Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  11 Rajab 1444 Na: 1444 H / 027
M.  Alhamisi, 02 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kati ya Kuwakandamiza Waislamu na Kuwatishia wa Mabaniani kwa Waislamu, Serikali ya Modi inaandaa Kampeni yake ya Uchaguzi Ujao
(Imetafsiriwa)

Hii hapa serikali kichaa maarufu ya Modi, ikihofia hatima yake katika uchaguzi ujao. Inaregea, kwa mara nyengine tena, sera za kukuuza hisia za tashwishi na hofu, miongoni mwa matabaka ya jamii, ikijionyesha kama mwokozi wa wapiga kura wake. Kuanzia tarehe 20 hadi 22 Januari, kwa muda wa siku tatu, Kongamano la 57 la Wakurugenzi Wakuu/Mainspekta Jenerali wa Polisi lilifanyika. Waziri Mkuu Narendra Modi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Muungano Amit Shah, Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Ajit Doval, na takriban maafisa 350 wakuu wa polisi nchini walihudhuria. Hotuba nyingi ziliwasilishwa kuhusu changamoto za usalama wa nchi, ikiwa ni pamoja na kile walichokiita kwa uzushi "Misimamo mikali, hasa ya vijana wa Kiislamu." Ilizingatiwa kuwa moja ya changamoto kuu kwa usalama wa taifa. Miongoni mwa mashirika yaliyoainishwa kuwa yenye itikadi kali, yenye misimamo mikali na yenye ghasia ni Hizb ut Tahrir. Nyaraka zilizowasilishwa zilionyesha haja ya mbinu nyingi za kushughulikia mashirika haya, ikijumuisha ufuatiliaji wa shughuli za siri na kuunda hifadhidata. Nyaraka hizo zilidai kwamba kuongezeka kwa siasa kali nchini India kimsingi kulitokana na kiwango cha juu cha mafundisho ya kidini, na kupatikana kwa urahisi kwa njia za kisasa za mawasiliano.

Kwa hivyo, inadhihirika wazi kwamba serikali ya Modi, na afisa wa usalama aliyeandaa waraka huo wa uzushi dhidi ya Waislamu, wanakusudia kuishughulisha rai jumla, na huduma za usalama nchini India, kwa wasiwasi wa kuzua, ambao lengo lake kuu ni kupanua mgawanyiko kati ya Waislamu na Mabaniani. Hii ni kupitia kueneza vitisho ndani ya Mabaniani vya Waislamu, huku wakiwahangaisha Waislamu.

Uvundo mkali wa kupagawa kwa watu wengi bado unavuma kutoka kwa serikali ya Modi, tangu ilipojitwalia mamlaka. Leo inaogopa na kuchanganyikiwa juu ya jinsi itakavyotoka kwenye shimo ambalo imeingia yenyewe. Tangu mwanzoni mwa 2021, maamuzi haya mabaya yalipochukuliwa, kwa msingi wa kukata tamaa kwa Modi na washauri wake. Walishajiisha watu kufuata maisha yao kama kawaida, na kuzingatia kwamba janga la COVID-19 lilikuwa limetoweka kutoka India. Halafu, kuzidisha kwa kihistoria kwa janga hilo kulisababisha India kuzamishwa katika mazishi yasiyokwisha kwa miezi kadhaa. Hii iliilazimu serikali kisha kufanya uamuzi wa kusambaza posho za nafaka kwa kila mtu. Tangu wakati huo, serikali ya Modi imekuwa katika hasara ima ya kusimamisha msaada huu kabla ya upungufu katika uchumi wa India kuwa mkubwa kuliko uwezo wake wa kurejesha, au kudumisha misaada ili rai jumla isikasirike, na kuathiri vibaya umaarufu wa Modi na Chama chake cha Bharatiya Janata.

Serikali iliendelea kuahirisha uamuzi huu. Iliendelea kuongeza muda wa makataa ya kusambaza nafaka na mbolea, hadi wakapita makataa ya uchaguzi, ambayo walikuwa wametanguliza hapo awali. Leo, wakati ambapo ufanyaji uamuzi huu umekuwa usio epukika, Modi, kama ilivyo kwa kila mwanasiasa aliyefilisika, anabonyeza kitufe kile kile anachotumia kila wakati. Anabonyeza kitufe ili kuchochea ubaguzi wa rangi na ugomvi wa kimadhehebu. Hii ikimaanisha kufuata sera za kuwahangaisha Waislamu ili kuwasukuma kujibu, huku wakizindua kampeni za kuwatishia Wahindu kuhusu Waislamu, ili kuwakusanya pambizoni mwa Modi na serikali yake.

Inasikitisha sana kwamba wakuu wa vyombo vya usalama, vilivyokabidhiwa ulinzi na usalama wa nchi na ulinzi wake dhidi ya hatari, wote walikosa kuiona hatari halisi kwa India, walipokuwa wakitayarisha nyaraka zao za utafiti na mapendekezo ya usalama. Hatari halisi kwa India na watu wake ni Narendra Modi na serikali yake isiyo na maono. Modi anaisukuma India kwa nguvu ili India ijumuishwe ndani ya mpango wa Amerika wa kudhibiti, na ikiwezekana kupigana, na China. Wasiwasi mkubwa wa Modi ni kwa Amerika kuitabanni India kama kiwanda chake kipya, ambao ni kuiruhusu kuinuka, kwani ikiwa itakua kiukubwa, itagoma kurudi kuwa nchi inayoendelea kama ilivyokuwa miaka ya 1970!

Ama kuhusu kuituhumu Hizb ut-Tahrir kwa itikadi kali na ugaidi, afisa wa usalama aliyewasilisha uzushi huu kwenye kongamano la New Delhi, ima ana uwezo wa utafiti usiozidi ule wa watoto, au ana chuki dhidi ya Waislamu wa India, huku akiwa bingwa wa uzushi, kama Modi. Kuhusu mpango wa Modi wa kukashifu na kuchochea dhidi ya Waislamu, anatumia, pamoja na chuki yake ya kipofu, mpango wa wakoloni, wakiongozwa na Amerika. Inampa kifiniko cha kisiasa ili kuzuia Uislamu usiingie madarakani, kwa kuhofia kwamba watu wanaodhulumiwa, wanaoishi maisha ya ufukara na dhiki chini ya ubepari, wataongozwa na Uislamu, ambao unahakikisha haki kwao. Kisha, watu hawa watageuka dhidi ya walafi, huku wakidai kuhukumiwa kwa Uislamu, kama itikadi ya kisiasa na mfumo wa maisha.

Kwa wale wenye Akili nchini India, kwa jumla, na kwa Wasimamizi wa Taasisi za Usalama, haswa:

Modi na serikali yake ni tishio la kweli kwa mustakabali wa India na watu wake. Wako tayari kuitupa nchi motoni, ili tu wabaki madarakani. Vipi kuhusu mwitikio wao wa hivi majuzi kwa makala ya filamu, yaliyopeperushwa na BBC kuhusu nia ya Modi ya kuizamisha mitaa katika machafuko na umwagaji damu? Wako tayari kufanya lolote ili kudumisha mamlaka, ikiwa ni pamoja na kujisalimisha kikamilifu kwa Amerika, ili kupata idhini yake ya kisiasa. Ndio maana tunakuiteni muuzuie mkono wa Modi na serikali yake iliyopitiliza, kabla hamujachelewa. Pia tunakualika muwe na ikhlasi katika kusoma kile Hizb ut Tahrir inachokilingania. Iwapo Uislamu utatekelezwa kwa mujibu wa Njia ya Utume, kama vile Hizb ut Tahrir inavyoufanyia kazi, basi utaleta kheri, ndani ya mtu binafsi pamoja na jamii, kuwainua wote kwa pamoja kwa viwango vya juu zaidi vya maisha. Raia katika dola ya Kiislamu ni wote ni sawa, hakuna tofauti kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Uislamu tayari umeshatekelezwa kwa zaidi ya miaka elfu moja, ambapo sifa za Waislamu hazijabadilika, kuhusiana na kujali neema, kuepuka uzinifuh, usafi, kuhifadhi heshima, upole kwa wanyonge, na uadilifu miongoni mwa raia wote. Waislamu wanajua kwamba Mwenyezi Mungu (swt) amewatuma kuwatoa watu katika giza la ukafiri na ushirikina, kuwapeleka kwenye nuru na uadilifu wa Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[الر كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ]

Alif Lam Ra. (A.L.R.) Hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha kwako ili uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye muwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifiwa [Surah Ibrahim 14:1].

Mhandisi Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu