu utukufu wa damu ya Waislamu. Wanasaidiwa katika hili na watawala wahalifu waovu nchini Iran na ule unaoitwa muungano wa Waarabu ukiongozwa na Ufalme wa Al Saud, kila mmoja wao akimwaga mafuta juu ya moto wa mapigano na kuongeza usaidizi zaidi wa kisilaha kwa vita hivi vya kihalifu vilivyo igeuza Yemen iliyokuwa na furaha, ambayo Mtume wa Allah (saw) aliwasifu watu wake kuwa wenye hikma na Iman, kuwa tanuri la uharibifu na maangamivu.

Nchini Misri, mtawala wake muhalifu hawatupi tu maelfu ya Waislamu gerezani na kuwadhulumu, bali pia analisukuma jeshi la Misri, ambalo watangulizi wake walivunja wimbi katili la Matartari katika vita vitukufu vya Ain Jalut, analisukuma kufanya oparesheni ya mauwaji na uharibifu eneo la Sinai, akiahidi kuhifadhi usalama wa Mayahudi na kutabikisha maagizo ya Washington, badala ya kuikomboa ardhi ya Isra na Mi'raj kutokana na uharibifu wa Mayahudi, na kuzitwahirisha biladi za Waislamu kutokana na majeshi ya kimsalaba yanayo eneza ufisadi ndani yake.  

Nchini Syria, Iran na washirika wake miongoni mwa wanamgambo inaowafadhili wanashindana na majeshi ya uvamizi ya Urusi katika kumwaga damu ya Waislamu, chini ya miito ya kirongo ambayo Imam Al-Hussein (ra) anajiweka mbali nayo.

Enyi Waislamu!

Allah Ta'ala, Mkweli, amewajibisha juu yenu kuunganisha kalima yenu na kuharamisha kuzozana kati yenu,

(وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ)

"Na mtiini Allah na Mtume wake wala musizozane mukaingiwa uoga, na zikapotea nguvu zenu…"  [Al-Anfal: 46].

Na kuharamisha umwagaji damu pasi na haki, kama ilivyo elezwa katika Hadith Sahih:

«لاَ تَرْجِعُوا بَعْدي كُفَّارًا يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقابَ بَعْضٍ»

“Musirudi baada yangu (yaani kufa kwangu) mukawa tena makafiri, munakatana shingo baadhi yenu nyinyi kwa nyinyi".

Yeye (saw) ameharamisha Waislamu kuwafanya makafiri washirika na wasaidizi wao na kutafuta ushindi kutokana nao, sembuse kuwasaidia katika kuwauwa Waislamu; imeelezwa katika Hadith Sahih kwamba Mtume (saw) amesema, akiihutubia Kaaba:

«وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لَحُرْمَةُ الْمُؤْمِنِ أَعْظَمُ عِنْدَ اللهِ حُرْمَةً مِنْكِ»

"Naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad imo mikononi mwake, utukufu wa muumini mbele ya Allah ni mkubwa zaidi kuliko utukufu wako (Kaaba)"

Hivyo basi, ni nini kilicho wasibu, kwa nini munawanyamazia kimya watawala wanaotekeleza uhaini wa wazi usiku na mchana, kuwafanya marafiki makafiri na kuongeza kasi katika umwagaji damu na uharibifu wa biladi na kuzuia hukmu ya Allah, huku Sharia ikiwahitaji nyinyi kuwazuia mikono yao na uhalifu wao?

Jukumu hili ni msingi juu ya watu wenye kumiliki nguvu na msemo miongoni mwenu, watakaoweza kuwazuia kutokana na batili kwa kuwabadilisha, na kwa wanazuoni, warathi wa mitume, kupitia kulingania neno la haki mbele ya nyuso za madhalimu hawa wasiozingatia ahadi wala hadhi yoyote ya muumini.

Allah ametuonya kutokana na kutumbukia katika yale ambayo wana wa Israel walitumbukia ndani yake, kwa Yeye (swt) kuwafananisha na:

(مثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا)

“Mfano wa waliobebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni kama mfano wa punda anaye beba vitabu vikubwa vikubwa.”          [Al-Jumu’a: 5]

Hii ni baada yao wao kupuuza ulinganizi wa sharia Yake, kuifanya maregeleo na kueneza uadilifu wake, bali waliificha na kukosa kuibeba. Ndiposa, akawafananisha na punda anaye beba vitabu na wala hafaidiki kutokana navyo; kwa kuwa hawezi kudiriki yaliyomo ndani ya vitabu hivyo, na kwa hivyo hafaidiki na uongofu uliomo ndani yake; Allah anatupigia mfano wa waliokuwa kabla yetu ili kuzingatia na kubeba yale aliyoyateremsha Allah kwetu, na yale ambayo Yeye Ta'ala ametufadhilisha kwayo. Ni sharti tutahadhari kutotumbukia ndani ya fedheha hii, na tuchukue jukumu hili kwa kujitolea kwa hali ya juu, vyenginevyo tutakuwa tunazikataa Aya za Allah, Ta'ala, Mwenye hekima. Hivyo basi, Yeye (swt) anatamatisha Aya hii kwa kusema:

(بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّهِ وَاللَّهُ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ)

 “Mfano muovu mno wa watu waliokadhibisha Aya za Allah, na Allah hawaongoi watu madhalimu.”  [Al-Jumu’a: 5].

Kwa hivyo, itikieni wito wa Allah anapo kuiteni katika yale yatakayo kupeni mwamko, kateni hatamu za watawala hawa wanaoshirikiana na maadui wa Allah, dini na mfumo (wa Kiislamu), na fanyeni kazi na wanaofanya kazi kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume:  

  يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ﴿

“Enyi mulio amini, muitikieni Allah na Mtume anapo kuitieni jambo lenye kukupeni uhai wa milele.”  [Al-Anfal: 24].

 

Dkt. Osman Bakhach

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu