Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  18 Sha'aban 1444 Na: 1444 H / 031
M.  Ijumaa, 10 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uzinduzi wa Tovuti ya Kifaransa ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kutangaza kuzinduliwa kwa tovuti yake kwa lugha ya Kifaransa, ambayo itatumika kama tovuti ya watu wanaozungumza Kifaransa kutazama maudhui ya habari yanayoangazia juhudi zilizofanywa katika mradi wa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Uzinduzi huu wenye baraka Insha’Allah ni matunda ya juhudi zisizokoma zinazofanywa na Hizb ut Tahrir na wanachama wake kuongeza mawasiliano na watu ili kuwafikia watu/ wafuasi wengi wa Ummah wa Kiislamu kadiri inavyowezekana, popote walipo.

Mradi wa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume unasonga mbele kwa uthabiti na ukali zaidi.

Kuanguka kwa Khilafah na fahari iliyokuwa nayo kwa Ummah mzima wa Kiislamu kunaombolezwa, huku umuhimu wa kuuelewa vyema Uislamu na mfumo wake wa utawala unazidi kuwa na hamu miongoni mwa vijana wa Ummah.

Hapa inakuja dori ya taswira ya vyombo vya habari, ambayo inafikisha ujumbe wa Uislamu kama kadhia nyeti, lazima ipate ufahamu wa kufahamu mambo mahususi ya mfumo wa Kiislamu, nini maana ya kusimamisha tena Khilafah, na jinsi njia ya Utume inavyotumika kuisimamisha na kuitawala.

Kwa sababu hii, tunawataka wanahabari wote wa kweli katika harakati zao za kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume, hususan wanahabari wanaozungumza Kifaransa, kuhakiki nyenzo zilizowekwa kwenye tovuti ya lugha ya Kifaransa ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir. Tukimuomba Mwenyezi Mungu awape ilham bora ya mambo yao na avue kutokana nayo yale yanayokamilisha kazi kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah.

Tunazindua tovuti ya lugha ya Kifaransa ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa baraka za Mwenyezi Mungu na tunamuomba atuongoze kwa kile Anachokipenda na anachofurahishwa nacho.

Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيداً عَلَيْهِم مِّنْ أَنفُسِهِمْ وَجِئْنَا بِكَ شَهِيداً عَلَى هَؤُلاء وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَاناً لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَى لِلْمُسْلِمِينَ)

“Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu,na rehema, na bishara kwa Waislamu.” [An-Nahl: 89].

Link ya Tovuti: https://www.hizb-ut-tahrir.info/fr/

Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu