Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  2 Ramadan 1439 Na: 1439/025
M.  Ijumaa, 18 Mei 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kupinga Urongo wa Mwandishi Majid al-Khatib
Da’wah ya Hizb ut Tahrir ni Safi Haichafuki Kutokana na Kelele za Porojo
(Imetafsiriwa)

 Katika Makala yaliyochapishwa na gazeti al-Asharq al-Awsat (Toleo 14144, Jumatano, Mei 16, 2018), chini ya anwani “Shambulizi la kigaidi la kisu la hivi majuzi jijini Paris lathibitisha hofu ya Wajerumani dhidi ya misimamo mikali ya Wachechen”, mwandishi wake Majid al-Khatib alidai kuwa kuna “kufanana kuliko wazi” kati ya ugaidi wa Kiislamu na ugaidi hatari wa mrengo wa kulia wenye msimamo mkali. Ingawa Makala hayo yaliandikwa dhidi ya mandhari ya shambulizi la kisu la hivi majuzi jijini Paris na hofu ya idara za Ujerumani ya operesheni zilizofanywa na Wachechen wenye misimamo mikali nchini Ujerumani na Ulaya, mwandishi huyu hakutaka isipokuwa kujaza makala haya madai ya tuhuma na hata kujumuisha uzushi wa wazi pindi alipoihusisha Hizb ut Tahrir na vyama vya vuguvugu la Nazi nchini Ujerumani. Alidai kuwa wachunguzi wa Ujerumani wameona “ushirikiano kati ya Hizb ut Tahrir iliyopigwa marufuku nchini Ujerumani, iliyoko jijini Berlin, na Chama cha Kitaifa cha Kidemokrasia cha Ujerumani (NPD).” Upande wa mashtaka ulizungumza kuhusu warsha ya pamoja iliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Berlin baina ya vyama viwili hivi, ikiangazia juu ya vita vya kuikomboa Kuwait”.

Ni wazi kuwa mwandishi huyu alichapisha hoja hizi kimakusudi, kwani kila mmoja anajua kuwa Hizb ut Tahrir, ambayo inajifakhiri kubeba Dawah ya kurudisha maisha kamili ya Kiislamu, kamwe haihusiki na matendo ya kisilaha licha ya madhila yote na kampeni dhalimu ambazo wanachama wake wamepitia na wanaendelea kupitia chini ya mikono ya serikali za kidhalimu katika biladi za Waislamu. Kila mmoja anajua kuwa njia ya Hizb katika Dawah imejengwa juu ya mvutano wa kifikra na wa kisiasa, na inapinga wazi wazi matumizi ya amali za kimada (ghasia). Na mtafiti yeyote aliye na chembe ya uadilifu hangeweza kuukosa ukweli huu. Kutokana na haya tunapata kuwa mwandishi huyu kuijumuisha Hizb katika muktadha wa makala yake maovu juu ya madai ya ugaidi wa Kiislamu na hatari ya ugaidi wa mrengo wa kulia yote hayana msingi wala hakuna udhuru kwa mwandishi huyu kudai kutojua, pamoja na kukashifu kwake kuwepo na “ushirikiano” baina ya Hizb ut Tahrir na “Chama cha Kitaifa cha Kidemokrasia cha Ujerumani”.  

Ama kuhusu yale aliyotegemea mwandishi huyu kujengea hoja kuhusisha kwake kipuzi “warsha ya pamoja iliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Berlin kati ya vyama viwili hivi vikiangazia vita vya kuikomboa Kuwait” hii kamwe haikuwa warsha ya pamoja, bali ulikuwa ni muhadhara uliofanywa na Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir kwa nchi zinazozungumza Kijerumani mnamo Oktoba 2002 kufichua mipango ya Amerika kutayarisha uvamizi wa Iraq (ambao ulifanywa mnamo 2003), na wala sio kuikomboa Kuwait, kama alivyosema mtafiti. Muhadhara ulikuwa wazi kwa watu wote, na baadaye iligunduliwa kuwa Udo Voigt, kinara wa Chama cha Kitaifa cha Kidemokrasia cha Ujerumani pamoja na mshauri wake Horst Mahler, walihudhuria muhadhara huo. Hivyo basi, vipi itaeleweka kuwa kuhudhuria kwao muhadhara wazi kwa watu wote ni kuwepo kwa madai ya ushirikiano!     

Makala hayo yalishughulikia kwa kina hatari ya hofu ya idara za Ujerumani kutoka kwa Wachechen ambao tayari walikuwa wamepata mafunzo ya kisilaha, upiganaji na kadhalika. Muktadha huu hauhalalishi kwa vyovyote kuihusisha Hizb ut Tahrir, chama cha kisiasa kinachojulikana vizuri na cha jadi, katika muktadha huu, isipokuwa kuna dhamira mbaya kutoka kwa mwandishi.  

Ama kuhusu sisi katika Hizb ut Tahrir, tunaendelea na ulinganizi wetu huku tukiwa tumejitolea imara katika njia ya Mtume (saw). Hatutatishika na kelele za porojo au wafuasi wa mamluki au ujanja wa maadui. Na Allah ni Mwenye kuinusuru Dini yake hata kama makafiri wanachukia hilo, na hata kama wanafiki wanachukia hilo.

  

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu